Ulikuwa umejijengea heshima ndani na nje ya nchi, ndani na nje ya bunge, tambua nguvu na heshima yako ilijengwa na sapoti ya wananchi waliokuzunguka hasa wanachama na viongozi wenzako wa Chadema ambao leo unataka kuwasaliti.
Kumbuka ulipokuwa jela ni wanachadema hawa hawa walikuchangia utoke sikumsikia Ndugai wala Mahera, ulipokamata kura feki ni wana Chadema hawa hawa walikuwa tayari kuumia na wewe, wale wanaokuona shujaa leo hasa wana CCM ndio waliokuwa wanakubeza na kukuzomea, ndio waliokucheka ulipovunjwa mkono na askari magereza.
Halima tambua nje ya umma utabaki Mdee wa kwenye mitandao ni sawa na samaki nje ya maji, alikuwepo Masumbuko Lwamwai akachagua tamaa, alikuwepo Mrema akachagua tamaa, na wewe umechagua njia hiyo.
Watawala wanaokutafuta leo ni kwa sababu uliteka mioyo ya wananchi wakishakunyang’anya hiyo nguvu ya umma kesho watagugeuza geuza kama chapati hutapata mtetezi.
Unashiriki kubomoa chama ulichokipigania kwa damu kwa miaka mingi kwa sababu ya ubunge wa miaka 5, hao watesi wako wa juzi ulioamua kuungana nao sio kwamba wanakupenda sana bali wanataka wakutumie baada ya hapo watakutupa kama mpira.
Uamuzi ni wako, karibu kwenye uwanja mpya wa mapambano, leo Ndugai ni rafiki kesho atakapoanza kukubeza bungeni usifedheheke, wananchi wakakapoanza kukuzomea mitaani ujue ndio njia uliyochagua.
Unafanya makosa lakini bado una nafasi, kama ulikwazika fikiria upya omba radhi kwa wananchi nafikiri watakusamehe.