Hali ya maisha Ethiopia Inasikitisha sana, vibaka wanavamia nyumba za watu kuiba chakula

ukiona nchi vijana hawaangaiki hata kutoka kwenda kukimbia nchi nyingine tena katika kipindi hiki cha utandawazi ujue hapo kuna amani na fursa..ndio tanzania hii sisemi kama tupo 100% peacefull hapana kinachotusumbua watanzania ni kutaka kuwa na maisha flani hivi standard na yanapatikana kama unapambana kweli tofauti na nchi za wenzetu kabisa wanamaisha ya ajabu serikali inawatenga ukanda flani kabisa kisa tofauti ya kikabila au dini au koo haiwajui kwa chochote..

kwa hapa tz sehemu ambayo ingeleta shida kwa mambo ya ukabila na ukanda ni unguja na pemba lakini cha ajabu serikali ya ccm ingawa mara nyingi kama si zote inakosa ushawishi wa kisiasa pemba ila maendeleo na miundombinu mbalimbali vinaendelea kujengwa sawasawa na unguja ndio maana unaona wapemba kadri muda unavyoenda wanazidi kutambua kuwa siasa kumbe sio uhadui.

ukweli ni kwamba nchi nyingi za afrika na duniani zinatakiwa zije kujifunza utawala bora hapa tanzania kutawala nchi yenye watu wa dini na makabila mbalimbali na wakaishi kwa amani na umoja kama ndugu si mchezo ..MUNGU awabariki viongozi wa ccm hasa waasisi wake ndicho ninachoweza kusema.
Tza ukiwa na akili iliyochangamka huwezi kufa njaa
 
N
Oromo wengi wao ni wasomi sana na maprofesa ila washamba.
Ni Ile chuki tu kwani washamba kwa kigezo gani ama wao ndio wanaitoa standard za ushamba na ujanja.
Shida ni kujiona nyie ni Bora kuliko wengine na kuwadharau.afrika ukabila unatumaliza. Yaani tutagawanyika mpaka Kijiji kitakuwa nchi
 
Ethiopia noma umeme unakatika na kuwaka unakatika then unawaka tena, vita ni kitu cha hovyo kuwahi kukijua
 
WaTigray ni wachache ila ni wafanya biashara mashuhuri sana na wana hela nyingi na mali.
Ndio wanaowatukana wenzao kuwa ni masikini na babu zao hawakusoma walikuwa wanachunga ng'ombe na kucheza ngoma.
Wanajiona wao wenyewe ndio wanaostahili kuila keki ya Taifa Ila wengine ni washamba na malimbukeni.
Saivi wengine wamesoma wanaumia Sana
 
Mzuka wanajamvi!

Wa Ethiopia wengi walioko nje Diaspora wanapitia wakati mgumu sana kwasababu ya ndugu zao nyumbani wanayopitia.

Sasa hivi wengi hawajui kama ndugu zao wako hai au wamekufa. Simu zao hazipatikani wala kwenye mitandao ya jamii hawaonekani.

Hali imekuwa ya sintomfaham sasa hivi Addis Ababa. Wale wenye uwezo ndugu zao wako ulaya wanawatumia hela wananunua vyakula kwa jumla 'panic buying'. Licha ya kununua vyakula kwa jumla wananunua kwa kujificha usiku au gizani kwasababu watu wakikuona watakuvamia kwako na kuiba chakula chako.

Addis Ababa sasa hivi imejaa watu waliotoroka kutoka majimbo mengine kwenda kwa ndugu zao kwaajili ya usalama wao. Katika nyumba yenye chumba kimoja na sebule wanaishi watu siyo chini ya saba.

Juzi kati hapa kazini marafiki zangu wa Ethiopia mmoja mtigray na mwengine Amhara walipigana kisa tofauti zao kikabila. Lakini ukiwaonaga kwa sura wanafanana tu kuwatofautisha ni ngumu.

Ila katika uchunguzI wangu wanawatambua WaTigray kwa majina na kitambulisho. Vilevile wa Oromo.

Nimekaa nao hawa watu nakuwahoji sana tukiwa kazini kwa muda mrefu.

Oromo wengi wao ni wasomi sana na maprofesa ila washamba. Yani wanaitwa watu wa porini barbaric. Muoromo anaweza kujenga nyumba akaipaka rangi ya kijani pinki njano toka kwenye paa ukutani hadi chini. Muoromo wanadai hajwajui kuwa smart hata kwa mavazi licha ya hata akiwa amesoma sana. Wan ile inferiority complex. Wakowako kivyako vyao hadi wameanzisha benki zao.

