Huu uamuzi kama ukifanyika ndio unaenda kuwa mwanzo wa tatizo jingine, hapa zitakuja assumptions za kila aina toka kwa maadui wa Chadema.
Hapa utatumika ukanda, ukabila, mahusiank, dini, na sababu nyingine zote ili kuhalalisha kina Mdee wameonewa ili wawekwe watu wao.
Nawashauri Chadema wabaki na msimamo wao wa mwanzo, kutoyatambua matokeo ya ubunge na Urais wa 2020 na kutopeleka wabunge bungeni, kama shida ni ruzuku, waendelee kuokoteza mitaani kama wanavyofanya.
Kwangu ni bora kupitia machungu ili kulinda heshima, kuliko kubadili msimamo wako na kupata kingi huku ukijipotezea heshima, hapa wasiyumbe kimsimamo.
Hakuna namna wanaweza "substitute" maamuzi yao ya mwanzo kwa kupeleka majina mengine bungeni ikiwa athari za uchaguzi ule bado zipo mpaka leo, hata kama serikali imebadilika.