Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA aidha ajiuzulu au aondolewe haraka kabla hajaleta madhara kwa Chama

Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA aidha ajiuzulu au aondolewe haraka kabla hajaleta madhara kwa Chama

Shukuru mungu wewe sio Halima kinyume na hapo ungeenda na maji
 
Fact
Fact
Fact
Hi inaonyesh Kuna Mambo ndivyo sivyo yanayo/yaliyo fanyika kwa maslai Binafs
 
Wazee wa keyboard, Mdee kavuja damu, kalala selo, kapigwa virungu sababu ya CHADEMA na ni Mbunge wa CHADEMA sasa hivi kwa mujibu wa katiba ya nchi wala sio hisani, sasa hapa wewe mzee wa kwenye keyboard hujawahi hata kutokwa na jasho, sio hata damu kwa ajili ya CHADEMA unadai Mdee afukuzwe. Hovyo sana nyie. Mdee na wenzake hawajakurupuka, wana baraka za Mbowe.
Umesema ukweli ila sidhani kama nyumbu watakuelewa
 
Chama kina taratibu zake za kupata habari na kuzifanyia kazi may be huu ndio muda mwafaka wangefukuzwa mapema watu wangedhani wanaonewa.
Exactly na uluchokisema. Hapa sasa wameingia kwenye 18 wenyewe. Hivyo kwa maamuzi yoyote hata nayo chukua kwa hakuna wa kulaumiwa.
 
Mkuu Mdee hajavuja damu peke yake wala hakujichagua mwenyewe kuwa M/kiti BAWACHA kachagulia na watu ambao wengine ni marehemu kwa kumpigania yeye ajulikane, hata unaowaita wazee wa keyboard wana mchango wao kwake.
Wanawaka 19 tena viongozi na wake wa viongozi wandamizi siyo wajinga kama unavyodhani tulia, yajayo yanafurahisha
 
CHADEMA hivi hakuna kitengo cha intelligence? Kama mmeshindwa si bora muwe mnamsoma Kigogo2014 kule Twitter, maana kila anachokutabiri kinatokea.

Waombeni hao wahisani wenu, wawapeleke vijana nje wakasome ujasusi.
Huwezi kuendesha taasisi kubwa bila ya kuwa kitengo imara cha kukusanya taarifa, kuzichakata na kuzitafsiri.
Information is power
Kweli wamtumie kigogo ni hazina Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuwatofautisha kati Mdee na Mbowe anacho kifikiria Mdee ndio anacho kifikiria Mbowe, msimamo wa Mdee ndio msimamo wa Mbowe, ndio maana Mdee alijiamini wakati alipo pewa nafasi ya kusema, aliongea kwa kujiamini kabisaa kuwa mwenyekiti Mbowe amebariki kila kitu.
 
Nidhamu katika taasisi yeyote ile ni jambo la msingi sana, iwe sehemu ya kazi iwe jeshini, kwenye biashara, pesa zako bila nidhamu huwezi kufanikiwa.

Kiongozi anapoenda kinyume na maamuzi halali ya taasisi ni aidha anajiuzulu au anafukuzwa. Halima Mdee amekiuka maamuzi halali ya Kamati Kuu hence ya Chama, awe amefanya kwa kushinikizwa au kwa tamaa zake, kwa kitendo kile hana uhalali tena wa kuendelea kuongoza kitengo cha BAWACHA.

Mbali na kukiuka msimamo wa Chama Mdee kaonyesha tamaa na ubinafsi wa hali ya juu, kajiteua yeye wa kwanza bila aibu badala ya kuwatafuta wanawake vijana wengine ndani ya chama nje ya BAWACHA nao wakapate ujuzi bungeni kama yeye.

1. Halima Mdee - M’kiti BAWACHA Taifa
2. Hawa Mwaifunga - Makamu M’kiti BAWACHA.
3. Grace Tendega - Katibu BAWACHA.
4. Jesca Kishoa - Naibu Katibu Mkuu BAWACHA.
5. Asia Mohamed - Naibu Katibu BAWACHA.
6. Agnester Kaiza - Mwenezi BAWACHA Taifa.
7. Ester Matiko- M’kiti kanda
8. Nusrat Hanje - Katibu BAVICHA

Juliana Shonza alikuwa Makamu M/kiti wa BAVICHA nakumbuka alileta vurugu kubwa ndani ya BAVICHA kiasi kwamba kuchelewa kwa chama kumfukuza ilikuwa al manusura akigawe chama, ilikuja kufahamika baadae kumbe Juliana hakuwa peke yake alikuwa ametangulizwa kama chambo, nyuma yake walikuwepo kina Zitto, Kitila, Mwigamba na wengineo.

Chama kimshukuru Mdee kwa kuijenga BAWACHA na yote aliyokifanyia chama lakini kitendo cha yeye kama kiongozi kukiuka maamuzi ya chama hakiwezi kuvumilika na chama kikiendelea kumlea anaweza kuambukiza mbegu ya uasi ndani ya chama na kuleta madhara makubwa ‘irreparable’ kwa sababu hatujui walio nyuma yake ndani na nje ya chama ni akina nani na wana nguvu kiasi gani.
Acheni mfumo dume nyie chandimu! Kwanza lissu mwenyewe kakuta wabunge 70+ kaacha 1, bora mbowe ndo angekuwa mgombea
 
Chama kilikaa lini kutoa maamuzi? Ama na wewe unatumia matamko ya viongozi wachache tu.

Lini CHADEMA ilifanya mkutano mkuu?
Lini chadema ilikaa mkutano mkuu kumpitisha maalim kugombea Zanzibar? Stuka chandimu kuna ombwe la uongozi!
 
Hakuunga mkono, lakini alikalishwa chini na Mdee. Hoja ya Mdee ni kuwa: Haya sio mapenzi yetu ni takwa la kisheria na tukifanya dharau watatoa adhabu, Jee tunajua adhabu yenyewe?
Mikwara tu ya wanasiasa, hakuna adhabu yoyote hapo, naona mko bize sana kutetea kufa kwa siasa za tz, ipo siku mtajakumbuka tulikotoka... Omba mungu ufe mapemaaa
 
Octoba 28/ 2020 baada ya kupiga kura, nilirudi home na kula chai na mbute, ndio kifungua kinywa ambachao mimi huwa kina nifaa maana ni kitamu na kinakaa kwa muda mrefu, tumboni.

Lakini baada ya matokeo ya uchaguzi kuanza kutokea nilistuka baada ya kuona kwenye mitandao ya hapa Tz na hata nje ya nchi kuona Halima Mdee aliyekuea mgombea ubunge Kawe akidai kukamata kura za wizi kwenye mabegi. Mimi niliona ni jambo zito na uchafu kwa taifa letu, kumbe kura huwa zinachakachuriwa!

Leo hii huyu Dada Halima aliyekamata kura za wizi kumbe alitudanganya! Nia yake apate ulaji?

Alijua fika ameshindwa ila akatengeneza uhuni, kudanganya kuna wizi wa kura, leo hii kalamba ubunge, hakuna wizi wala theft! Kwa kweli Halima ni mhuni na hafai.
 
Back
Top Bottom