Dodoma. Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.
Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.