PreGE2025 Halima Mdee: Sitamani kuiacha CHADEMA. Kama itanifungia milango, basi nitaangalia mbadala mwingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa kweli huyu dada alikuwa imara kwelikweli. Amewakomaza wadada wengi mitaani pamoja na Bulaya na Matiko.

Kwa maelezo yake ni kama anaomba msimaha na inawezekana alishawishiwa.

Nukuu: Nitakuwa wa mwisho kuhama chadema.

Tukumbuke maneno ya Boni Yai waligongewa mhuri wa wizi na dalali wa Chauma wakaenda bungeni. Ishu ya Covid 19 Chadema iangalie upya kwa wale ambao wako tayari kubisha hodi kama dada yangu Halima.

Yale masurufu yameondoka.

Halima karibu chadema utimize ndoto yako.

Na mimi ni mmoja wapo namwembea..

Huyu dada na Mnyika nikikumbuka kipindi wanatafuta ubunge walipambana sana. Mnyika alikuwa anatembea na miguu na bendera yake amevaa mgongoni ya chadema. Nilikuwa nasoma na alimishawishi sana.

Halima na Mnyika tulikuwa tunawaita mapacha.
 
atuambie kwanza vizuri walifikaje bungeni 2020, na je yuko tayari kwa no reforms no election
 

huyu kamanda afunguliwe milango chap! kukosa kupo, ndio maana kutubu kupo
 
Nimekuwa nikitamani wale Covid 19 wasamehewe warudi kundini.
CDM ifike mahari itambue zile zilikuwa Ajali za kisiasa zilizosababishwa na JPM.
 
wana CDM ni wamoja, hakuna makundi ya walioijenga kwa damu na jasho na waliokuta matunda yapo tayari.

kwa sasa utamjua mwanaCDM kwa msimamo wake wa #NoReformsNoElection

Kama unakubaliana na msimamo huo, karibu sana CDM

kama la, wahi ubwabwa huko CHAUMMA

stori za jasho na damu na kukuta matunda hazitusaidii wkatii huu, kwani hao wanaodaiwa kujenga CDM kwa jasho na damu ndio wafaidika wa ruzuku za chama na ubunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…