Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Ukiambiwa utoe uthibitisho wowote wa wao kushawishiwa na CCM huna. Hivyo usipende kuongea vitu vya kubuni. Hiyo ni mojawapo wa viashiria vya upungufu wa uelewa...

Acha upotoshaji wa kijinga dogo, watuhumiwa hawakuruhusiwa kujitetea, wakati waliitwa na hawakutokea?
 
Mkuu ufahamu upi niliojitoa? Nani asiyeona kuwa CHADEMA hakuna demokrasia ila uhuni na political mongers wamejazana huko?
Hah hah hah. Eti CHADEMA hakuna demokrasia! Vipi huko CCM wanachapisha fomu 1 tu ya mgombea urais. NdIo demokrasia hiyo! Yaani CCM ukifikiria tu kugombea urais unatimuliwa chama. Muulize Membe!
 
Mbowe ni kiongozi mzuri, tatizo anataka kuwaplease wanachama wachache wa mtandaoni wasiofika hata 500.
Angewaacha hao wamama waende bungeni, lazima uwe flexible katika hii dunia, sio kushupaza shingo muda wote, itavunjika...
 
Chadema walifanya makosa makubwa sana kuwafukuza wabunge wao bila ya kubaini ukweli wa Jambo lenyewe.
Hakuna kosa lolote lililofanyika na hao CHADEMA kutowafukuza uanachama maana yake ni hao 19 waendelee kuwa wabunge maana tayari waliisha apishwa... CHADEMA Haitaki kupeleka vitu maalum ili kutuma ujumbe serikalini, kwenye Taasisi na Bungeni kwamba wizi wa kura haukubaliki.

cha ajabu, system inalazimisha CHADEMA cha kufanya na CHADEMA inafanya kinyume na system inavyotaka...
Kwa nini system iwapangie CHADEMA cha kufanya?

Kuwavua uanachama ni kupotezea ubunge automatically.. kosa ni la akina Mdee kutokujua maamuzi ya chama chao na msimamo wao CHADEMA juu uchaguzi.

System itafanye muafaka na CHADEMA ili nchi iendelee... vinginevyo ni yale yale ya mwaga mboga na ugali pamoja.... hakuna wa kushinda au kushindwa bali ni Watanzania sote...
 
Amekwepa kusema nani aliwaruhusu kwenda bungeni.

Yeye kama mjumbe wa kamati kuu ni kikao gani kilikaa kuwapitisha kuwa wabunge. Nilitegemea kama alivyosema yeye ni chadema na ataendelea kuwa Chadema angetumia taratibu za chadema kupata suluhu lakini kitendo cha kutumia wanasheria kinaleta picha tofauti.
Alitakiwa kuzungumzia kauli ya Ndugai kuhakikisha wataendelea kuwa wabunge.
 
Kwa nini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
 
Du poleni sana makamanda. Ila naona dalili ya cdm kutumbukia dhambini. Maana wamejiuahdi kuhakikisha adamu wa chama anaanguka dhambini wakashindwa sasa wakaona wamtumie eva. Eva akakubali kulila tunda la rudhuku sasa kilichobaki ni kutubu dhambi ili tuweze kuuridhi uzima wa tz.
 
Ila kusema kweli haya mambo tunayakuza zaidi sisi watu mitandaoni....tukiambiwa tuandamane tunatulia kimya...viongozi wanafungwa tupo kimyaaa...ila leo tunawaona hao wanawake kama ndo wasaliti kuliko sisi.

Tuanze kuingia barabarani kwanza kupinga matokeo kisha ndo tuwanyooshee vidole hao wanawake....siyo kusubiri hao wanawake wagome kupeleka viti maalum bungeni ili tuwekewe vikwazo,unakua ni unafiki.

Tuache wayamalize ndani ya Chama kama ikishindikana basi ila tuache unafiki kama hatuwezi ingia barabarani kudai haki zetu na kutegemea hao wanawake wasiende bungeni....kwanza tungeacha waende tu mbona yule mmoja kaenda...wanaume ndo tulitakiwa tuandamane siyo hao wamama.
 
Ukweli ulikuwa upi zaidi ya kushawishiwa na CCM na kuwarubuni. Hawa wadada wakajisahau namna walivyokuwa wanavurumishwa na hao hao ambao leo wamewakumbatia.
Ibilisi alimwambia Yesu nisujudu nami nitakupa milki yote hii.... Yesu alikataa kwani ufalme wake si wa dunia hii!

