Hoja hizi zinajadilika sana, kwa bahati mbaya muda wa kutuliza akili juu yake ni shida sana.
Akina Halima ni swala ndani ya chama moja kwa moja. "Uchafuzi" uliofanyika 2020 ni zaidi ya CHADEMA, ni swala la nchi nzima. Mhusika mkuu wa 'uchafuzi' kwa kudra za Mwenyezi hayupo tena. Hawa wasaidizi wake, wengine tayari wanamkana waziwazi.
Kuwaondoa akina Halima kwa ushiriki wao katika kukihujumu chama chao ni swala ambalo limo ndani ya uwezo wa chama chenyewe, bila ya kuhusisha watu wengine nje ya chama. Ni haki ya chama kufanya maamuzi wanayoona yanafaa, kama ilivyo haki ya chama hicho kuamua kutoitambua serikali iliyotokana na 'uchafuzi' au kuamua kushirikiana na serkali hiyo kutafuta suluhu ya maswala ambayo ni muhimu kwa taifa ili ule uchafuzi usijirudie tena.
Mbowe, kama kiongozi wa chama, anao wajibu wa kueleza na kushawishi viongozi wenzake na chama kwa ujumla kufanya maamuzi wanayoona yanafaa kwa kwenda mbele, na kutoshikilia yote yaliyopita.
Huu utakuwa ni uamzi utakaofanyika ndani ya chama hicho.
Nitakujibu kwa kila paragraph uliyoandika.
- Sawa, wakina Halima ni suala la ndani ya chama, na chama chao kimeshawashughulikia na kimemelizana nao. Uchaguzi wa 2020 ulioharibiwa ulikuwa ni wa kitaifa, sawa, lakini hata kama ulikuwa wa kitaifa, mbona kina Mdee wameadhibiwa kwa athari za uchaguzi huo?
Hata kama muhusika alifariki, hawa waliopo wanatakiwa kufuta makosa ya yule muhusika kwasababu alitoka ndani ya chama chao, na wengine wao walikuwa ndani ya serikali yake. Kutafuta suluhu lazima kuendane moja kwa moja na kufukia mashimo yaliyosababishwa na ule uchafuzu, ikiwemo kurudia uchaguzi mkuu.
- Hoja yako ya pili;
Kwanini basi, chama hicho kikae na yule aliyewasababishia matatizo ndani ya chama chao mpaka wakafukuzana, ili kutafuta maridhiano, lakini walishindwa kutafuta maridhiano na wale wanachama wake waliowafukuza?
Hapa unaonesha upendeleo, unaipenda sana serikali ya CCM iliyotuharibia uchaguzi, huku ukiwaona kina Halima walioadhibiwa kwa matokeo ya kuharibiwa uchaguzi ule ndio wenye makosa na kuadhibiwa na chama chao, coz ni suala lililopo ndani ya uwezo wa chama chao, unakosea.
Nakuona kuna jambo unalikwepa, hutaki hawa jamaa warudie uchaguzi, bila kurudia uchaguzi ni kutwanga maji kwenye kinu. CCM wataendeleza mazoea yao ya rafu za uchaguzi kila mwaka, labda wapunguze "scale" ya rafu hizo. Nataka tutafute solution ya hili tatizo moja kwa moja, ili wakae wakijuwa, wakiharibu tena uchaguzi, utarudiwa [fundisho].
- Hoja yako ya tatu;
Mbowe kama kiongozi wa chama aliyesimamia kufukuzwa kina Mdee, leo Mbowe huyo huyo arudi tena kukishawishi chama chake walegeze misimamo yao kuhusu matokeo ya ule "uchafuzi" wa 2020 nitamshangaa sana kwa ukigeugeu wake.
Jambo lolote linalohusu maamuzi ndani ya chama huamuliwa na vikao halali vya chama, Mbowe kama atapeleka hiyo agenda huko vikaoni asubiri jambo hilo lipigiwe kura.
Kama wengi watakubaliana na hoja yake, then wakumbuke athari zilizosababishwa na jambo hilo walilopigia kura, ikiwemo kuwafukuza wenzao chamani, wasiwe wabinafsi wa kuibembeleza serikali ya CCM.
NB.
Kati ya yote uliyoandika, nakuona unaikwepa sana hoja muhimu ya kurudiwa uchaguzi, kurudiwa uchaguzi ndio suluhisho la haya matatizo yote.
- Haki za walioporwa ushindi wao majimboni zitapatikana.
- Viti maalum watapelekwa wanaostahili.
Zaidi, pesa za kurudia uchaguzi sio za CCM na serikali yake, ni mali ya walipa kodi wa nchi hii, usiwahurumie hawa, waache wavune walichopanda.