Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Hawa wenye post ndefu achana nao wanaliloa Ruskington ya UN baba kwa serikali wakiwa na upinzani au kambi rasmi ya upinzani amabayo inaundwa kwa asilimia fulani na kuwa na kambi rasmi ya upinzani bungeni
 
Uchaguzi wa 2020 ulikuvuruga sana. Ulipata kipigo kibaya sana. Bado unakinyongo.

Sijawahi kugombea cheo chochote hata ndani ya familia yangu, ila uchaguzi wa 2020 chini ya dhalimu ulikuwa wa kihayawani kuliko maelezo. Kinyongo na dhalimu nilianza toka alivyoanza ulevi wa madaraka, uchaguzi wa 2020 ulisimika rasmi kinyongo na yeye. Imeisha hiyo.
 
KK ilikaa tarehe 11, Tarehe 13wakawepo BUNGENI, chadema wakati huo bado haijaandika barua rasmi kuiwakilisha BUNGENI,
Chadema watakapo andikia bunge barua ikafaamika rasmi na spika akapata kizunguzungu hapo ndipo tuta judge kunanini?, maana mchakato wa chadema ulikuwa wazi.
 
Kuhusu Lowassa kuhamia CHADEMA 2015 na kupewa nafasi ya kugombea urais, msingi ule ule wa Katiba, Viongozi, wanachama na vikao ulitumika kufanikisha hilo. Na huo unabakia kuwa ni uamuzi wa Chama. Upende au usipende.
Mnachekeshaga!

Sawa mlikaa mkakubaliana matokeo yake ni aliyekuwa makamu mwenyekiti wenu Chacha Wangwe, aliyekuwa makamu mwenyekiti wenu Zitto, aliyekuwa katibu wenu mkuu Dr. Slaa, waliyekuwa wenyeviti wenu wa Bavicha (, Shonza, Katambi, n.k) na Bawacha (Mdee). Na kadhalika na kadhalika.

Ni hivi, kwa attitude yenu ya kutojichunguza wenyewe na mifumo yenu na kulea vitabia vya kulaumu laumu wengine kwa matatizo yenu mnayojisababishia wenyewe, mtafukuzana wote hadi abaki mbowe peke yake ili ajifukuze mwenyewe.

Uneutral wangu au kutokuwa neutral wala si hoja ya msingi. Unaweza kuassume kwamba sipo neutral and that's fine. Na pengine sina sababu yoyote wala interest yoyote kwa nini hata nicomment hapa kuhusu chadema. Si mwanachama, sijawahi kuwa mwanachama na wala sijawahi kufikiria kuwa mwanachama. Sema tu ni hiki kitabia changu cha kuwa too analytical na vile naona watu wanavyoweza hata kuchukiana kiwango cha hatari kwa sababu ya mambo ya chadema na siasa zao zisizo za kisayansi na kuendeshwa king'ombe ng'ombe sometimes ni ngumu kupotezea na kuandika mawazo yangu. Na mawazo yangu ni kwamba Chadema mnahitaji radical reforms.
 
Siasa ni kuzidiana uhuni. Kama unadhani kunaustaarabu kwenye siasa basi huijui.
 
Acheni maneno yasiyo na ukweli[emoji116]
View attachment 2223608
Hawafukuziki wapi? Kama ni kwenye chama wameshafukuzwa. Huko bungeni ni jukumu la spika na wale waliohusika kuwaweka huko. Wakiamua kukaa nao bungeni hadi mwisho, yaani 2025, huo ni uamuzi wao. Kuwalipa pesa za mishahara na posho zingine pamoja na mafao ya mwisho, wabunge 19 si kitu sana, kodi zetu zipo, wacha waendelee kuwepo bungeni.
 
Kuna ugumu kwa muhimili kulitolea uamuzi swala hili. Kuwatoa bungeni ni kuiabisha Tume ya Uchaguzi kuwa ni kweli ilipeleka majina ambayo hayakuwasilishwa na Chadema. Hili si jambo dogo kwa chombo kilichoundwa kusimamia sheria za Uchaguzi. Tume haitakubali ionekana imekosa sifa za kufanya majukumu yake. Maadamu Chadema hawataki kutipoti jinai dhidi ya kashfa hii huenda Bunge/Tume imewashauri Akina Mdee waende mahakamani kutetea mchakato wa kupatikana kwao.
 
