Hali ya maisha ya Mtanzania ni ngumu sana. Rais asipochukua hatua sasa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi

Hali ya maisha ya Mtanzania ni ngumu sana. Rais asipochukua hatua sasa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
655
Reaction score
1,069
Ee Mungu nipe hekima yako niweze kuandika kitu kitakacho weza kuwapa uwelewa viongozi wenu juu ya hali ilivyo mbaya kwa wananchi wake πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™.

Awali ya yote Samia mama naomba elewa hali za Watanzania ni mbaya sana na inatisha kweli kweli 😭😭😭. Tujiulize sisi kama taifa tumemkosea wapi Mungu na je viongozi wetu hamuoni jinsi wananchi wanavyo teseka.

Ukitaka kujuwa udhaifu wa mtu mtese usimpe chakula nyie kama viongozi juu ya hili mmeliweza wananchi hawana chakula kabisa.

Swali la kujiuliza Mama hivi kweli shilling 10,000 haitoshi kabisa kwa bajeti ya siku kwa familia mfano mdogo tuu, nikuonyeshe mama;

Familia yenye watu 5 tu baba mama na watoto 3, Asubuhi baba aache 10000

~ Asubuhi wanunue vitafungwa tu 2,000, watoto wapewe nauli za shule 1000Γ—3=3000 hii ni nauli pamoja na hela ya kula shuleni. Mchana mama haha chochote labla mama amejikaza kanunuwa mihogo ya 1000 na bibi nyingi akala.

Mfukoni imebaki 4000 je, hii hela itatosha kwa chochote kile ila waweze kula jioni?

~ Mchele kilo ni 3,500.
~ Mafutaa pishi ni 500.
~ Mkaa 2000.
~ Mboga za majani 1000.
~ Nyanya +karoti + kitunguu 2000.

Je, swali kwenye Ile 10000 baba alio acha asubuhi imebaki shingapi?

Naomba ujue kitu kimoja mama watu wanaoumia juu ya huu mfumuko wa bei ya chakula ni wananchi wa chini sio wa juu 😭😭😭😭.

Je, wewe kama Rais unawaza juu ya hili? Just imagine wewe unatumia shingapi kwa siku juu ya chakula, jaribu kuchukua 10000 halafu ujaribu kuibajetia kama itatosha kwa chochote kwanzia asubuhi hadi jioni.

Ushauri wangu; huu ni muda muafaka wa serikali kusitisha kuuza nafaka nje. Mama naomba achana na Bashe kabisa, huyu ni mfanyabishara mkubwa wa mahindi Kenya na wewe unalijuwa hilo.

Toeni yale mazao yaliyopo kwenye ghala la taifa yauzeni kwa bei nafuu maana hali ni mbaya mtaani huku. Wekeni mikakati ya kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwapa vijana mikopo wakalime ili kukabiliana na hili tatizo la njaa siku za mbeleni huko.

Ukiendele kufubaza shingo juu ya hili nililo kuambia tutakumbana na baa la njaa ifikapo mwezi wa 6 mwaka huu. Pia angalia mishahara ya watanzania sio rafiki kabisa na Hali ya uchumi ilivyo

Una mlipa mtu 300000 kwa mwezi huyu mtu kulingana na hesabu ya siku anapokea 10000 hapo bado hajalipa Kodi, NSSF anabakiwa na shingapi hapo lakimbili na nusu je hiyo laki mbili na nusu itatosha kumwendesha maisha kwa mwezi mzima embu fikirieni juu ya hili.

Boresheni mishahara kwa sector zote private sector hawajaongezewa hela hadi saa hizi, ina maana hawa sio Watanzania. Je, gharama za maisha zimepanda kwa wafanyakazi wa serikali tuu?

Mnakwenda kutengeneza kizazi ambacho ni hatari sana kwa hili taifa. Hakuna ajira kwa vijana na wanao hitimu ni wengi, je, nini kinaenda kutokea hadi ifikapo 2035?

