Hali yangu baada ya kujibiidisha na kusoma na kufuatilia makala za kifalsafa

Hali yangu baada ya kujibiidisha na kusoma na kufuatilia makala za kifalsafa

Miguel Felix Gallardo

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2024
Posts
2,841
Reaction score
5,218
Habari wanajf.

Najihisi kuwa na furaha na amani tele.Nimejikuta ninaOVERCONFIDENCE hatari mbaya kabisa😀😀😀.

Sielewi ni kwanini ila nametokea kuwa mpenzi wa makala na maandiko ya wanafalsafa wale watukutu,RADICALS.

Baada ya kukutana na vitu ambavyo nimekuwa najiuliza maswali na kukosa majibu sahihi au hata kukosana na jamii yangu maana wengi wao nilikuwa nikiwauliza hayo maswali magumu wanakosa majibu na badala yake wananizodoa na kunikataza nisipende kuhojihoji.

Sasa baada ya kusomasoma na kuwa mchimbaji wa U-TUBE kwa muda sasa nimejikuta napata majukwaa ambapo mada zile ngumu kumeza zinajadiliwa bila chenga.Nimejikuta addicted hatari fire🔥🔥🔥.

Nifuraha iliyoje kujikuta mawazo yako yanashabihiana na wanafalsafa WATUKUTU na waliopingwa muda mrefu ila walikuja kukubalika baadae sana na jamii za wenye akili timamu.

Hawa wakulungwa wamenifuta ujinga na kunibadilisha haswa kiasi kwamba nimekuwa najiogopa maana KNOWLEDGE niliyoipata kutoka kwenye hivi vichwa inamizani mizito hata PhD za wasomi wa bongo ni takataka tupu.Takataka over!!!!😀😀😀

Kijana kama bado kunamaswali yanakusumbua kuhusu hii dunia na vilivyomo basi anza na hawa WAKULUNGWA;

1. BAROUK SPINOZA( KATAA DINI )- huyu mwamba atakufunulia ufunuo wa kweli🙏😀

2.ATHUR SCHOPENHAUER(KATAA NDOA KINDAKINAKI)-Huyu COMRADE atakupa ukweli wote,mbivu na mbichi kuhusu ndoa kuwa utapeli.Na mapenzi ni game kama game nyingine tu.

3.NICOLLO MACHIAVELI(MZEE WA MBINU ZA KUITAWALA DUNIA)-Huyu atakuivisha kwenye mbinu za kimafioso za jinsi ya kuwa GURU katika sehemu yoyote na jinsi ya kutawala mazingira na watu wake.

📌Wale wapenda vitabu tafuteni vitabu vya hawa magwiji hamtajutia.Utajutia tu kwanini hukuwajua muda mrefu.

🔥🔥Kwa wavivu ingia U-TUBE wasearch ukipata video zinazochambua mambo waliokuwa wanaelezea nakuhakikishia usipokuwa addicted wewe ni fala!!!

NB:HAKUNA RAHA KAMA KUSOMA NA KUANGALIA DOCUMENTARIES ZA WATUKUTU KAMA HAWA!!!

#KATAA NDOA,NDOA NI UTAPELI!!!

#KATAA DINI,DINI ZOTE NI MIFUMO YA KIUTAWALA!!!

📌LIVE YOUR LIFE,YOUR THE ALFA AND OMEGA.TAKE IT OR LIVE IT GADEMIT!!!!

##PUVU RUKSA!
 
Hiyo knowledge ifanye ikuongezee pesa na hadhi katika jamii sio ujuaji tu. Ukiwa na pesa na hadhi ni rahisi mawazo yako kusikika kwenye jamii.
Wewe masikini sikia:

Bila maarifa sahihi hiyo pesa unayoipambania hutaipata na ukibahatisha kuipata utaipoteza mapema.

Wakati unatafuta pesa,japo kuwa pesa inategwa wanaotafuta huwa hawapati😀😀😀.Hakikisha huachi kuwekeza na kwenye kujinoa kimaarifa.
 
Ulichosoma/jifunza kibadilishe kiwe pesA.....

Hii dunia bila pesa haimuonei kima yoyote yule huruma.... hata uwe na digrii gunia zima !

Wewe msaka tonge endelea kutafuta hela,ila jua maisha ni zaidi ya pesa.

Kama huna maarifa sahihi huwezi kuwa na pesa utaishia kuwa PAID SLAVE!!!

Pesa inatulia kwa wenye maarifa ya hii dunia,kama huna maarifa wewe utakuwa mtumwa wa pesa na itakuzika mapema sana.
 
Ukiwasoma hao wakulungwa ukamaliza ukaongezea na hawa:

1.Marcus Aurelius
2.Seneca
3.Su Tzu
4.Confucious.

Hahahaa hii dunia utaishi raha mustarehe.Yaani utaenjoy sana.Maana vyotee ambavyo leo tumeaminishwa ni starehe ni ubatili mtupu na vyote tulivyoaminishwa ni huzuni ni ubatili mtupu.
 
Wewe masikini sikia:

Bila maarifa sahihi hiyo pesa unayoipambania hutaipata na ukibahatisha kuipata utaipoteza mapema.

Wakati unatafuta pesa,japo kuwa pesa inategwa wanaotafuta huwa hawapati😀😀😀.Hakikisha huachi kuwekeza na kwenye kujinoa kimaarifa.
Upuuzi mtupu.

Utaishia kukariri nawazo ya watu tu na kuwa mjuaji wa kinachoitwa maarifa wakati huna mchango wowote wa mawazo mapya kwenye jamii yako. Tafuta pesa, acha kuropoka kama mwendawazimu.

Mimi sihitaji ushauri wako maana huna jipya. Upo na mawazo ya watu wengine kwenye bichwa lako unahisi una elewa mambo kumbe ni mbumbumbu tu.
 
Wewe msaka tonge endelea kutafuta hela,ila jua maisha ni zaidi ya pesa.

Kama huna maarifa sahihi huwezi kuwa na pesa utaishia kuwa PAID SLAVE!!!

Pesa inatulia kwa wenye maarifa ya hii dunia,kama huna maarifa wewe utakuwa mtumwa wa pesa na itakuzika mapema sana.
Sasa wewe una maarifa gani uliyoweka hapo zaidi ya kuongea vitu ambavyo ni obvious na kutaja majina ya wanaume wenzako.

Vijana kama wewe ndio mnashinda kijiweni kuchambua vita vya marekani kwa taarifa za wamarekani kutoka Google ya wamarekani na kujifanya mnajua kumbe ni hamnazo.

Huna akili. Tafuta pesa
 
Mchawi na mtawala wa yote ni PESA tu kijana, hayo mengine unauchosha ubongo wako bure tu

Anyways ungetupa jina la kitabu angalau hata kimoja tu
 
Na wanapiga stories hizo baada ya kula mihogo ya Jerome huku wamevaa vipensi vifupi, hawana maisha hao
 
Mchawi na mtawala wa yote ni PESA tu kijana, hayo mengine unauchosha ubongo wako bure tu

Anyways ungetupa jina la kitabu angalau hata kimoja tu
😀😀😀yaani mnafurahisha nyie watu maskini wa akili na fikra.

Afterall hiyo pesa huna na hutakuja kuishika.Keep dreaming, hii kanzu kwako ni oversize.

Tafuta mada za siasa na kula kimasihara.Huku panahitaji matured brains sawa bwana mdogo!
 
Back
Top Bottom