Hoja hii imetumika sana na nimesikia kwenye mjadala wmmoja imeshikiwa bango
Hii ni hoja inayofanana na ile ya kwanini Chadema hawakwenda mahakamani kuhusu uchaguzi
Mkuu
Pascal Mayalla naomba niamini kwa dhati kwamba tunaishi dunia na Tanzania moja
Halima Mdee alikamata kura feki akaripoti Polisi kwa ushahidi. Polisi hawakufanya lolote lile
Mgombea wa Ubungo alikamata kura feki akawaonyesha Polisi, hakuna aliyechukua hatua
Uchaguzi wa Kinondoni, kura feki maboksi yameletwa, si Polisi wa NEC waliosughulika na tatizo
Watu wamekamatwa kuhusu vifo vya wana Chadema, watu hao wameachiwa huru
Arusha mtuhumiwa wa mauaji Usa River alikimbia mahakamani Polisi akiwa na bundiki, hadi leo
Dodoma watu wameomba Video ya nyumba za serikali iliyoondolewa, hadi leo hakuna
Wananchi wamehoji nani aliondoa walinzi, hadi leo hakuna jibu kwa keshi nzito kama ile
Kichekesho ni pale Polisi wa Tanzania wanapomsubiri dereva wa Tundu Lissu wafanye uchunguzi
Katika mazingira ya ushahidi huo hapo juu Chadema hawakuona haja ya kwenda Mahakamani kwani mahakama zimekuwa ''compromised' kipindi cha Mwendazake hadi leo ambapo CJ anasema hukumu ziangalie maeneo ya mihimili mingine na si sheria tena
Kuhusu Forgery Chadema wamebaini kwenda mahakamani ni kosa kwa advantage ya 19.
Spika aliyejiuzulu aliwaapisha COVID19 mapema sana kwa sababu maalumu.
Chadema waende mahakamani, suala liwe uchunguzi kesi inaahirishwa kwa miaka 5, simple.
Wabunge wasingefukuzwa suala lipo mahakamani uchunguzi haujakamiliki, Spika angedai hawezi kulizungumzia . Hivyo Chadema wametumia njia za ufundi kulimaliza suala.
Chadema Wanajua kwavyovyote vile Polisi, Mahakama, Spika Ndugai na NEC wangekaa vikao na kulirefusha kwa njia za kiufundi tu na ulaghai laghai kwa miaka 5.
Ni njia hizo ndizo zinamfanya Spika Tulia avute muda ili 19 waende mahakamani, suala likiwa mahakamani halizungumziwi tena. Tunajua mbinu hii
Spika ana barua bado anataka kutoa nafasi kiufundi kwa COVID19 kukimbilia mahakamani.
Hivyo mkuu
Pascal Mayalla haya mambo nadhani unayajua lakini kama alivyosema
JokaKuu unaona wasomaji ni mazuzu sana.
Tindo Proved Mag3