Ng'wale
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 4,690
- 3,399
Unaijua siasa vizuri na kujua Halima Mdee ni nani katika CHADEMA?Hivi kati ya Wabunge walio teuliwa wa Chadema ni Halima Mdee pekee kwa nini lawama kwa Halima Mdee pekee.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaijua siasa vizuri na kujua Halima Mdee ni nani katika CHADEMA?Hivi kati ya Wabunge walio teuliwa wa Chadema ni Halima Mdee pekee kwa nini lawama kwa Halima Mdee pekee.
Hao Covid hawawezi kukiua chama,wafukuzwe mara moja!Msimtisha bhana, leo mnasahau huyu dada alivunjwa mkono akikipigania chama, leo mnamuona hafai. Mwisho wa chadema kesho kama misimamo yenu ndiyo hii
Hallima Mdee YUKO SAHIHI KABISA.
Baadhi yetu watanzania tunaanza kutoa TAFSIRI isiyo sahihi ya ni nini USALITI KATIKA SIASA.
Mdee Hajasaliti...bali ameangalia MBALI KISIASA.
Zanzibar ni ndogo na waliokuwa wanachama wa CUF kule hawakuwa ni wengi Kama Hawa wa CHADEMA. CUF iliamua KUTOSHIRIKI UCHAGUZI wa mara ya pili kulikopelekea KUKAA NJE YA BARAZA LA WAWAKILISHI KWA MIAKA 5 mfululizo.
[emoji117]Hakukuzuia BARAZA LA WAWAKILISHI KUENDELEA NA KAZI ZAKE.
Bali kulisababisha CHAMA KIKOSE RUZUKU....
Bali kulisababisha WAWAKILISHI wakose "maslahi ya kazi yao walioichagua...".
Tusisahau kuwa SIASA NI KAZI..
Tusisahau kuwa NYUMA YA watu hawa 19 kuna AJIRA NYINGI....je tunataka AJIRA HIZO ZIFUTIKE?!!
Je, tunataka CHADEMA ifukuze WAFANYAKAZI wake nchi nzima kwa sababu ya "ukata" wa Kukosa RUZUKU?
MAMBO HAYA TUYAANGALIE KWA UHALISIA NA KUACHA HISIA.
CHADEMA wapunguze JAZBA kwani "siasa zetu Afrika" hazioani Sana na WENZETU waliokwishakutangulia KIDEMOKRASIA.
Tujikongoje sasa na huko MBELENI nasi TUTAFIKA LEVELS kubwa za KIDEMOKRASIA.
KUCHUTAMA SI UNAFIKI.
KUCHUTAMA SI USALITI
Kamati kuu ya chama haijawapitisha,spika anajua na Mahera anajua!Nini kimetokea mpaka wakaapishwa?Kwanini Mahera na Spika wamekuwa tayari kuvunja katiba na sheria kwa kupitisha watu ambao hawajateuliwa na chama?Kwanini wameshiriki dhambi hii?Eti halima katunukiwa na CCM, kila mtu akivuruga CHADEMA Basi kanunuliwa na CCM, ila akivuruga wa CCM amejitambua hajanunuliwa na upinzani, so sad
Sijui niambie ni nani?Unaijua siasa vizuri na kujua Halima Mdee ni nani katika CHADEMA?
Loooh....Acha kupotosha watu chama kinategemea michango ya wanachama wake hayo mambo ya ruzuku hayo ni ya vyama dola kama CCM.
Kama kuna jambo litakalokiangamiza chama cha Siasa ni pale kitakapoacha wasaliti waendelee kubakia katika chama. Jibu ni moja tu hao wote ni kuwafukuza wameshindwa kuthamini michango yao katika chama kama ni pesa za kuimarisha chama mbona mabeberu wako tayari kutoa wakati wowote kwanini awe na njaa ya hivo kiongozi mkubwa kama huyo.
Binafsi nimemtetea sana katika jimbo la kawe hasa kwenye kata yetu na alipata kura nyingi sana. Ametukosea kiasi kikubwa sana tuliokiwa tunamuamini lakini sasa kwenye Siasa huwa hauhitajiki ushahidi wa mahakamani kwamba mtu anahatia kule kujulikana kuwa amekwenda kuapa bila kufuata utaratibu wa chama na yeye akiwa ni kiongozi amepoteza Sifa ya kuwa mwanachama.
Future ipo chadema? Ulisikia wapi?
Mdee ana uhakika wa ajira ya miaka mitano, mshahara mono na uhakika wa kuinua mgongo!
Alafu hivi ni viti ni nafasi ya wanawake, mbona mma gubu nyinyi
A good and wise appeal. I'm not sure whether it will land on a live ear.Ulikuwa umejijengea heshima ndani na nje ya nchi, ndani na nje ya bunge, tambua nguvu na heshima yako ilijengwa na sapoti ya wananchi waliokuzunguka hasa wanachama na viongozi wenzako wa Chadema ambao leo unataka kuwasaliti.
Kumbuka ulipokuwa jela ni wanachadema hawa hawa walikuchangia utoke sikumsikia Ndugai wala Mahera, ulipokamata kura feki ni wana Chadema hawa hawa walikuwa tayari kuumia na wewe, wale wanaokuona shujaa leo hasa wana CCM ndio waliokuwa wanakubeza na kukuzomea, ndio waliokucheka ulipovunjwa mkono na askari magereza.
Halima tambua nje ya umma utabaki Mdee wa kwenye mitandao ni sawa na samaki nje ya maji, alikuwepo Masumbuko Lwamwai akachagua tamaa, alikuwepo Mrema akachagua tamaa, na wewe umechagua njia hiyo.
Watawala wanaokutafuta leo ni kwa sababu uliteka mioyo ya wananchi wakishakunyang’anya hiyo nguvu ya umma kesho watagugeuza geuza kama chapati hutapata mtetezi.
Unashiriki kubomoa chama ulichokipigania kwa damu kwa miaka mingi kwa sababu ya ubunge wa miaka 5, hao watesi wako wa juzi ulioamua kuungana nao sio kwamba wanakupenda sana bali wanataka wakutumie baada ya hapo watakutupa kama mpira.
Uamuzi ni wako, karibu kwenye uwanja mpya wa mapambano, leo Ndugai ni rafiki kesho atakapoanza kukubeza bungeni usifedheheke, wananchi wakakapoanza kukuzomea mitaani ujue ndio njia iliyo hatua.
Unafanya makosa lakini bado una nafasi, kama ulikwazika fikiria upya omba radhi kwa wananchi nafikiri watakusamehe.
sina wivu nao mkuu. mimi ni mtu mdogo sana labda nionee wivu wadogo wenzangu. Bungeni waende hata miaka 100 lakini kuna utaratibu. Why walazimishe na kuleta taharuki?Yaani kweli mnawaonea wivu wanawake kwenda bungeni kuwatetea wanawake wenzao? ungekuwa wewe kweli ungekataa? Acha wivu aisee.
Mungu anakuona