Tuna uandishi wa kikasuku usiozingatia taaluma. Yani mtu anaokota habari bila kuilewa vizuri anaichapa. Ndio maana baadhi ya vyuo vya habari kama SAUT ukisoma uandishi lazima usome Media Law, Human Rights Law na Constitutional Law. Pia kuna option za Criminal Procedure Law na Law of Evidence ili ukiripoti mambo ya kisheria usiwe tabula rasa (angalau uwe na uelewa kidogo).
Anyway; ngoja nitoe shule kidogo maana wengi wamepotoshwa eti akina Halima wamerudishiwa uanachama. SI KWELI. Kwanza ieleweke hawakufukuzwa uanachama na Baraza Kuu, bali Kamati kuu (angalia next slide). Kamati Kuu iliwafurusha tar.27/11/2020 na uamuzi huo kutangazwa na Mwenyekiti Mbowe tar.28/11/2020.
Akina Halima wakakata rufaa Baraza kuu ambalo liliketi tar.12 May 2022 na kubariki maamuzi ya Kamati kuu. Akina Halima wakaenda Mahakamani kupinga maamuzi ya Baraza kuu.
Hoja zao;
1. Hawakupewa haki ya kusikilizwa.
2. Suala lao kushughulikiwa kwa dharura
3. Kuhofia usalama wao
4. Wajumbe wa Kamati kuu kuwa pia wajumbe wa Baraza kuu na hivyo kuathiri maamuzi (law of impartiality).
Leo Jaji Cyprian Mkekha ametoa maamuzi yafuatayo;
1. Kuhusu haki ya kusikilizwa amesema waleta maombi (akina Halima) walipewa haki ya kusikilizwa lakini wakaamua kutokuitumia.
2. Kuhusu suala lao kushughulikiwa kwa dharura, amesema Chadema walikua na haki ya kushughulikia kwa dharura kwa mujibu wa Katiba yao ibara ya 6.5.1(d)
3. Kuhusu kuhofia usalama wao, Jaji Mkekha amesema hoja hiyo haina mashiko maana waleta maombi (akina Halima) hawakuripoti kwenye chombo chochote cha usalama.
4. Kuhusu "Law of Impartiality" hapa ndo pameleta shida. Jaji Mkekha amesema haikua sahihi wajumbe wa Kamati kuu (iliyowafukuza uanachama akina Halima), kushiriki kikao cha Baraza kuu ambacho kilisikiliza rufaa zao. Amebatilisha maamuzi ya Baraza kuu kwa sababu ya kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati kuu.
Kwa kifupi Jaji Mkekha amesema Baraza kuu la Chadema likae tena (bila uwepo wa wajumbe wa Kamati kuu) na lipitie upya rufaa za akina Halima. Kwahiyo akina Halima bado SIO WANACHAMA WA CHADEMA mpaka Baraza kuu litakapopitia upya rufaa zao. Kama hujaelewa muite Miso Misondo umuulize Malisa amepigaje hapo?
View attachment 2842875View attachment 2842876
Sent using
Jamii Forums mobile app