Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Mkuu Pasco kuna bandiko nimekuwekea mlolongo wa matukio ambayo Polisi wamepewa taarifa na hawakufanyia kazi kwasababu tu yanagusa ima serikali au chama tawala.

Kazi ya msingi ya Polisi ni kuzuia uhalifu na kusimamia sheria.

Kuna wakati Polisi walifanya mzoezi kuzuia maandamano ya Chadema. Nani alipeleka taarifa?
RPC alizuia mkutano wa wapinzania kwasababu ya intelejensia ya ugaidi. Nani alipeleka ripoti
Polisi wanakamata wauza madawa kwa 'intelejensia zao'

orodha ya Polisi kuingilia kati mambo bila taarifa ni ndefu...

Maana yangu ni kuwa palipo na taarifa za uhalaifu Polisi wanatakiwa kisheria kuingilia kati (kuzuia), halafu kuwakanata wahusika na kuwafkisha mahakamani (kusimamia sheria)

Taarifa ya Chadema kuhusu forgery iliwatuhumu NEC na Spika alliyepokea majina hayo
Hii ni kashfa kubwa sidhani ingalikaliwa kimya

Pasco aliitwa kwa kipande cha gazeti. CAG Assad aliitwa kwa neno dhaifu etc etc

Tume ya uchaguzi isingekaa kimya na tuhuma nzito, huu ni uchafu mkubwa wa nchi
Hakuna aliyekanusha forgery, si NEC , Ndugai au Msajili wa vyama

Nimeeleza kwanini CDM hawakutaka kuendeleza jambo hili.
NEC , Ndugai na Msajili walitaka kutumia muda kwamba suala linafanyiwa uchunguzi na Polisi lipo mahakamani halizungumzwi.Wabunge wanakaa miaka 5 kesi inaisha

Pengine ungejiuliza yale mawasiliano ya E.Bulaya na KM wa CCM yalihusu nini?
Ungejiuliza Nusrat Henje alitokaje magereza usiku bila amri ya mahakama na kuwa Mbunge?
Ungejiuliza kwanini waliapishiwa jikoni na si mbele ya ukumbi wa Bunge?
Ungejiuliza kwanini 19 hawatoi ushahidi wa uhalali wao kutoka Chadema?
Ungejiuliza kwanini kama ni halali hawakuta kuhudhuria CC na ushahidi tena wakiwa viongozi?

Mkuu jitathmini ,wewe ni nguli.

JokaKuu
 
Jamani kwani nyie hamtaki kuona Ndugai na Mahera wakibananishwa na kibatala mahakamani? mzee mdee na mabinti zake 18 wakilambishwa sakafu?

Acheni iendelee hivihivi dunia ishuhudie unafiki wa nchi inayojifanya inafata sheria na demokrasia
 
Mimi ni kada wa CCM, ila ni CCM contemporary.... hivi ninapoona Chadema inapoteza assets kama Halima Mdee na Esta Bulaya, kwa sababu za kijinga jinga, tunaumia!.
P ukiwa na ''assests' zikabadilika kuwa liabilities huna sababu ya kuziita assets tena
Hawa walikuwa viongozi tena wa Kitaifa, walitakiwa kufanya mambo kwa weledi

Viongozi hao waliwashawishi wanachama wao akiwemo Mbunge Catherine Ruge aliyekataa upuuzi

Katika nyakati walizopitia wale waliokataa akina Halima walikuwa chini ya koti la Ndugai
Hawa ndio assets badala waliobaki wakipigani haki Ubalozini USA na mkutano kule Iringa?