Sasa wakati wa tatizo hawa wadada wakaambiwa ni wanyonge na watatetewa kwa sababu ccm inatetea wanyonge. Wakazawadiwa ubumge wa viti maalum na ahadi kuwa hakuna wa wa kuwaondoa. Zaidi wakakaribishwa ccm!

Nimefurahi kwa haya aliyosema Kamanda mdee. Hili ni tangazo la kum nock out ibilisi.

Chadema wasifanye makosa wapokelewe kama mashujaa. Halima kamaliza kazi aliposema wao ni wanachama wa hiari na hii inamaanisha kuwa wao sio wabunge tena maana mbunge ni mwanachama kamili wa chama cha siasa kwa baraka za chama.

Hili ni pigo kwa waliojitia kuwatetea.

Chadema mhh!

Mimi binafsi nawhehimu sana Halima na pacha Ester... Nawapenda halafu.
 
Halima dadangu kwenye hili we kubali tu kwamba umechemka tena saana... kuna mambo hadi ya jinai mule kugushi sahihi ya Katibu Mkuu wa chama na kumlisha Mwenyekiti wa chama maneno kwamba ulipata baraka zake!!

Kibaya zaidi zaidi ukagoma kwenda kujadiliwa na kamati kuu...

Aise sioni ukilikwepa hili rungu la kipepe... ushayavulia nguo hayo!!!
 
Watanzania ni kama tunachanganywa.

Spika Ndugai amesema wabunge 19 wanawake wa Chadema wananyanyasika kwa sababu chama hicho kina mfumo dume tena ni kampuni inayoongozwa na mtu mmoja..
Mpaka hapo ni aibu kubwa sana kwa Ndugai.
 
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Naibu Katibu Mkuu kuna kitu wanakijua kuhusu sakata hili ambacho Mnyika hakijui
Mmeshaanza kuhamisha magoli baada ya kuabika kama kondoo asiye na masikio
 
Kwa nini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010 ,2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
Mzee hii sio hoja hata kidogo...hakuna atakayehangaika kuijibu labda kama kichwa chako hakifanyi kazi.. usipokunya leo haina maana kesho hautakunya.
 
Wanakwenda kuyajenga. Hapo ndipo wasipohusika mnapotakiwa kuweza kujitambua nafasi zenu zilipo!
Wayajenge ila watoe ufafanuzi maana zimetoka tuhuma kibao kutokana na suala hili na hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote,sasa isije wakayajenga halafu wakaacha hivihivi bila kutueleza ni nini kilitokea. Maana hadi sasa Halima Mdee na wenzake bado wanaonekana ndio waliyokosea.
 
Halima dadangu kwenye hili we kubali tu kwamba umechemka tena saana... kuna mambo hadi ya jinai mule kugushi sahihi ya Katibu Mkuu wa chama na kumlisha Mwenyekiti wa chama maneno kwamba ulipata baraka zake!!

Kibaya zaidi zaidi ukagoma kwenda kujadiliwa na kamati kuu...

Aise sioni ukilikwepa hili rungu la kipepe... ushayavulia nguo hayo!!!
Hakugoma ila waliomba muda usogezwe na wakatoa sababu zao,kamati kuu ndio imekataa na kukimbilia kutoa kuhukumu.
 
Hoja kuu kwa aliyemsikiliza Halima Mdee leo, ni kuwa CHADEMA uteuzi wa Wabunge wa viti maalumu ni mpango wa Chama.
Sasa mtaanza kutuelewa tuliposema kuwa hatua zote zilizochukuliwa na Mbowe na kamati yake ni mbinu mkakati za ku control Uharibifu uliotokana na makosa ya maamuzi waliyofanya ya kuwaudhi wanachama na wapenzi wa chama kwa kupeleka majina Bungeni, wanachama walioaminishwa hakuna compromise na CCM "Hatuingii bungeni".

Halima anasema Sio mara yaa kwanza kutotambua matokeo ya uchaguzi. Hata kama hatutakuwa sisi wengine wataenda. "Tulifanya hivyo 2010, 2015 kwa nini isiwe 2020"
 
Inahitaji mtu uwe umechangamsha akili kidogo na maji yetu yale ili kujua majukumu ya mwanachama wa hiyari..
 
Back
Top Bottom