Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Mahakama kazi yake ni kutafsiri yaliyopo kwenye katiba ya chama CHADEMA syo katiba ya CCM na ile ya Mwendazake.
Sasa katiba ya CHADEMA imetumika kuwafukuza mahakama ina mamlaka gani kuingilia yaliyopo ktk katiba ya CHADEMA.
Mahakama iridhie forgery?
Pyuuuuuuuf
Mkuu, unatakiwa kujua kua mahakama ndie muamuzi wa mwisho kwenye jambo lolote nchi hii.

Kwa hiyo wana haki ya kwenda mahakamani wakitaka. Kumbuka ishu ya Zitto.

Nachokisema, inawezekana mahakama ikakubaliana na uamuzi wa chadema 100% na hilo halina ubishi.

Ila kwa kitendo cha kwenda mahakamani, wanafanya mchezo wa kuchelewesha ama delaying techniques. Kwa hiyo hata Bunge haliwezi kuwafukuza maana bado ni wanachama hadi mahakama itoe majibu, tayari huo muda unakua umeenda na kama ni vikao vya bunge 2 ama 3 wnaakua wamekula hela zetu.

Tusubiri tuangalie.
 
Halima Mdee kukataa kuongea kuwa uhuni gani umefanyika inaonyesha anaenda mahakamani kupinga

Ngoma bado mbichi
 
Hawa watu hasa huyu Mdee bado sijajua kwanini walikubali kudanganyika wakasaliti maamuzi ya chama chao, kama kilikuwa kiburi cha uwepo wa mwendazake pole yao.

Kinachomkuta sasa hivi hakuna yeyote mwanye akili atakayemuelewa na utetezi wake, walipewa ruhusa ya kujitetea kwenye KK wakagoma kwenda.

Kile kiburi walichoonesha pale ndio ulikuwa uhuni wenyewe, na ule uhuni ndio umeleta hii hasira kwa wajumbe wa Baraza Kuu "kuwachinjia baharini" kwa kura zakutosha toka kwenye kila kanda.

Kama walikuwa na nafasi ya kuomba msamaha ilikuwa ni wakati ule, pale anagalau wangeweza kusikilizwa, lakini kugoma kwao kwenda kwa kisingizia cha kitoto "usalama wao" 'ile ilikuwa ni dharau kwa wajumbe wa KK.

Hakuna mjumbe kichaa wa KK wa kuwafanyia fujo, wamevuna walichopanda, sasa waende mahakamani kama wakipenda, ingawa naamini wanajua hata huko mahakamani hawatavuna heshima yoyote, simply wameshapotea.
 
Hawa watu hasa huyu Mdee bado sijajua kwanini walikubali kudanganyika wakasaliti maamuzi ya chama chao.

Kinachomkuta sasa hivi hakuna yeyote mwanye akili atakayemuelewa na utetezi wake, walipewa ruhusa ya kujitetea kwenye KK wakagoma kwenda.

Kile kiburi walichoonesha pale ndio ulikuwa uhuni wenyewe, na ule uhuni ndio umeleta hii hasira kwa wajumbe wa Baraza Kuu kuwachinjia baharini kwa kura zakutosha toka kwenye kila kanda.

Kama walikuwa na nafasi ya kuomba msaha ilikuwa wakati ule, pale anagalau wangeweza kusikilizwa, lakini kugoma kwao kwenda kwa kisingizia cha kitoto "usalama wao" 'ile ilikuwa ni dharau kwa wajumbe wa KK.

Hakuna mjumbe kichaa wa KK wa kuwafanyia fujo, wamevuna walichopanda, sasa waende mahakamani kama wakipenda, ingawa naamini wanajua hata huko mahakamani hawatavuna heshima yoyote, simply wameshapotea.
Ngawira....
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ndani ya Baraza hilo ni uhuni.

Matokeo ya jumla

Idadi ya wajumbe 423

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%

Huyu akili Hana,watu 357 wakukstae harafu unasema ni wahuni,!!!?huyu Binti hajafundwa kabisa!!
 
Weka picha inayowaonyesha wakiwa wamegoma
 
Mkuu, unatakiwa kujua kua mahakama ndie muamuzi wa mwisho kwenye jambo lolote nchi hii.

Kwa hiyo wana haki ya kwenda mahakamani wakitaka. Kumbuka ishu ya Zitto.

Nachokisema, inawezekana mahakama ikakubaliana na uamuzi wa chadema 100% na hilo halina ubishi.

Ila kwa kitendo cha kwenda mahakamani, wanafanya mchezo wa kuchelewesha ama delaying techniques. Kwa hiyo hata Bunge haliwezi kuwafukuza maana bado ni wanachama hadi mahakama itoe majibu, tayari huo muda unakua umeenda na kama ni vikao vya bunge 2 ama 3 wnaakua wamekula hela zetu.

Tusubiri tuangalie.
Wakienda mahakamani hawatalipwa tena na bunge, mpaka labda washinde kesi ndio watalipwa malimbikizo yao ya mishahara! ni sawa na kufukuzwa kazi, ukipinga mahakamani hulipwi mshahara mpaka ushinde kesi....
 
Sasa tunasubiria majina ya hao 19 wa mbadala hapo chadema wasije wakaleta kutafutiana ulaji
Huu uamuzi kama ukifanyika ndio unaenda kuwa mwanzo wa tatizo jingine, hapa zitakuja assumptions za kila aina toka kwa maadui wa Chadema.

Hapa utatumika ukanda, ukabila, mahusiank, dini, na sababu nyingine zote ili kuhalalisha kina Mdee wameonewa ili wawekwe watu wao.

Nawashauri Chadema wabaki na msimamo wao wa mwanzo, kutoyatambua matokeo ya ubunge na Urais wa 2020 na kutopeleka wabunge bungeni, kama shida ni ruzuku, waendelee kuokoteza mitaani kama wanavyofanya.

Kwangu ni bora kupitia machungu ili kulinda heshima, kuliko kubadili msimamo wako na kupata kingi huku ukijipotezea heshima, hapa wasiyumbe kimsimamo.

Hakuna namna wanaweza "substitute" maamuzi yao ya mwanzo kwa kupeleka majina mengine bungeni ikiwa athari za uchaguzi ule bado zipo mpaka leo, hata kama serikali imebadilika.
 
Back
Top Bottom