Mkuu
Nguruvi3, the most important document kwenye utawala wa nchi ni katiba, na the most important document kwenye utawala wa chama cha siasa ni katiba zao. Kwenye utawala wa nchi, rais akivunja katiba, anashitakiwa na Bunge, anaondolewa madarakani. Lile swali langu kwa JPM pale Ikulu, kuwa amepata wapi mamlaka ya kwenda kinyume cha katiba, ni kama kusema JPM amevunja katiba, Bunge lingepaswa kumshitaki. Nilipoandika kuhusu Bunge, nyote mnakijua kilichonitokea, hivyo maadam Chadema ina katiba, there is no excuse why Chadema isifuate katiba yake. Kama kijikatiba hiki tuu kidogo cha Chadema inashindwa kukifuata, jee Chadema Ingekabidhiwa nchi na lile ji Katiba kubwa la JMT, wangeiweza?.
Mimi ni kada wa CCM, ila ni CCM contemporary, kuna ma CCM ambao ni ma burgeoges na kuna ma CCM ambao ni ma lumpenproletariat, sisi ma CCM Contemporary tunapenda haki, tunapenda CCM ishinde kwa haki, tunapenda Bunge letu liwe na opposition, tunawapenda baadhi ya baadhi ya wapinzani makini na tunapenda kuona Tanzania ina opposition makini, hivyo kuna wana CCM, mimi nikiwemo, hatufurahii kuona Bunge la Chama kimoja na mara baada ya uchaguzi, tuliwaombea kwa Mwenyekiti wetu, awateue baadhi ya wapinzani muhimu waingie bungeni
Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni? na Zitto nikamuombea uteuzi rasmi
Ombi Maalum kwa Rais Magufuli: Mteue Zitto Kabwe kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, ndiye mpinzani pekee mzalendo, Capable kuongoza PAC! hivi ninapoona Chadema inapoteza assets kama Halima Mdee na Esta Bulaya, kwa sababu za kijinga jinga, tunaumia!.
Kama kuna forgery yoyote, ili Chadema waweze kuipata nakala halisi ya barua ya uteuzi kutoka Chadema kwenda NEC iliandikwa na nani, ilisainiwa na nani, Chadema walipaswa kuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike, Chadema haikufanya hivyo kwasababu inaujua ukweli kuwa hakuna forgery yoyote!. Voices from within, inanieleza yule "kigogo" baada ya Chadema kama Chama kususia kuteua wajumbe wa viti maalum, Halima Mdee akiwa ameandamana na Esta Bulaya, wali seek an audience na kigogo wa Chadema na ku consult umuhimu wa nafasi hizo, kigogo huyo akatoa a go ahead, ndipo Halima aka proceed kuwatafuta na kuwa organize. Kigogo akasaini na process ikaendelea. Mambo yalipochemka, kigogo akawaomba kina Halima wajitoe to save his face, wakamgomea. Kiukweli Halima ni Mwanamke wa shoka, shujaa aliyefundwa akafundika, na ana command a very high respect kwa hao wote 19 kwa kuwasihi wasifungue midomo yao kusema chochote kwenye Baraza Kuu, and take it from me, Halima ali consult na Kigogo, kigogo akamshauri wao wanyamaze na wasijibu kitu, yeye atawaombea msamaha, watasamehewa na kuendelea na ubunge wao, hivyo wakakubali, wakanyamaza na kutotoa siri ya kigogo wa Chadema, hivyo baada ya matokeo kutoka wamepigwa chini ndipo Mdee akajikuta wamefanyiwa uhuni!.
P