Chinu Mkodoli
Member
- Apr 8, 2024
- 17
- 23
Habari za muda huu wana JF,
Licha ya kuwepo kwa mvua nyingi na vyanzo vingi vya maji katika mkoa wetu huu wa Mbeya lakini maeneo mengi yamekumbwa na ukosefu mkubwa wa maji.
Kwakweli hali ni mbaya, mfano, hapa mtaani kwangu ni kama mwezi hivi sasa hakuna maji na kama yakitoka basi hutoka usiku sana na speed huwa ni ndogo mithili ya mkojo wa paka.
Maeneo ya Airport, mtaa wa nyuma wa chuo cha TIA, kuzunguka Mzumbe na maeneo mengine mengi hali ya upatikanaji wa maji si nzuri.
Kwa sasa tunategemea maji ya mvua na maji ya visima ambayo si salama kwa afya zetu.
Najiuliza kama upatikanaji wa maji utakuwa hivi, itakuwaje kipindi cha kiangazi?
Nashangaa sana sehemu kama Mbeya kuwa na shida ya maji kwa kiwango hiki lakini cha ajabu sijawahi kusikia kiongozi yeyote akisema lolote kuhusiana na hali hii.
Ni kama jambo la kawaida tu na hakuna mtu yeyote anayestuka. Au labda sehemu iliyoathirika na uhaba huu ni ndogo kiasi kwamba hata viongozi wameshindwa kugundua tatizo? Lakini sehemu nyingine pia wanalalamika sana kutopata huduma hii.
Ni kama tupo katika dilemma kwasababu hatujui huduma hii itarudi lini.