Samia awe makini sana hasa wakati huu anaposisitiza maridhiano, kitendo cha kuendelea kuwaweka bungeni hao wanawake itatafsiriwa ni dharau, muhimu awe na heshima kwa mwenzake kama naye anavyotaka kuheshimiwa.
Samia hana mamlaka ya kuwatoa watu bungeni, hilo ni jukumu la Spika.
 
AMEN
 
Kama bado wapo bungeni ni kashfa na aibu kwa Serikali ndani na nje ya nchi, kwa CHADEMA ni credit na turufu kisiasa ya kuonyesha ubovu wa Serikali kutozingatia sheria.
 
Ndugu Pascal Mayalla

Hivi ilikuwaje kwa yule dada Nusrat Hanje, aliyekuwa gerezani Singida, akatolewa saa tatu usiku na kusafirishwa usiku kwa usiku kuelekea Dodoma kuapishwa na kuwa mbunge!?

Hapa CHADEMA walifanyaje mkuu Pascal Mayalla
 
Huu ni mwaka wa pili katiba inavunjwa na hakuna kilichotokea.
Mamlaka zimeanza kulea hii tabia,Kuna siku zitawarudi wao,wanadhani wanawakomesha watu wa chache lakini wanatengeneza ubovu na uchochoro kwa watu wengine na hata taasisi zingine pia kuchezea katiba na sheria za nchi bila woga.

Hii mbegu aliyoipanda Ndugai na Mwendazake na wenzao wengine ya kuchezea katiba ya nchi na sheria zake bado inaota Kuna siku isiyo na jina itatugharimu sana,unamwingizaje bungeni mtu ambaye amepoteza uhalali wa kuwa mbunge!Hata theater haiingii mtu ambaye siyo daktari husika, hata news room haingii kila mtu,msikitini haingii asiye muislam, hata sisi wazee wa kwichi kwich hatuingizagi kila mtu bedroom wengine tunawapeleka gest na wengine tunamalizana nao hata kwenye magari huwezi ingiza kila mtu, sehemu nyeti kama hana vigezo vilivyowekwa.

Kesho wataingia watu ikulu wasio na uhalali wa kuwa ikulu kumbe sababu tu kwa ujinga wenye mamlaka wameanza kuharibu heshima ya katiba na sheria walizo kula kiapo kuzilinda na kuzitetea.

Kwa crises iliyokuwepo wakati Mwendazake ametangazwa kuondoka Kama Mabeyo na timu yake,wasinge kuwa na utiisho wa kutii katiba,sheria na itifaki za ki nchi na viapo vyao na kufanya maigizo na michezo Kama alivyofanya Ndugai na Sasa Tulia sasahivi tungekuwa na historia nyingine tofauti.
Hawa wehu wanachokifanya Sasa wanaipunguzia katiba ya nchi utiisho wake,historia itawahuku hata kwenye makaburu yao.
 
Wakina nani?!
 
Mlisema Magufuli ndiyo anawakingia kifua wasiondolewe,

Kwani bado yupo?
 
Ester Bulaya si asset bali ni pandikizi, hii fracas imesababisha aangaliwe kwa jicho la tatu hivyo kumtumia kama reference kunanifanya nihisi una agenda maalum kwenye mlolongo wa posts zako.

Uwepo wa Ester Bulaya ndiyo umem-mcopromise Halima Mdee, watu wenye nia njema na chama chao hawawezi kung'ang'ania kwenda kinyume na majority kwenye chama chao regardless taratibu za katiba zikoje. Mshikamano wa chama ni primary goal, sasa hawa wanaosababisha mpasuko wanafanya hivyo kwa faida ya chama gani?

Katika watu ambao walikuwa wakidai mtu wa opposition anaposhabikiwa na kuwa supported na chama tawala basi huyo si mpinzani wa kweli sasa leo hii unadhani hilo limemtoka kichwani? Malengo yao yako dhahiri na si bahati mbaya kwa CCM kuwakingia kifua lakini hata wakiendelea kuwa bungeni haisaidii kuwarudisha CDM na kamwe hawatarudi hivyo acha waendelee kuvuna pesa za bure kwa uwepo wao ambazo ni kodi za Watanzania.
Sasa Halima Mdee(this is according to your posts) atakuwa akishiriki vikao vya CDM kwa cheo chake ndani ya chama.
 
Ni Wakati rasmi kufungua kesi kuomba ufafanuzi wa hili atajulikana aliyekaa Nyuma yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…