Spika Ndugai akisema CDM wanaonea wanawake, COVID 19 walikuwa na CCM wanashangilia
Kama kuna forgery yoyote, ili Chadema waweze kuipata nakala halisi ya barua ya uteuzi kutoka Chadema kwenda NEC iliandikwa na nani, ilisainiwa na nani, Chadema walipaswa kuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike
Polisi hawa wanaomsubiri dereva wa Tundu Lissu ndio unaamini wangefanya uchunguzi, please
Hii ingalikuwa ni dana dana, uchunguzi haujakamilika, suala lipo mahakamani etc.
Chadema wasingeweza kufuta shauri kwasababu anayefungua ni Jamhuri a.k.a Polisi ni mashahidi

Hivyo Polisi na Mahakama zetu zinazoangalia mihimili mingine(CJ) zingechelewesha tu.
Hili lipo kiufundi zaidi na unalielewa
Chadema haikufanya hivyo kwasababu inaujua ukweli kuwa hakuna forgery yoyote!.
Haya maneno unasema wewe , hukutuhumiwa. Waliotuhumiwa NEC na Ndugai wapo kimya

Tunapenda utueleze haya
Kikao gani cha chama kiliwateua 19?
Nusrat Hanje alitokaje magereza usiku bila amri ya mahakama? Kigogo gani wa CDM alimtoa?
Kwanini COVID19 hawakuhudhiria CC ya Chadema?
 
Kwa mujibu wa katiba ya chama,chombo chanye mamlaka yakuwafukuza uanachama kina mdee ni mkutano mkuu na sio baraza kuu kama walivyofanya Chadema.Jitahidini kufuata miongozo ili huu mjadala uishe.
 
Inaonekana hawafukuziki hawa.
Huu ilikuwa mpango wa Magufuli na Ndugai hvyo Bunge la sasa likiongozwa na Tulia lisipofuata sheria, itakuwa wazi kuwa nao ni wafuasi wa Magufuli wanye lao jambo kutaka kumuangusha Samia.!
 
Elezea vema hapa Mkuu
 
Kwa mujibu wa katiba ya chama,chombo chanye mamlaka yakuwafukuza uanachama kina mdee ni mkutano mkuu na sio baraza kuu kama walivyofanya Chadema.Jitahidini kufuata miongozo ili huu mjadala uishe.

..walifukuzwa na kamati kuu.

..wakakata rufaa ktk baraza kuu.

..baraza kuu likakazia hukumu ya kamati kuu.

..kama unayosema ni kweli kwanini Halima na wenzake walikata rufaa kwa baraza kuu?

..lakini kwanini tuzunguke kote huko? Kwanini Halima na wenzake hawaelezi kikao kilichowateua, wala kiongozi aliyepeleka majina yao kwa tume ya uchaguzi?

Cc Erythrocyte
 
..walifukuzwa na kamati kuu.
Kamati Kuu ni mamlaka ya nidhamu ya wabunge but not Halima. Kesi ya wabunge iliendeshwa kikangaroo hivyo hukumu ile ya CC ni batili.
..wakakata rufaa ktk baraza kuu.
Baraza Kuu ndio mamlaka ya rufaa ya wabunge. Baraza Kuu lilipaswa kwanza kujiridhisha kama CC ilitenda haki, halikufanya, likaubariki ukangaroo wa CC!. Hapa sasa ndio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee. Hakuna kesi yoyote ya Halima iliyowasilishwa Baraza Kuu. CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kufukuza Halima wakati hata Baraza Kuu halina mamlaka hiyo?!. Kesi ya Halima ingetoka Baraza Kuu na kuingia Mkutano Mkuu ndio pekee wenye mamlaka hiyo. Kilichofamyika ni uhuni, ambao mimi nimeuita ni ukangaroo.
..baraza kuu likakazia hukumu ya kamati kuu.
Kitendo cha kukazia hukumu batili nao ni ukangaroo!.
..kama unayosema ni kweli kwanini Halima na wenzake walikata rufaa kwa baraza kuu?
Rufaa zote lazima zifuate kikao kinachofuatia, Halima alikata rufaa Baraza kwasababu CC sio mamlaka yake ya nidhamu na haina uwezo wa kumfukuza!.
..lakini kwanini tuzunguke kote huko? Kwanini Halima na wenzake hawaelezi kikao kilichowateua, wala kiongozi aliyepeleka majina yao kwa tume ya uchaguzi?

