Hali za kawaida kiuchumi kwa waganga wengi ni kwasababu wao ni madalali wa majini na wanaotaka fedha, hawataki balaa za pesa za majini

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
FAHAMU MGANGA ANAKUPA UTAJIRI YEYE ANABAKI MASIKINI

Sababu kubwa kuliko zote mganga anajua madhara ya pesa za masharti, kwahiyo hawezi kuhatarisha maisha yake na familia yake.

Ukienda kwa mganga unataka utajiri atachofanya mganga anakuwa kama dalali wa kukuitia majini watakaokupa huo utajiri kwa masharti watakaopanga wao.

Kama unavyojua dalali lazima umlipe kwa kazi anayokufanyia ya kukurahisishia unachokitaka mganga naye utamlipa kiasi chake kwa shida uliyompelekea akuunganishe na wenye nacho.

Mashetanu na majiini hayahitaji malipo ya kumpa mtu utajiri kwa kulipwa riba ya pesa maana wanazo za kutosha, malipo wanayotaka huwa ni muhitaji wa pesa kumuua mtoto wake, kumuua mama yake, kumtia uchizi kaka yake, n.k.

dalali (mganga) anaweza kukuficha hali halisi siku za mwanzo ilimradi apate chake lakoni huko mbele utajua tu hakuna cha bure, ni kama vile dalali atakupeleka nyumba flani ambayo huwa inavuja mvua ikinyesha ila kwakua ni kiangazi hatakwambia ilimradi yeye apate pesa yake utapokubali kuishi hio sehemu utayoiona ipo shwari kwa wakati wa kiangazi, mvua ikianza kunyesha ndio ataanza kujifanya alisahau kukwambia au kujifanya ndio umemjuza, kwa mganga nae mwanzo atakwambia ulete kuku au mbuzi achinje huku akijua kabisa majini hayataridhika na yatahitaji damu hata ya mama yako kama sio kumtia uchizi.

Kuna watu wanalala kwenye majeneza na vitimbi vya kila aina, hata ukirudi kwa mganga kuomba avunje mkataba huwa ni ngumu maana una deni kwa jini na sio kwa mganga, hapo ili umalizane nalo unaweza kuambiwa uue baba yako, mama yako umtie uchizi, mdogo wako umsababishie ajali, ulale na mke wa kaka yako, umuingilie nguruwe, n.k. ili mradi tu kuwekewa ugumu wa kujinasua.
 
Unapataje ujasiri wa kumtoa kafara Mzazi, mtoto ama mtu yeyote yule asie na hatia kisa pesa.

Je unajua ni ndoto za wangapi zitazima baada ya yeye kuondoka???

Hakika duniani kuna watu na binadamu.
 
hakuna cha bure duniani, huwezi kubahatisha kufanikiwa na wala akili na maarifa pekee havitoshi kukupa utajiri.

Unahitaji kiwango flani cha nguvu za kiroho ili ufanikiwe katika mambo yako...Mungu ana masharti yake na shetani ana masharti yake. Binafsi sijawahi Kuwaona walokole matajiri, wengi waliofanikiwa katika dini ni hawa manabii na mitume matapeli tu Ila wale wanaosali Sana ni maskini sanaaaaa.

Ila yote ni ubatili na kujilisha upepo
 
Hivi mafuta ya mwamposa anayapiga sh ngapi mkuu
 
Hakika haya uyasemayo....nikusahihishe tu Majini ni viumbe walioumbwa kwa asili ya moto. Wapo wema na waovu kama vile binadamu tulivyo. Wale waovu ndio huitwa mashetani . Kwahiyo ushetani ni sifa ya kiumbe muovu iwe ni binadamu au jini. Hivyo kuna mashetani ya kijini na mashetani ya kibinadamu. Mfano wa mashetani ya kibinadamu ni yale yanayosema kuwa ili tukupe pesa au mkopo ni lazima uhalalishe mapenzi ya jinsia moja. Hao ndio mashetani wa kibinadamu na mashetani ya kijini ni hayo mfano uliyoyataja yanayokwambia kuwa ili upate utajiri ni lazima uue mzazi au mtoto wako.

Hawa mashetani ya kijini na kibinadamu yote ni mawakala wa ibilis. Lengo kuu ni kuwafanya wanadamu wamkufuru mola wao kama wao (mashetani ) walivyokufuru ili mwisho wa siku wote waende wakaishi ktk moto wa jahannam
 
FAHAMU MGANGA ANAKUPA UTAJIRI YEYE ANABAKI MASIKINI

Sababu kubwa kuliko zote mganga anajua madhara ya pesa za masharti, kwahiyo hawezi kuhatarisha maisha yake na familia yake.

Ukienda kwa mganga unataka utajiri atachofanya mganga anakuwa kama dalali wa kukuitia majini watakaokupa huo utajiri kwa masharti watakaopanga wao.

Kama unavyojua dalali lazima umlipe kwa kazi anayokufanyia ya kukurahisishia unachokitaka mganga naye utamlipa kiasi chake kwa shida uliyompelekea akuunganishe na wenye nacho.

Mashetanu na majiini hayahitaji malipo ya kumpa mtu utajiri kwa kulipwa riba ya pesa maana wanazo za kutosha, malipo wanayotaka huwa ni muhitaji wa pesa kumuua mtoto wake, kumuua mama yake, kumtia uchizi kaka yake, n.k.

dalali (mganga) anaweza kukuficha hali halisi siku za mwanzo ilimradi apate chake lakoni huko mbele utajua tu hakuna cha bure, ni kama vile dalali atakupeleka nyumba flani ambayo huwa inavuja mvua ikinyesha ila kwakua ni kiangazi hatakwambia ilimradi yeye apate pesa yake utapokubali kuishi hio sehemu utayoiona ipo shwari kwa wakati wa kiangazi, mvua ikianza kunyesha ndio ataanza kujifanya alisahau kukwambia au kujifanya ndio umemjuza, kwa mganga nae mwanzo atakwambia ulete kuku au mbuzi achinje huku akijua kabisa majini hayataridhika na yatahitaji damu hata ya mama yako kama sio kumtia uchizi.

Kuna watu wanalala kwenye majeneza na vitimbi vya kila aina, hata ukirudi kwa mganga kuomba avunje mkataba huwa ni ngumu maana una deni kwa jini na sio kwa mganga, hapo ili umalizane nalo unaweza kuambiwa uue baba yako, mama yako umtie uchizi, mdogo wako umsababishie ajali, ulale na mke wa kaka yako, umuingilie nguruwe, n.k. ili mradi tu kuwekewa ugumu wa kujinasua.
Kweli kabisa kwenda kwa waganga ni kuuza uhuru wako!
 
Back
Top Bottom