Nina maswali hapa mtaalamu, namba za madeni zilizotajwa humu na hasa kuhusu deni aliloacha JK ni Dollar bilioni 31, trilioni 35, trilioni 41, trilioni 43. Deni linalosemwa leo aliloacha Magu ni trilioni 71.
Mkapa akiondoka madarakani, aliacha deni kiasi gani? Maana nakumbuka nchi kusamehewa deni lote mwaka 2000, kabla ya kusamehewa lilikuwa kiasi gani na kabla ya kukabidhi nchi kwa JK, deni lilikuaje?
Wakati Mkapa anasamehewa deni, tuliambiwa amesamehewa lile deni halisi ila riba ataendelea kulipa, riba ilikuwa kiasi gani?
Je, mikopo iliyofuata haikuwa na riba? Kama ilikuwa nayo, ni kiasi kati ya hayo madeni yaliyorithiwa kutoka utawala mmoja kwenda mwingine?
Kiukaguzi, pesa iliyokopwa, ililingana na matumizi halisi ya sababu ya kukopewa?
Kama wewe au mtaalamu yoyote atanisaidia nielewe kwenye hayo maswali, nitashukuru sana.