Mabibi na mabwana na hasa wale walio wazalendo. Ni ukweli ulio wazi kuwa maji yakishamwagika huwa hayazoleki. Hata hivyo tunaweza kuganga yajayo.
Ni ukweli usiopingika kuwa, Bi. Halima ni mmoja kati ya makamanda shupavu kabisa walioipigania CDM kwa uaminifu mkubwa, licha ya kupitia katika changamoto nyingi.
Wandugu, kujikwaa si kuanguka na kosa moja halifukuzishi mke!
Siyo siri kuwa, tukio hili lililopelekea mtafaruku huu, limetusikitisha na kutusononesha mno. Kwa hakika itakuwa vyema sana kama tutashirikiana sote kulimaliza suala hili kistaarabu kwa mustakabala mwema wa chama chetu.
Ni furaha iliyo je mbinguni, mwenye dhambi mmoja akitubu?
Msingi wa hoja kama chama ni kutokutambua haramu ya uchaguzi 2020 na yote yatokanayo nao. Huu haupingiki aliye na hoja tofauti na atushawishi kwa hoja. Hiyo ndiyo demokrasia.
"Hapa pana namna ambayo suala hili Bi. Halima, litakwisha na adui yetu akatepeta na kulegea vilivyo:
1.Ombeni radhi kwa dhati kabisa mkijutia yote yaliyotokea.
2. Wekeni wazi bila kuficha kama ni Hadaa, ghiliba, ahadi, vitisho, nk na mkiwaweka wazi wote waliohusika na sarakasi hii. Koleo na likaitwe kwa jina lake.
3. Tuunganeni sote kumshambulia na kumwaibisha mbaya wetu.
4. Mengine kama yatakavyo shauriwa na waungwana wengine."
Sote tu wakosaji, shuruti tuwe tayari kusamehe 7x70.
Hayupo aliyepanga kukufukuzeni. Chonde chonde uamuzi wa kutofika huko mnao pia mikononi mwenu.
Ashindwe mbaya wetu na washirika wake wote.
Washindwe na walegee!