Katashekadm
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 728
- 775
Usisahau Yuda alikesha na kuomba pamoja na Yesu, lakin mwisho alimsaliti YesuMsimtisha bhana, leo mnasahau huyu dada alivunjwa mkono akikipigania chama, leo mnamuona hafai. Mwisho wa chadema kesho kama misimamo yenu ndiyo hii
Wangeanza kutubu wale ndugu zangu walionajisi uchaguzi na kupelekea yote haya. Usimbebeshe mmojawapo wa waathirika wa uchafuzi huu na ukawaacha wahusika. Nadhani wao kwenda bungeni wameonyesha ukomavu kisiasa. Acha maisha yaendelee mkuu.Mdee alikuwa role model wa wengi.
Ukomavu gan mkuu?Wangeanza kutubu wale ndugu zangu walionajisi uchaguzi na kupelekea yote haya. Usimbebeshe mmojawapo wa waathirika wa uchafuzi huu na ukawaacha wahusika. Nadhani wao kwenda bungeni wameonyesha ukomavu kisiasa. Acha maisha yaendelee mkuu.
Usisahau na yule aliyempiga dole la kundu Ester Matiko.Hivi ilikuwaje polisi hawakuwachukulia hatua?
Hivi ni nani alimvunja mdee mkono?
Hivi ni nani alimbambikia kesi Nusrati?
Hivi ni nani alimuweka matiko ndani miezi 2?
Hivi ni nani aliwaibia mdee, matiko, bulaya na wengine wanawake wengi wa chadema kwenye uchaguzi
Endelea na unafik wako maana ndo unakupa kula
Mkuu imewapa USHAURI mzuri Sana,rudisha kila kilicho Chao, jiondoeni, ombeni msamaha kwa wanachama na chama, mtaeleweka ,vinginevyo mtapotea kisiasa, mtaandamwa na masononeko kwenye nyoyo zenu, mtaanza kujinyanyapaa na Jamii zenu zilizowazunguka nazo zitawanyanyapaa,Ulikuwa umejijengea heshima ndani na nje ya nchi, ndani na nje ya bunge, tambua nguvu na heshima yako ilijengwa na sapoti ya wananchi waliokuzunguka hasa wanachama na viongozi wenzako wa Chadema ambao leo unataka kuwasaliti.
Kumbuka ulipokuwa jela ni wanachadema hawa hawa walikuchangia utoke sikumsikia Ndugai wala Mahera, ulipokamata kura feki ni wana Chadema hawa hawa walikuwa tayari kuumia na wewe, wale wanaokuona shujaa leo hasa wana CCM ndio waliokuwa wanakubeza na kukuzomea, ndio waliokucheka ulipovunjwa mkono na askari magereza.
Halima tambua nje ya umma utabaki Mdee wa kwenye mitandao ni sawa na samaki nje ya maji, alikuwepo Masumbuko Lwamwai akachagua tamaa, alikuwepo Mrema akachagua tamaa, na wewe umechagua njia hiyo.
Watawala wanaokutafuta leo ni kwa sababu uliteka mioyo ya wananchi wakishakunyang’anya hiyo nguvu ya umma kesho watagugeuza geuza kama chapati hutapata mtetezi.
Unashiriki kubomoa chama ulichokipigania kwa damu kwa miaka mingi kwa sababu ya ubunge wa miaka 5, hao watesi wako wa juzi ulioamua kuungana nao sio kwamba wanakupenda sana bali wanataka wakutumie baada ya hapo watakutupa kama mpira.
Uamuzi ni wako, karibu kwenye uwanja mpya wa mapambano, leo Ndugai ni rafiki kesho atakapoanza kukubeza bungeni usifedheheke, wananchi wakakapoanza kukuzomea mitaani ujue ndio njia iliyo hatua.
Unafanya makosa lakini bado una nafasi, kama ulikwazika fikiria upya omba radhi kwa wananchi nafikiri watakusamehe.
Kwa nini atubu na kwa nini chama kisimuache aendelee kuwakilisha watanzania wanyonge