Halima Mdee: Deni la Taifa limefika Tsh. 71 trillion, maana yake kila mtanzania anadaiwa Tsh. 1 million na ushee

Halima Mdee: Deni la Taifa limefika Tsh. 71 trillion, maana yake kila mtanzania anadaiwa Tsh. 1 million na ushee

Hizo pesa Trilioni 71 alipeleka kwenya akaunti zake binafsi za uswisi? very poor argument.Barabara zilizojengwa huzioni? umeme kila kijiji huuoni? Elimu bure huioni? Ndege huzioni? Vituo vya afya nchi nzima huvioni? nk wewe kipofu?

Hizo zote ni fedha zetu za ndani, alisikika akijinasbu.
 
Ole wako uje kwangu kunidai hiyo hela! Nakukata panga akyamungu! Tena panga butu,hapa nadaiwa na kikoba,nadaiwa na mama birigita yule wa dukani,nadaiwa na muhindi ninayefanya kibarua kwake,nadaiwa na jamaa mwingine alinipa hela yake nimwekee nikaitafuna,nadaiwa kodi ya banda(nyumba?) Ya miezi saba,nadaiwa hela kibao baba kevi wa pale kilabuni,nadaiwa na muuza maziwa na wengine weeeeeengi kabisa,niacheni,nisije kuua mtu akyamungu

[emoji28][emoji28][emoji28] Huyo muhindi unafanya kazi kwake anakudai vipi, ulichukua salari advansi?
 
Wale wanaotudai wapewe nchi tu waweke CEO wao apige kazi atengeneze faida warudishe chao🤣🤣
 
Deni gani tena!?
Sikumbuki kukopa...wala kukubaliana na mtu achukue hii mikopo mingi inayofanana na mikopo ya chupa za plastic za maji na juice zilizozagaa huko mitaani.

Nachojua benki wameninyima mkopo!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mbunge wa viti maalumu asiyefungamana na upande wowote Halima Mdee amesema kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya February 2021 deni la taifa limefikia tsh 71 trillion.

Hi maana yake ni kama kila mtanzania anadaiwa tsh 1 milion na points.
Mdee alikuwa akichangia hotuba ya mpango wa maendeleo.

Ngoja niitafute hiyo ripoti nijiridhishe.

Ramadhan Kareem!
Pamoja Mshahara wake usio Halali ndio umepandisha hilo deni
 
Ukiona mtu hataki kuambiwa kitu wala kukosolewa, anatesa na kuua bila kujali, analazimisha kusifiwa na kuimbiwa mampambio ni viashiria vya kulinda ajenda zake za kishetani.
Madikteta wote walikuwa hivyo na waliishia kufilisi nchi zao kwa kutumia hazina za nchi zao kama mali zao binafsi, kabla ya Mungu kuweka mkono wake.
Bomba la gesi toka Mtwara na mitambo/magenereta ya kutumia gesi vilivyotumia gharama kubwa sana na vilivyokuwa tayari kabisa kutumika kuzalisha, alivitelekeza na tukaendelea na mgao wa umeme kwa sababu TU havikumuingizia 10%. Bila hata chembe ya aibu akaanza mradi wake mpya.
Wanaoendelea kuimba uzalendo wa huyu mwendazake ni wa kuwatazama vizuri USONI, lazima utangundua alama za ushetani.
Mungu atuongoze na atuondolee mashetani hayo pia
AMEN
Ukweli MUNGU ametusaidia sn
 
Mzee si alikuwa anafanya miradi mikubwa kwa pesa za ndani!
 
Deni la taifa tuna wasomi wajinga sana hawajui kusoma takwimu na kuzitafsiri.Wawaachie wataalamu wa statistics wawape tafsiri.Wachumi wapumbavu tu wao ni kama wahasibu kazi yao kuanandaa vitabu vya hesabu tu mfano wahasibu huandaa financial statements lakini hawawezi ku analyise akiwemo CAG pia wachumi wana uwezo wa kutengeneza nationak accounts lakini wako zero kutafsri hizo hesabu waluzotengeneza

Tanzania inadharau wataalamu wa takwimu na kuwaona hopeless.Lakini ndio pekee wenye uwezo wa kutafsiri takwimu yeyote proffessionally sio wahasibu au wachumi they are zero
Uchumi na uhasibu ni kada mbili tofauti, hicho ulichoita "tafsiri" yaani upembuzi, katika mambo ya uchumi na fedha hufanywa na wachumi. Kwa watu wasiofahamu huhisi ni kama kada moja, lakini si kweli ni kada mbili tofauti
 
Uchumi na uhasibu ni kada mbili tofauti, hicho ulichoita "tafsiri" yaani upembuzi, katika mambo ya uchumi na fedha hufanywa na wachumi. Kwa watu wasiofahamu huhisi ni kama kada moja, lakini si kweli ni kada mbili tofauti
Wengi hujua kuwa wote ni Accountants tu

Wachumi hutengeneza National Accounts na Wahasibu hutengeneza Financial Accounts
 
Mwendazake apewe tuzo bora ya mtia hasara Mkuu.
Yeye ndie ametia hasara kubwa kuliko wote toka enzi ya mkoloni hakuna mfanowe
 
deni la kurith mkuu, hata ukiondoka duniani kizazi chako kitalilipa tu - kweli hii si HAKI kabisa.