WaTigray ni wachache ila ni wafanya biashara mashuhuri sana na wana hela nyingi na mali. Majumba na maghorofa mengi Addis Ababa yalikuwa yao ila yote wameporwa sasa hivi. Wana madharau sana nakujiona juu.

Hii chuki imedumu miongo na miongo. Mungu asipoingilia kati kutatokea uchinjaji wa aina yake.

Nitawaletea uzi mwengine kutoka Cameroon maisha yao na uhasama.

Source simulizi za wa Ethiopia wenyewe nafanya nao kazi.
Na hao wanaokamatwa Tanzania wazamiaji kwenda Afrika kunisini ni kabila gani?
 
Ndio wanaowatukana wenzao kuwa ni masikini na babu zao hawakusoma walikuwa wanachunga ng'ombe na kucheza ngoma.
Wanajiona wao wenyewe ndio wanaostahili kuila keki ya Taifa Ila wengine ni washamba na malimbukeni.
Saivi wengine wamesoma wanaumia Sana
Wanajiita ukoo wa malkia Sheba (Sabaaa)
 
ukiona nchi vijana hawaangaiki hata kutoka kwenda kukimbia nchi nyingine tena katika kipindi hiki cha utandawazi ujue hapo kuna amani na fursa..ndio tanzania hii sisemi kama tupo 100% peacefull hapana kinachotusumbua watanzania ni kutaka kuwa na maisha flani hivi standard na yanapatikana kama unapambana kweli tofauti na nchi za wenzetu kabisa wanamaisha ya ajabu serikali inawatenga ukanda flani kabisa kisa tofauti ya kikabila au dini au koo haiwajui kwa chochote..

kwa hapa tz sehemu ambayo ingeleta shida kwa mambo ya ukabila na ukanda ni unguja na pemba lakini cha ajabu serikali ya ccm ingawa mara nyingi kama si zote inakosa ushawishi wa kisiasa pemba ila maendeleo na miundombinu mbalimbali vinaendelea kujengwa sawasawa na unguja ndio maana unaona wapemba kadri muda unavyoenda wanazidi kutambua kuwa siasa kumbe sio uhadui.

ukweli ni kwamba nchi nyingi za afrika na duniani zinatakiwa zije kujifunza utawala bora hapa tanzania kutawala nchi yenye watu wa dini na makabila mbalimbali na wakaishi kwa amani na umoja kama ndugu si mchezo ..MUNGU awabariki viongozi wa ccm hasa waasisi wake ndicho ninachoweza kusema.
Amina,na sisi CCM tunasema,

Inshallah ALLAH atuongoze tuepuke majaribu ya kuvuruga kizuri tulichokuwa nacho (Amani).

Wabilahi Tawfiq.
 
ukiona nchi vijana hawaangaiki hata kutoka kwenda kukimbia nchi nyingine tena katika kipindi hiki cha utandawazi ujue hapo kuna amani na fursa..ndio tanzania hii sisemi kama tupo 100% peacefull hapana kinachotusumbua watanzania ni kutaka kuwa na maisha flani hivi standard na yanapatikana kama unapambana kweli tofauti na nchi za wenzetu kabisa wanamaisha ya ajabu serikali inawatenga ukanda flani kabisa kisa tofauti ya kikabila au dini au koo haiwajui kwa chochote..

kwa hapa tz sehemu ambayo ingeleta shida kwa mambo ya ukabila na ukanda ni unguja na pemba lakini cha ajabu serikali ya ccm ingawa mara nyingi kama si zote inakosa ushawishi wa kisiasa pemba ila maendeleo na miundombinu mbalimbali vinaendelea kujengwa sawasawa na unguja ndio maana unaona wapemba kadri muda unavyoenda wanazidi kutambua kuwa siasa kumbe sio uhadui.

ukweli ni kwamba nchi nyingi za afrika na duniani zinatakiwa zije kujifunza utawala bora hapa tanzania kutawala nchi yenye watu wa dini na makabila mbalimbali na wakaishi kwa amani na umoja kama ndugu si mchezo ..MUNGU awabariki viongozi wa ccm hasa waasisi wake ndicho ninachoweza kusema.
Umeongea ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom