Halima Mdee: Serikali iache kukimbilia kukopa inadumaza akili

Bajeti ya serikali ni trillion 32
Kwa mawazo yako pesa zote ziende kwenye miradi, mishahara utalipaje?
Watanzania hawapendi kulipa kodi yani wafanyakazi wa uma ndio tuna lipa kila kitu kwa sababu mishahara inapitia kwenye check number, ila ukifanya starehe zako na mwanamke una taka matibabu bure
 
Tozo ni ukwapuaji uliohalalishwa maana kwenye transaction moja kodi inakatwa mara mbili.
 
Humu JF Kuna watu kila siku wanaimba Mungu wabariki wazungu kisa wanahudhuria mahakamani.
Sasa mwenzao anaona wazungu siyo wa kutuletea maendeleo.
Chadema hawajielewi.
Unapakatwa au umeshavimbiwa na hayo makiti moto
 
Kilio cha kumuunga mkono aliyemkingia kifua kubaki bungeni kimagumashi akizifaidi pesa za mkopo
 
Humu JF Kuna watu kila siku wanaimba Mungu wabariki wazungu kisa wanahudhuria mahakamani.
Sasa mwenzao anaona wazungu siyo wa kutuletea maendeleo.
Chadema hawajielewi.
Duuuh! Chadema inahusikaje ikiwa cdm inasema wazi imemtimua halima?
 
inasikitisha sana kwa nchi kama Tanzania kila kitu tunapitisha bakuli

watu wanafurahia kwakuwa mkopo unajenga mashule hivi hiyo ni logic kweli?

akina marehemu kaka Rwakatare wamejenga ma shule nchi nzima hii sembuse serikali?

mbona tunajitia aibu jaman? ipo miradi ambayo serikali inatakiwa ikope mfano sgr, bwawa la mwalimu nyerere hata tukiambiwa serikali imekopa kidogo inatia moyo

lakin serikali inaenda kukopa kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya elimu? wakati huo huo serikali inayokopa ndio serikali yenye gas, nadini ya kila aina, bandari za kutosha, bahari za kutosha, mito mikubwa na maziwa, ardhi yenye rutuba kwa mazao ya chakula na biashara, mifugo ya kutosha, mbuga za wanyama za kutosha

yaani ina raslimari za kutosha leo hii unaenda kuomba mkopo kwa ajili ya miundo mbinu ya shule hivi kweli jamani inaingia akilini?

inachofanya serikali kuhusu baadhi ya mikopo kwa kweli ni aibu maana inaenda kukopa pesa ambayo hata MO Dewij anatembea nayo kwenye mfuko wa shati
 
Mbee
Mdee anaongea nani atamsikiliza sasa?! Ndugai aliuliza akaishia kuondolewa kwenye uspika, itakua sembese mbunge wa covid 19?! Huna Chama, huna muwakilishi, sasa nani atakusikiliza? Bora akae tu kimya, watu wamsahau.
 
Sehemu ya hiyo mikopo inatumika kuwalipa wao kule bungeni, hii serikali ya sasa ni ya wavivu wa kufikiri wasio na plan yoyote, kila wakitulia wanawaza kuomba mikopo ya "masharti nafuu" kama sifa.
Mikopo haitumiki kulipa mishahara
 
acha ujinga huyo sio mbunge wa chadema ni waccm kwani alishafukuzwa uanachama.
 
Hawa wabunge wengine ndoo maaana hata hawaolewi nivigumu sana kumuelewa,au je anafaa kuwa kiongozi?
 
Hawa wabunge wengine ndoo maaana hata hawaolewi nivigumu sana kumuelewa,au je anafaa kuwa kiongozi?
james; inawezekana wewe ndio umeshindwa kumuelewa halima

ila alichoongea pale kina maana sana , hii nchi ujue ina utajiri wa kutisha, ni nchi ambayo ina kila raslimari

hivyo kinachotakiwa ni kukomaa kwanza na matumizi bora ya raslimari zetu, inapokuja miraji mikubwa sana ya kimkakati ndio tuombe msaada

lakini sisi unakuta hata ka inshu kadogo tu tunahitaji kukopa sasa hii sio kitu kizur sana,

nchi kukopa pesa kuboresha miundombinu ya elimu maana yake ime fail kabisa kupata hata iyo pesa ndogo toka kwenye vyanzo vyake

miradi kama ile ya SGR & BWAWA LA NYERERE ni miradi mikubwa sana hata tukikopa sio mbaya sana lakini hii midogo tufanye kwa pesa yetu

kwaiyo halima yupo sahihi sana sababu ile mikopo tunayopewa ina riba sasa huoni kama tutakwama?

halafu hata ki mentality imejengeka kwamba akili ukishaielekeza uko maana yake kila utakacho plan kufanya bas cha kwanza kabisa utaangalia ukamkope nan

Ndio maana hata mama mwenyewe kaweka wazi kwamba fursa yeyote ya mkopo ikitokea lazima yeye akope tu bila kuangalia ratio ya deni imekaaje

kwa kufanya hivyo anaamini kuwa iyo ndio njia sahihi ya kutuletea maendeleo , sasa bado hajatufahamisha pato la ndani nalo linafanya kazi gani au kama hatuingizi hata buku aseme ili tujue kwamba tanzania hatuna kabisa pato la ndani
 
kupitia chadema???...chadema ipi. maana iliyopo ilishamkataa au huko ccm mmeunda chadema yenu?
 
Klekippo,naamini wewe ndo ukunielewa vizuri, Mimi siyo kwamba naunga mkono kwa serikali mikopo isiyo na tija, ila mimi nachukulia mfano nchi hii tokea tumepata uhuru, Hawa watangulizi wa Mama Samia wamekuwa wanakopa tu. Sisi kama wananchi wala hatuanbiwi ila utasikia deni la taifa sasa tilioni flani! Lakini kwa huyu mama anasema tumepa mkopo,nafikili sasa nikupata washauri kwamba hii mikopo enatosha au inayoitajika ielekezwe wapi kama ulivyo sema, lakini mimi naamini wazanzibar siyo wanafiki kama tulivyo sisi wabara, sisi tumezidi unafiki hatuwi wawazi
 
Mikopo haitumiki kulipa mishahara
Umesema uongo, mikopo hutumika pia kulipa mishahara.

Ipo hivi makusanyo mwezi wastani ni tril 1.3 kwa mwezi.
Mishara inakula bil 700, operation bil 400, Deni la taifa bil 700
Hebu tuambie kwa makusanyo tuliyonayo hiyo pesa nyingine inatoka wapi?
 
Umesema uongo, mikopo hutumika pia kulipa mishahara.

Ipo hivi makusanyo mwezi wastani ni tril 1.3 kwa mwezi.
Mishara inakula bil 700, operation bil 400, Deni la taifa bil 700
Hebu tuambie kwa makusanyo tuliyonayo hiyo pesa nyingine inatoka wapi?
1.3 ni makusanyo ya TRA pekee
Serikali ina vyanzo vingine vya mapato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…