Mwendazake alikuta deni la bei gani? na kalifikisha kuwa gani? Maana alituaminisha kwamba kila Project ni HELA ZA NDANI tena cash.
@FUSO anaitwa Mwendazake sio?
Kweli usipostaajabu ya Musa utashangaa ya Firauni


Sent from my V2027 using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa viti maalumu asiyefungamana na upande wowote Halima Mdee amesema kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya February 2021 deni la taifa limefikia tsh 71 trillion.

Hi maana yake ni kama kila mtanzania anadaiwa tsh 1 milion na points.
Mdee alikuwa akichangia hotuba ya mpango wa maendeleo.

Ngoja niitafute hiyo ripoti nijiridhishe.

Ramadhan Kareem!
Kwani yale makinia ambayo yangetuletea zile trilioni za kila mmoja kupata Noah yaliishia wapi? Si yangetumika kulipa hilo deni?
 
Wenye mahekalu na walio kula rushwa wao walipe zaidi,...hatuwezi kulipa hilo Deni sawa na watu wa Mbagala, au kigera Etuma huko sijui Manzese noo!! sisi wenye Magari, Mahelikopita, tunalipa zaidi wastani wa Million 5 hivi!!

hao wa mazogoroni wao walipe laki mbilimbili tu!....au km hawana hizo hela waandike maombi ya kulipiwa madeni yao na wenye uwezo walioko Masaki tu!.... wao watawalipa kidogo kidogo! km wakipata! kipaumbele wapewe wadada, madume yakafanye kazi!

Ili ukuu wetu na heshima zetu, haki za kutawala , kuongea sana zibaki palepale! ......laiti km tutalipa sawa na Maskini!!! Matajiri wengi tutaiaga nchi, na nchi itakufa kibudu, lazima ukuu wetu tuuuishi km ulivo.... mkipinga make wengi bongo mtaolewa na wa-Kenya!

Matajri sisi tunaona raha ya kifahari sana kudaiwa kila mara na Mabenki ya kidunia. kwa maskini kudaiwa ni tofauti sana, atakufa au ku-paralyse mazimaaa!!! lkn sisi matajiri ndo kwaaanza tuna nenepa!! ....

Mtu tajiri akifirisiwa na Bank ndo kwaanza ananenepa!! wanamuachia kanyumba kamoja tu, atakaa weeee humo....lkn anaweza panda tena na hawana aibu anaenda kopa tena kwa Bank ileile, watu wale wale, mahali palepale, masharti yaleyale km mchezo tu anapewa......hii Dunia tofauti sana.
 
Mbunge wa viti maalumu asiyefungamana na upande wowote Halima Mdee amesema kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya February 2021 deni la taifa limefikia Tsh. 71 trillion.

Hi maana yake ni kama kila mtanzania anadaiwa tsh 1 milion na points.
Mdee alikuwa akichangia hotuba ya mpango wa maendeleo.

Ngoja niitafute hiyo ripoti nijiridhishe.

Ramadhan Kareem!
Halima yeye si ana bilioni 10? basi asaidie kulipa deni la taifa
 
Tatizo la wasomi kama mdee ni ujinga .Baadhi ya Vyuo vyetu vinazalisha watu wenye IQ ndogo mno.Wansona deni utafikiri wakopeshaji badala ya kuona vitu vilivyofanywa na hiyo Trilioni 71 imefanya kazi hukua hiyo hela ambayo iko kwenye miradi kamilika au endelea halafu gawia Kila mtanzania kwa hiyo miradi yote ya barabara na majengo nk halaf ujue kila mmoja anamiliki mali ya kiasi gani kwenye ndege zote zilizonunuliwa na barabara zote zilizojengwa ikiwemo miradi ya umeme na hospitali nk

Kuangalia nchi inadaiwa kiasi gani hiyo hasa ni kazi ya mkopeshaji wewe mkopaji unatakiwa kuangalia kilichofanyika ukigawa wananchi wako kila mmoja ana Asset kiasi gani kwa makert value ya sasa

Tatizo la wasomi wetu ni kumeza tu notisi vyuoni logic wengi wako zero akiwemo.Mdee nk huko bungeni ndio maana hadi bungeni akina msukuma na kibajaji ambao ni darasa la saba wanawaporomoshea matusi wasomi mchana kweupe
Kuna miradi hailipi maana yake inatia hasara mfano huo wa ndege, masoko, stend ni miradi return yake ni very minimum saa nyingin hasara kabisa
 
Hizo pesa Trilioni 71 alipeleka kwenya akaunti zake binafsi za uswisi? very poor argument.Barabara zilizojengwa huzioni? umeme kila kijiji huuoni? Elimu bure huioni? Ndege huzioni? Vituo vya afya nchi nzima huvioni? nk wewe kipofu?
Pesa za madini, utalii, kodi, matozo huwa zinakwenda wapi hivi!?
 
Back
Top Bottom