PreGE2025 Halima Mdee: Sitamani kuiacha CHADEMA. Kama itanifungia milango, basi nitaangalia mbadala mwingine

PreGE2025 Halima Mdee: Sitamani kuiacha CHADEMA. Kama itanifungia milango, basi nitaangalia mbadala mwingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Halima aache kucheza na maneno, yeye sio mwanacdm, aende kwenye vyama anavyoweza kupata ubunge maana hicho ndio kipaombele chake. Hao waliokwenda Chauma ndio hasa kundi lake, hapo alipo anatafuta maneno ya ghiliba kuongopea wasiojua lolote. Cdm hata wakimrudishia tena Mdee uanachama wake, wasimpe nafasi yoyote ya uongozi.
 
Mnaonaje tumpe second chance?
Sio kwenye cheo, akae pembeni kama mwanachama wa kawaida. Hakuna namna Mdee anaweza kurejea cdm bila kuwa na uhakika wa cheo. Hata hofu yake sasa ni baada ya kuona bado cdm ina ushawishi mkubwa kwa wananchi, huku Chauma ikionekana ni wasaka vyeo bila ushawishi wowote wa maana kwa umma.
 
Kwasasa watamrudisha,saa hizi hawachagui tena
Mdee ni mpinzani ni vile alijichanganya Sema Lissu anapenda mambo ya transparency aliwambia waombe msamaha wananchi then wasema waliendaje Bungeni hapo kwenye kusema waliendaje Bungeni ndo Kuna msumari wa mwisho wa kisiasa wa Mbowe Lissu akili mingi sana yule ni vile yuko Upinzani
 
Sio kwenye cheo, akae pembeni kama mwanachama wa kawaida. Hakuna namna Mdee anaweza kurejea cdm bila kuwa na uhakika wa cheo. Hata hofu yake sasa ni baada ya kuona bado cdm ina ushawishi mkubwa kwa wananchi, huku Chauma ikionekana ni wasaka vyeo bila ushawishi wowote wa maana kwa umma.
Mimi nadhani Mdee ni 'career politician' sidhani kama atakubali kukaa bench lakini kati ya wale 19 yeye ndio kaamua kutubu basi tumpe second chance.
 
Kwa kweli huyu dada alikuwa imara kwelikweli. Amewakomaza wadada wengi mitaani pamoja na Bulaya na Matiko.

Kwa maelezo yake ni kama anaomba msimaha na inawezekana alishawishiwa.

Nukuu: Nitakuwa wa mwisho kuhama chadema.

Tukumbuke maneno ya Boni Yai waligongewa mhuri wa wizi na dalali wa Chauma wakaenda bungeni. Ishu ya Covid 19 Chadema iangalie upya kwa wale ambao wako tayari kubisha hodi kama dada yangu Halima.

Yale masurufu yameondoka.

Halima karibu chadema utimize ndoto yako.

Na mimi ni mmoja wapo namwembea..

Huyu dada na Mnyika nikikumbuka kipindi wanatafuta ubunge walipambana sana. Mnyika alikuwa anatembea na miguu na bendera yake amevaa mgongoni ya chadema. Nilikuwa nasoma na alimishawishi sana.

Halima na Mnyika tulikuwa tunawaita mapacha.
Halima na Bulaya na Matiko warudishwe haraka sana chadema. mbona Dr Slaa karudishwa.
 
Mdee na Bulaya, hawa watu nawaona ktk upinzani wa kweli, ni vile ajari kazini, wasamehewe na warejeshwe kundini, km ni usaliti, mbna Slaa alisaliti kambi, akapewa na Ubalozi huko nje, na Leo kapokelewa kundini?

Kwanini mdee akataliwe? Na hapo kaomba msamaha kiutu uzima, km Chadema ilimpokea Lowassa na kumpa fomu ya urais, ndo ishindikane kwa Mdee?

Nampenda sana Mdee, jamaniii
 
Back
Top Bottom