Cc Erythrocyte
Hawaeezi chochote kwasababu hakuna kikao chochote kilichowateua, kule NEC hawahitaji taarifa za kikao, wanahitaji barua ya uteuzi na fomu zilizosainiwa. Barua ilikuwepo na fomu zilikuwepo na aliyezisaini yupo ukumbini na ameketi meza kuu!.
P
 

..umelenga kuwatetea lakini ndio kwanza unawakandamiza. you need to proof read what you write before you click the reply button.

..kwenye bandiko lako unasema hakuna kikao kilichowateua. Hilo ni TATIZO na halikutakiwa lishughulikiwe na Chadema. Tatizo lilipaswa kushughulikiwa na POLISI na TAKUKURU.

..Again, Halima na wenzake hawakuteuliwa na vikao vya Chadema. Suala hilo lilipaswa kuheshimiwa na kuzingatiwa kwasababu sheria inaelekeza kwamba wabunge wa viti maalum watateuliwa na vyama.
 
Kwa mujibu wa katiba ya chama,chombo chanye mamlaka yakuwafukuza uanachama kina mdee ni mkutano mkuu na sio baraza kuu kama walivyofanya Chadema.Jitahidini kufuata miongozo ili huu mjadala uishe.

..hebu tuletee katiba ya chadema ili tujiridhishe na hayo uliyoyasema.

..hakuna kikao cha chadema kilichowateua hivyo hawakupaswa kuwa bungeni.
 
Kwa mujibu wa katiba ya chama,chombo chanye mamlaka yakuwafukuza uanachama kina mdee ni mkutano mkuu na sio baraza kuu kama walivyofanya Chadema.Jitahidini kufuata miongozo ili huu mjadala uishe
Msome JokaKuu hapo juu kuhusu katiba!
 
Kamati Kuu ni mamlaka ya nidhamu ya wabunge but not Halima. Kesi ya wabunge iliendeshwa kikangaroo hivyo hukumu ile ya CC ni batili.

..CC imemshughulikia Halima kama MBUNGE.

..Halima hakuhukumiwa kama mwenyekiti wa Bawacha, au kwa makosa aliyoyafanya akitekeleza majukumu ya mwenyekiti wa Bawacha.

..Hoja yako inafanana na hoja aliyopambana nayo Dr.Slaa na wakili wake Dr.Sengondo Mvungi [ r.i.p] walipomshtaki Benjamin Mkapa alipojaribu kuvunja halmashauri ya Karatu.

..Kulitolewa pingamizi kwamba Mkapa hawezi kushtakiwa kwasababu ana kinga ya Uraisi.

..Dr.Slaa na Wakili Dr.Mvungi wakajibu kwamba wana haki ya kumshtaki Mkapa kwasababu alipojaribu kuvunja halmashauri ya Karatu alikuwa akitumia madaraka yake kama Waziri wa Tamisemi, na sio madaraka yake kama Raisi. Na hoja yao ilipita.

..Tukirudi kwenye hoja yako, umetafsiri kimakosa kilichofanywa na CC ya Chadema ilipomuadhibu Halima Mdee.

..CC imemuadhibu Halima Mdee kama MBUNGE. Haikumuadhibu kama Mwenyekiti wa Bawacha.

..Kwa maoni yangu, hoja yako haina mashiko bila kulazimika kuhakiki kama umenukuu katiba ya Chadema kwa usahihi, au la.