Sina mengi ya kuyasema zaidi ya hayo kwa unyenyekevu mkubwa na shukuru mwenyezi Mungu kwa kunifungulia haya na kuyaona na kukueleza Mama nimekuwa mnyenyekevu kwako kwaajili ya Watanzania wote πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™.

Kingine japo sio cha mwisho angalia Mama swala la vifurushi vimekuwa ni hatari sana.

Shilingi elfu moja unapata MB 490 Mama hii sio haki kabisa, Nape ni kidonda katika hii wizara, haiwezeka kuwa hivi. Mnawanyosha sana wananchi wa chini, SEMA neno moja juu ya hili swala na hakika utarejesha matumaini kwa wananchi wa hali ya chini.

πŸ™πŸ™πŸ™
 
Ee Mungu nipe hekima yako niweze kuandika kitu kitakacho weza kuwapa uwelewa viongozi wenu juu ya Hali ilivyo mbaya kwa wananchi wake [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Nadhani auwajui Watanzania, hii inabaki tu kama hadithi uliyoisimulia siku ya leo.

Na bi samia na ccm yake wala hawajali na hawana hofu kwani wanatujua hatuna mpango wa kudai haki zetu dhidi ya haya maumivu.

Umeibaini standard ya hiyo elimu watoto wanayoifuata?? Ni uchafu mtupu, ndio huo unaotupa div4 na zero kwa 80%, na km hatuko tayari kutoka nje kuwaeleza watawala juu ya matendo na uovu wao dhidi yetu basi tutulie makalio yakiwa juu ili sindano zituingie haswaaa.

Overrr
 
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa, wahenga walisema. Tuombe tu Mungu, mvua za masika zinyeshe maskini tuweze kujipatia chakula chetu.

Pia kumbuka damu ni nzito kuliko maji, huyo bwashee hawezi kufunga mipaka wakati ndugu zake hawana chakula. Sana Sana atawahimiza waje wakati wa mavuno, waingie mpaka huko vijijini ndani ndani wakusanye shehena ya kutosha na wasafirishe makwao.
 
Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
 
Ee Mungu nipe hekima yako niweze kuandika kitu kitakacho weza kuwapa uwelewa viongozi wenu juu ya Hali ilivyo mbaya kwa wananchi wake...
Bro unapigia mbuzi gitaa una hoja nzuri sana.

Hapa tegemea kejeli na shombo za kuambiwa mfumuko wa bei ulaya ni mkubwa kuliko Tanzania.

Kiufupi Samia alifail from day one japo kuna watu hawataki kuamini ni Raisi asiyekuwa na msimamo wala Dira.
 
Gharama za maisha zimepanda ni matarajio yangu serikali ingekua imeshapeleka muswada wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Na ni mategemeo yangu bajeti mpya itakwenda kuongeza mishahara na kima cha chini
Kosa walilofanya walitangaza mapema kiwango cha mishahara mipya mwaka jana,so wafanyabiashara wakawahi pandisha bei kabla,walipokuja kuongeza wakaongeza mshahara mbuzi.

Bora wasingetangaza
 
Hapo Kuna cost tele hujaeka
Mchele 1kg 3500
Unga nusu 1000 mchana
Mboga walai 2000
Nyanya 500
Kitunguu 100
Mafuta 500
Mkaa 1000
Sukari 400

Maji 500
Umeme 700
Vifafunwana 1000
Nauli ya watu 4 @4000
Beki tTu 3000 per day
Matunda wanahimi,a tule 2000
Buku ya mwalimu 1000
Mboga join 4000
Pango 3000 per day
Dawa ya viatu 200 daily
Mswakin200
Mafuta ya kujipaka 100


Sabini 400 daily hapa unapata 29000*30=
870000
Halafu mtu salary haifiki hat 400000
 
Back
Top Bottom