Mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako.
Inaelekea ni mtu safi sana kwa maneno yako tuu unaweza kujua wewe ni mtu wa namna gani..
Mkuu kwa sasa kama kijana ambaye najitafuta kwa hapa dar ni sehemu sahihi kwangu...
Ila sasa likija suala la nimejipata nina source permanent ya kupata pesa hapo jicho langu lita focus moja kwa moja mikoani.
.ila kwa sasa acha nipambane maana nishatake risk
Kama wewe bado kijana bado una muda mwingi wa kupambana endelea kukaa hapo kama unaona kuna michongo mizuri. Uzuri wa dar mzunguko wa hela ni mkubwa sana sasa wewe pima maji kina chake kwanza mimi nime graduate mlimani miaka 32 iliyopita enzi zile tulikuwa na dhana kuwa mtu ukiwa na degree huwezi kwenda mikoani.
Kuna mikoa ambayo ilikuwa inaonekana ukienda huko hutoboi lakini leo hii waliofika kule pengine walikuta watu wamelaa wakajichukulia maviwanja sasa ni ma taita. Wachaga hapa ndipo wanapo wini
Sasa mdogo wangu usikate tamaa MUNGU wakati mwingine ili akupe kitu kizuri anakupitisha kwenye majaribu makubwa mno mwisho ndio anafungua milango yako Ona wana wa Israeli walivyoteseka kwa miaka 400 misri na safari ya kurudi kwao walitumia miaka 40 japo Israeli na Misri ni karibu mno.
Kuna mwanasayansi mmoja Albert Eistein alipata kusema mtu ambaye anaogopa kukosea akifanya jambo basi mtu huyo hajajaribu kitu chochote.
Mafanikio ya mtu huwa hayapimwi kwa alivyo vizuri kwa sawa ila ni kwa ni changamoto gani alizipitia na akapambana nazo akafanikiwa.
Nikupe mfano mtu aliyepata utajiri wa ghafla sana kwa ufisadi na akafanya mambo mazuri kiukweli huyo hajafanikiwa chochote aliyefanikiwa ni yule aliyeanzia chini kabisa na uelewe utajiri wa haraka ulio na mashaka unaporomoka kwa haraka sana maana sio halali.
Hivi unajua Bakhresa ameshawahi uza magazeti na pia ameshawahi uza ice cream kwenye baiskeli?
Hivi unajua marehemu Reginald Mengi kiwanda chake cha kwanza alikifungua na mke wake kutengeneza kalamu chini ya mti nyumbani kwake na mke wake wino walikuwa wanavuta kwa mdomo.Hizi kalamu tulizitumia tukiwa std7 mwaka 1978.
Hivi unajua tajiri warren Buffet Marekani ameshawahi kuuza magazeti?
Erick Shigongo nimeshawahi soma historia yake aliandika ameshawahi kulala kwenye ma benchi nje alivyoingia dar alikuwa na taaluma ya medical lakini kumbe mungu alijua ana talent ya Uandishi.