Rafiki wa kweli mtamjua wakati wa njaa!! Atakuja adui atawatupia mfupa kuwapima imani yenu... ni kweli hapo ndipo utajua kiwango cha mshikamano wenu kikoje.
Fedha ndugu zangu ina ushawishi mkubwa mno, vyovyote mtakavyosema hapa ila fedha imeshindwa tu kuumba na kumfufua mtu mengine yote inaweza.
Ni kipindi cha kuisuka upya idara hii ya wanawake CDM imeyumba; imetikisika; adui kapenya kwa kutumia rupia kafanikiwa....hakuna haja ya kutafuta mchawi cha msingi ni kuisuka upya idara hii.
Hao waachwe wawe wabunge wa mahakama, wataisemea mahakana na yule aliyewaapisha na wataitekeleza ilani ya CCM...yawezekana Bulaya alitumwa kwa kazi maalum na kaitimiza tayari who knows!!