Uchaguzi 2020 Halima Mdee: Gwajima alijaza fomu ya maadili nyumbani kwake badala ya kuja mbele ya msimamizi wa uchaguzi hivyo hana sifa ya kugombea

Uchaguzi 2020 Halima Mdee: Gwajima alijaza fomu ya maadili nyumbani kwake badala ya kuja mbele ya msimamizi wa uchaguzi hivyo hana sifa ya kugombea

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kanuni ya 26(3) ya Kanuni za Uchaguzi zinataka Fomu ya KUTEKELEZA MAADILI kujazwa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi. Ndugu yangu wa CCM KAWE alijaza tarehe 20/8/2020 NYUMBANI kwake. Na BADO MSIMAMIZI wa UCHAGUZI Kinondoni AKAMTEUA!⁩ HUYU Mgombea HANA SIFA-Halima Mdee on twitter.

1598466784934.png
 
Pingamizi za Mgombea Urais CHADEMA (Mh Tundu Lissu) kwa Mgombea Urais CCM (Mh Magufuli).

1) Mgombea urais CCM hakuambatanisha picha ya Passport Size.

2) Wadhamini wake hawaja hakikiwa na TUME, badala yake wamehakikiwa na wasaidizi wa Uchaguzi.

3) Tarehe alizo hakikiwa hazipo kwenye ratiba iliowekwa.

# Jaji Kaijage - Simamia uadilifu na haki kwenye kuhukumu mapingamizi ya wagombea wote. Usiangalie chama wala cheo. Historia itakukumbuka kwa moja kati ya mawili "SHUJAA" au "KIBARAKA".

# Mapingamizi yanatakiwa kujibiwa mbele ya TUME na wakiwepo wahusika wote - Lissu Vs Magufuli.
 
Kwahiyo Halima Mdee ameshaweka pingamizi rasmi ndani ya muda kama sheria inavyotaka au anatuhabarisha tu?

Kisheria, muda wa ku - submit mapingamizi ya ubunge na udiwani ni siku mbili baada ya zoezi la kurejesha fomu na uteuzi kufanyika....

Kwa hiyo kuna siku ya leo J'tano tarehe 26/8/2020 na kesho Alhamisi tarehe 27/8/2020....

Hata akipeleka pingamizi kesho kabla ya saa 10 jioni, ni OK hajachelewa..
 
Sasa atathibitisha vipi aliijaza nyumbani ?Na kama aliijaza akiwa kwa msimamizi wa uchaguzi tarehe hiyo ?Halima Mdee hapa kachemsha.
Kweli wee akili zako ni sawa na kinyesi changu ..fomu ya tamko la mgombea linajazwa mbele ya msimamizi wa uchaguzi siku ya kurejesha fomu ambayo ni trh 25, haya hapo juu kajaza trh 20 ..hv hapo Gwajiboy anaponaje???
 
Sheria zilizo tungwa na wabunge wa Ccm darasa la saba. Sasa zina warudi wrnyewe maana huzipitisha wakiwa usingizini
Hakika mkuu Tanzania ni yetu sote huwa nashangaa kwa nini tunataka kukomoana wakati wote tunajenga taifa moja tatizo tumejaa uchama
 
Daah Ni aibu kubwa Sana kwa Mwanasiasa Nguli Kama Halima kuja kuleta Tatizo la kifundi Kama hili huku mitandaoni badala ya kwenda kuweka pingamizi kwa NEC Kama alivyofanya John mrema kwa Bonna.

Yani muda wa mapingamizi umeisha ndo unasema Hana sifa Ukiwa Kama tume ya uteuzi ama Ukiwa Kama halima mdee.

Unachokitafta kwa huyo gwaji boy soon utakipata Naona unamchokonoa afungue Domo lake,, Kuna yule alikuwa RC wa Dsm aligalagazwa mdomoni vibaya mnoo na huyo gwaji hivyo kuwa makini Sana na huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom