Ni heshima na uwajibikaji.
Huwezi kumkosea heshima raisi wa nchi halafu uviheshimu vyombo vya ulinzi na usalama.
Vivyo hivyo huwezi kuvidharau vyombo vya ulinzi na usalama na kisha umheshimu raisi wa nchi.
Heshima kwa amiri jeshi mkuu huenda sambamba na heshima kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Uwajibikaji kwa vyombo vyetu khasa polisi ni kwamba haupo na wote wapo kazini kujilimbikizia mali na kuwabambikia kesi watu au kupora mali zao (uporaji wa mali za wamachinga wakti wa usiku).
Pengine (si wote) hao wahalifu wote ni ndugu, jamaa na marafiki wa askari wetu wa polisi, megereza na vyombo vingine vya ulinzi.