Halima Mdee tubu yaishe lakini eleza ukweli wote Covid 19

Halima Mdee tubu yaishe lakini eleza ukweli wote Covid 19

Ni policcm gani angeweza kuchunguza jinai hiyo wakati huwo ulikuwa ni mpango wa ccm kutakakufanikisha jambo hilo. Uchunguzi wa kushambuliwa Lissu hadi leo hawajaufa ndio Mnyika aende kuripoti kwamba wamefoji saini huku ccm lengo lao nikuiua chadema. Ccm ina laana sana.
Huyo mayala aka nzala ni mtu mzima hovyo, ukitaka kujua ni hovyo msikilize akiwa pale jambo TV tutaona kumbe wanajf Huwa mnamkuza bure halafu hajui kitu hasa kwenye Sheria anaijua juu juu sana ila ambao hawajui Sheria wanamuona anajua. Hebu image hao police walioshindwa kuchunguza tukio la Lissu uwapelekee tukio la forgery unafikiri watachunguza? Mayala aendelee kumsifia mama yake wa ccm tu akiwa jambo tv na hakuna kingine anachoweza.
 
Sii kweli!, JJMnyika kama KM wa Chadema alipaswa kusaini barua ya kuwateua, kwa vile wamewasilisha barua ya uteuzi iliyo sainiwa na mtu mwingine yeyote ambaye sio KM, kitu cha kwanza ni
  1. JJMnyika as KM wa Chadema, alipaswa kuripoti polisi kuwa ameona wabunge wa Chadema wakiapishwa huku yeye hakusaini barua yoyote ya uteuzi, hivyo saini yake itakuwa imefojiwa.
  2. Kwa vile KM hajaandika barua yoyote, ni jukumu la polisi kuchunguza hiyo barua ya hao 19 ilisainiwa na nani.
  3. Baada ya kuripoti hiyo jinai polisi, ndipo sasa Chadema ingeitisha ile kangaroo court yake kuwauliza aliyesaini barua ni nani?.
  4. Ni mamlaka tuu ya uchunguzi ndio inaweza kuomba ushahidi wa hizo barua na sio KM wa Chadema, ikifanyika jinai yopyote, hatua ya kwanza ni kuripoti polisi.
  5. Hili jambo lingekwisha pale pale.
  6. Polisi wangethibitisha jinai, then uthibitisho wa polisi ungepelekwa NEC kuwa hao 19 wamefoji uteuzi, then NEC ingewatengua na kumuarifu Spika, wangetenguliwa!

This was a police case, ili iwe police case, KM aliopaswa kuripoti!.

NEC wampe barua Mnyika kama nani?!. KM alipaswa kuripoti polisi, uchunguzi wa polisi ndio waombe barua, watu wa forensic wa polisi wachunguze forgery ya saini ya KM kuwateua!.

Kosa ni la KM kutoripoti!, and this is not the first time, ile siku kabla TAL hajashambuliwa aliitisha press conference na kusema kuna gari inamfuatilia!. Hakuripoti polisi!, polisi did nothing kwasababu hawafanyii kazi taarifa za magazeti, TAL alipaswa kwanza kuripoti polisi, kisha ndipo afanye press, na kueleza ameripoti polisi!. Huu ni uzembe!. Niliuliza humu Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?

No!, Chadema imepata mbunge mmoja wa jimbo na viti maalum 19!, kwa vile vyuma vya JPM, that was fursa to make money na Chadema to survive!. Kuna kigogo wa Chadema aliwasaidia kila kitu, na alikuwepo kwenye CC iliyowatimua!. Kati ya hao 19, 4 wana cohabit, na wajumbe wa CC ya Chadema, wanaishi nyumba moja kinyumba, wanalala kitanda kimoja, pika pakua, mwenzi wako anaibukia kuapishwa eti wewe hujui?.
P
Hapo kwenye polisi unamaanisha polisi ipi mkuu....
 
Utakuwa unawashwa kwa mada zizsizokuwa na mwelekeo hizi.
Hili ndilo jambo muhimu kujadiliwa humu wakati huu?

Mtafute mzungumze; akupe msimamo wake ni upi kwa sasa; halafu njoo hapa utueleze.

Unachokonoachokonoa maswala hata bila ya kupima muda wake sahihi upoje?

Unataka akwambie sasa, halafu iweje?
Mtafute mzungumze.... Non sense
 
Mtafute mzungumze.... Non sense
Wewe na huyo niliyemjibu hapo hamtofautiani kwa kuweka mada za kipuuzipuuzi., bila ya kuwa na maelezo yanayoendana na vichwa vya mada mnavyovitumia. Inaonyesha hamna uwezo wa kujengea hoja mnayotaka watu wayajadili.
 
Halima hana haja ya kuusema ukweli wowote utakaowaibisha watu mliowaheshimu sana!. Mimi nakuhakikishia hata JJ Mnyika anaujua ukweli ila hausemi!, angalia hapa nilimuuliza nini na alijibu nini!

View: https://youtu.be/-M8HnYQgtAc?si=STE5W7DTrIuVjDJX

Niliendelea kumbananisha JJMnyika, kwanini hawakuripoti polisi jinai ya forgery, kwasababu polisi ndio mamlaka ya uchunguzi wa kijinai
View: https://youtu.be/CH1amKvbsQc?si=j3eSmy1R1KctIuAb

Mnyika alichomoa!.
Ukweli ni huu
1. Hakukuwa na forgery yoyote ndio maana Chadema hawakuripoti popote jinai ya forgrey
2. Barua iliyowaigiza hao 19 Bungeni, ilikuwa barua bonafide genuine, ndio maana wamemaliza miaka yao mitano Bungeni.

P

Paskali unajichanganya mwenyewe, Mnyika majibu yake yamenyooka kama rula.
Ametumia reference nzuri ya assassination attempt ya Lissu, hivi polisi upelelezi wao umefikia wapi? Huwa wanafanya press conference hata kwa matukio ya wizi wa simu au wizi wa kuku hili la Lissu huu ububu unatoa picha gani? As the old saying goes 'once bitten twice shy', kwa nini waendelee kukinga maji kwenye ndoo ambayo wameshabaini kuwa imejaa matobo yanayopitisha maji?
 
Naona Halima Mdee anapima upepo, miongoni mwa wabunge maalumu wapo wake wa viongozi Chadema ilichelewa kufanya maamuzi magumu kuwatosa hao wabunge na mabwana zao
 
Back
Top Bottom