Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Dodoma. Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.​

View attachment 2222525

Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Ungejua taratibu za ajira usingeshangaa, hao mwajiri wao wa ubunge ni bunge hivyo ni bunge ndilo litawaambia wasiingie bungeni na si mtu mwingine yeyote, kazi ya Chadema iliishia kwenye uanachama wao tu.
 
Haha..ngoja tuone hii movie inavyoendelea
 
Siyo wabunge tangu hapo bungeni walipelekwa rais kichaa siyo chadema
Haya ni mengine...lakini kwa kuwa wanaingia bungeni na kushiriki mijadala kama wabunge...basi ni wabunge (haijalishi uhalali wao wa kuingia bungeni)...kama chadema wakipeleka barua rasmi kumjulisha kiongozi wa bunge (spika) kuwa hao sio wanachama wao...basi itabidi ubunge wao ukome...maana kwa sasa inatambulika (kwa rekodi rasmi za bunge) kuwa wako bungeni kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), sio kwa hisani ya Rais
 
Dodoma. Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.​

View attachment 2222525

Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Wameshaenda mahakamani lakini?
 
hii nchi mwendazake alitaka kuiharibu vibaya sana, sema mkono wa Bwana umetuokoa !! mambo kama haya ni aibu kubwa kimataifa, looks like we're not organized & uncivilized.
MWENDAZAKE ana mwaka na miezi kadhaa tunga afariki lakini hakauki kwenye mabakuli (midomo) ya baadhi ya wanajF hapa, kana kwamba hakuna vitu vya kujadili.
 
1652426655088.png
 
MWENDAZAKE ana mwaka na miezi kadhaa tunga afariki lakini hakauki kwenye mabakuli (midomo) ya baadhi ya wanajF hapa, kana kwamba hakuna vitu vya kujadili.
Kaua wengi ndugu tena wasio na hatia na ndiyo maana damu zao zinanena hapa - hakuwa kiongozi makini - aliongozwa na mihemko. Imagine unamtoa mfungwa gelezani usiku wa manane then kesho yake asubuhi anaapa ati kuwa ubunge - akili hiyo.
 
Dodoma. Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.​

View attachment 2222525

Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Hapo mdee yupo wapi au kichwa cha jina nimesoma vibaya
 
Spika atasema kwamba hajapata barua rasmi kutoka chadema inayo mtaarifu kwamba wamefukuzwa uanachama.
Ama kama amepata barua kutoka chadema, atasema kwamba hana taarifa rasmi kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa.
Baada ya hapo bunge litalipuka kwa shangwe na kisha spika atatangaza kwamba yeye anawatambua kama wabunge halali wa chadema.
Hapo Sasa tutaludisha mamlaka kwa wananchi maana ndowenye maamuzi ya mwisho
 
Bado ni wabunge maana Chadema bado haijapeleka barua rasmi kwa Spika juu ya kufukuzwa kwao chamani
I'm not sure kama CDM wamepeleka barua au bado lakini wangeheshimu viongozi wa chama chao, kitendo cha kwenda bungeni ni dharau kwa chama na wanaonyesha hawajali lolote ikitokea wakatimuliwa bungeni watarudi kuomba msamaha kwa nani ?
 
hii nchi mwendazake alitaka kuiharibu vibaya sana, sema mkono wa Bwana umetuokoa !! mambo kama haya ni aibu kubwa kimataifa, looks like we're not organized & uncivilized.
Hakika. Unafukuzwa unafukuzwa unakomaa, Njaa Mbaya saaana. Ndio ujue Watu Wapo kwa ajili ya tumbo tuu.
 
Back
Top Bottom