Cc Nguruvi3, Petro E. Mselewa , Erythrocyte
 
Mkuu JokaKuu nimeisoma hoja ya Pascal Mayalla kwa mshangao mkubwa hasa ukizingatia ni mtu wa sheria. Pasco anasema Halima Mdee ni mwenyekiti wa Bawacha , CC si mamlaka yake ya nidhamu. Nina uhakika Pasco anatafuta mahali pa kushika hajapata. Upotofu wake ni huu;

Halima Mdee ni mwanachama wa Chadema, alikuwa Mweyekiti wa Bawacha na Mbunge
Kuwa mwanachama kunatoa haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo H.Mdee alichaguliwa

Utumishi katika uongozi ni dhamana na fursa (privilege). Chama kinaweza kukukondoa katika uongozi ukabaki mwanachama au kukuondolea vyote. Chama chochote hakiwezi kufuta uanachama ukabali na dhamana na fursa ndani ya chama hicho

CC iliwatimua Wanachama wa Chadema waliokwenda Bungeni na kuapishwa na Ndugai kama Wabunge wa Ndugai kwa kutumia jina la CDM. Adhabu iliwahusu Wanachama!

Baraza kuu limeridhia kuwafuta Uanachama. Ukifutiwa uanachama unapoteza fursa zingine zote
Halima Mdee hakuhukumiwa kama M/Kiti wa Bawacha bali mwananchama wa Chadema

Kwani Sophia Simba wa CCM ilikuwaje?
 
Ukitumia hii Id huwa unatulia kiduchu. Tofauti na ile ya Tindo
 
Ndugu,
Hadithi za aina hii kwenye siasa hasa za Tanzania ziko nyingi mno, sehemu kubwa ikiwa ni za kubumba tu, ili mawakala na wa aina zenu waendelee kujifariji na kupoza AIBU waliyopata baada KUCHEMSHA.
Mahera, Ndugai na hasa Mwendazake, hawakuwahi kuwapenda covid 19 kwa lolote; IWE wote, Nusrat Hanje au Halima Mdee pekee. Isipokuwa waliwahitaji tu kwa ajili ya kusaidia kuweka picha ya kuwavutia wafadhili na zaidi ya hapo kuikomoa CHADEMA.
Zitto pia alianza vizuri lakini baadae NAE akakubali kuwa pandikizi kama wengine wengi waliyowahi kutumiwa na wenye nchi wanaokoseshwa raha na uimara wa CHADEMA na hasa uwepo wa Mbowe.
Hakika haya yote yanaibuka na kuzidi kukuja JUU hadharani taratibu. WAPENDA haki twasubiri hata ifikie huko MAHAKAMANI ili yote yazungumzwe kwa uwazi na sauti zaidi kama yalivyokuwa ya akina Kingai. Kwa bahati njema kabisa, CHADEMA ndio itazidi kuwa imara kwa juhudi zenu mnaopigana na kushindana kuiua. AMEN.
 
Wew mzee acha Ujinga wako usituone sisi sote ni wachumia tumbo Kama wewe.
Kama jeshi la polisi ukiripoti kitu linafanyia kazi kwa nini Hawaja wakamata Wala kufanyia uchunguzi kupigwa Risasi Tundu Lissu?
 
Haya wadau tulichosema kimetokea.

Tulijua Tulia Aksoan sasa anajificha nyuma ya kivuli cha ''mhimili mwingine''.

Uwepo wa akina Halima Mdee una nguvu ya dola , Bunge na huko walipo sasa

Wanaodhani ni suala la Chadema tu na tararibu si kweli. Kuna nguvu kubwa sana

Kosa
Rais SSH ana R4 moja ikiwa ni reconciliation. Kwa mwendo huu reconciliation sijui kama itatokea
Lakini pia inamuondolea uaminifu mbele ya umma
Mambo ya akina Halima yana derail agenda za SSH. Leo Mdee amekuwa mkubwa kuliko Royal tour
Rais SSH asidharau upinzani, kuna kundi kubwa la wananchi
Nina wasi wasi sana na hali ilivyo kuelekea miaka 5 mbele!

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…