Hali ya zao la Korosho sokoni

Hata kwa mkulima hamridhishi kwasababu ukipga gharama za uuandaji na hyo bei anatapa kiduchu sana
Hiyo bei kwa wakulima wenyewe sio mbaya, ndio bei wanayouzia, ila kwa wale wachuuzi wa kuungaunga (kambangwa) imekula kwao mwaka huu.
 
Hata kwa mkulima hamridhishi kwasababu ukipga gharama za uuandaji na hyo bei anatapa kiduchu sana
Uko sawa,mkulima hapa ataumia hasa anapopiga hesabu ya gharama alizozitumia na kile anachokipata,serikali iwaangalie hawa wakulima wa hili zao kwa jichio la pili...
 
Daaahhhh mpk natak kujihc nina nuksi yan nimeivest about mil 2+ kweny kukodi na uendeshaji wa mashamba yangu nikiangalia harvest hailizishi na bado nao wa mnada bei yake inazd kunichanganya akili tuu yan daaahhhhhhh it pains me much now maeneo ya kibiti na jaribu mpakan na baadhi ya maeneo ya pwani hapo aiseee badoo wanazipandisha tuu hope now watakuwa wameshusha dadekiii
 
New update
Kwa mara nyingine Leo Oct 23 wakulima wamegoma kuuza Korosho zao kwenye mnada wa pili uliofanyika Wilayani Nanyumbu(MAMCU)..Bei ya juu imeporomoka hadi Tsh 2520 kwa kilo na ya Chini Tsh 2000.

Jana wakulima waligomea pia mnada wa kwanza..Bei ya Juu ilifikia 2717.
 
Hao wakulima niliwashangaa sana. Sasa bei inaweza kushuka zaidi.
 
Duh halafu tatizo bei ikianza kushuka huwa inashuka zaidi
 
Leo ni tarehe 24 mkuu!! au unareport news za jana?
 
Nenda kapime HIV
Ukimwi sio wa kuuogopa kiivyo! Wanausalimika wasiojua kusahau.

Nikirudi kwenye mada:-
Nilichoki quote kimepostiwa leo tarehe 24 rejea kisha uombe msamaha hadharani.
 
Leo tarehe 24/10/2018 umepigwa mnada mkoa wa Lindi ndani ya wilaya nachingwea katika chama kikuu cha RUNALI (Ruangwa,Nachingwea na Liwale) bei ya juu ni 2656 na bei ya chini ni 2200 ,nako wakulima wamegoma!!!!

Hivi wakishagoma kinafuata nn??
 
Issue kubwa iliyosababisha haya yote ni demand na supply basi ukielewa hayo unatulia tu

Kuna jamaa yangu alitaka naye kujiingiza kwenye hii biashara msimu Huu nadhani akizisikia hizi habari hatathubutu

Msimu uliopita ambao ulikuwa mzuri na bei juu ilitokana na uhaba wa korosho duniani huenda giants wa ulimaji wa korosho hawakuwa na msimu mzuri na supply yao ikawa ndogo hivyo kukawa na demand kubwa kufil gap lao hapo lazima bei ipande na kwa kuwa Tanzania tulikuwa nayo walikuja kununua huku kwa bei kubwa kwa sababu ilikuwa inalipa na wakulima wetu wakapata super normal profit hii profit iliwaattract wengi inawezekana hata walioacha kulima walilima na Wafanyabiashara wengi nao wakajiingiza huko wakitegemea nao watafaidika msimu huu

Kinyume chake msimu huu kwenye soko la dunia korosho imeshuka bei simply because walimaji wakuu wamekuwa na mavuno mazuri na hivyo supply yao imekuwa kubwa sana na hivyo demand imeshuka lazima bei nayo ishuke na itaendelea kushuka tu hata wale waliokuja kununua msimu uliopita hawawezi kuja maana korosho ipo ya kutosha kwa hiyo watabaki Wafanyabiashara wa ndani tu ambao nao hawawezi kununua yote na hivyo wakulima na Wafanyabiashara wategemee normal profit tu

Kwa hiyo wao wauze tu wasitegemee bei itapanda
 
Wanasiasa huwa hawaambii ukweli wakulima mfano RC wa Mtwara anadiriki kuwasifia wakulima kwa kukataa kuuza korosho. Jambo la kujiuliza yeye hakuwepo wakati inapagwa bei dira ambayo ni bei iliyokokotolewa kulingana na gharama za uzalishaji wa korosho katika mwaka husika. Yote kwa yote wakulima watazidi kulia watapoambia bei kila siku yazidi kushuka kutokana na uwepo wa korosho nyingi duniani huku idadi ya walaji haijaongezeka kwa sana.
 
Just imaging west africa watu wamenunua korosho zikawatosha,mpaka zingine wameacha....!!!!

Vietnam ambapo kuna makampuni makubwa ya kubangua korosho, kuna big giant company zimefunga viwanda kwa sababu mbali mbali.

Soko lote la comodities limedorora sana mwaka huu...
 
Fanya networking na watu unaowafahamu.After that, it means mtandao wako utakuwa na channel ya kazi.
 
Kama wameanza kununua West Africa ina maana korosho yetu siyo first priority kwao ukilinganisha na zingine,

Kwa hiyo tuna kazi pia ya kuifanyia market korosho yetu ili when it come to choice kwa buyers waifikirie kwanza wizara inatakiwa ya kilimo inatakiwa kulishughulikia hili

Lakini kwa hali ilivyo sasa wakulima ili hali isije kuwa mbaya zaidi wakashangaa wanauza kwa bei ya chini zaidi kuliko ya sasa ni bora wakaiuza tu wasijekudhani bei itaimarika huko mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…