Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kua watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Points sana umeongea, yaan wewe no kichwaa 'na km Samia akiamua kuweka kifua hata hiyo kesi itapigwa danadana mpya 2025, yaan mwenye maamuzi hapo Samia 'na wala sio Mbowe 'na kamati kuu
 
Ndiyo maana Mahakama zipo kwa ajili ya kupambana na wahuni.

Mbunge Halima Mdee ameendelea kusisitiza yeye na wenzake 18 bado ni wanachama halali wa Chadema.

Kilichotokea kwenye kikao cha Baraza Kuu ni Uhuni.

Wabunge hao wana Haki ya Kikatiba kupinga Uhuni Mahakamani.
 
Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kua watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Katiba ua CHADEMA inazuia mtu kwenda mahakamani kwa masuala yanayohusiana na chama, labda kama masuala hayo ni ya jinai.

Hapo kwa suala la uwanachama wao, ndipo lilipoishia.
 
Ndugu yangu, kumbe hata basics za sheria huzijui kiasi hiki?

Ukishapatikana una hatia na chombo chochote kwa mujibu wa kanuni, katiba yenu au sheria, unaendelea kuwa na hatia (hata kama umekata rufaa), mpaka siku ile mahakama au chombo cha juu kinapotengua.

Hayo mawazo yako yangekuwa yapo hivyo, gerezani kusingekuwa na wafungwa, maana ingekuwa baada ya kuhukumiwa na mahakama, unakata rufaa, unakuwa huru, kusubiria hukumu ya rufaa!!

Ukishapatikana na hatia na mahaka ya mwanzo, ukahukumiwa kifungo, siku ile ile unafungwa, hata kama utasema unakata rufaa. Hata wakati rufaa yako inaendelea kysikilizwa na mahakama ya juu, wewe utaendelea kuwa mfungwa, mpaka siku ile mahakama ya juu itakapotengua ule uamuzi wa mahaka ya chini.

Mdee na wenzake wataendelea kuwa siyo wanachama, mpaka siku ambayo chombo kingine kitakuwa na uwezo wa kuwarudishia uwanacha wao. Na chombo hicho, hakipo kwa sababu katiba ya CHADEMA inatamka wazi kuwa mamlaka ya mwisho ya maamuzi kuhusiana na masuala ya wanachama na wanachama ni Baraza Kuu, na Mdee analijua hilo.
 
Shetani siku zote ana ushawishi.
Inahitaji imani thabiti kumshinda shetani.

Mwendazake alikuwa ni shetani mwenye vivutio vingi kwa yeyote atakayekubali kumsujudia. Wengi walianguka na kuangamia kwenye dhambi wakati wa uhai wake.

Fikiria waliokubali hata kuwaua, kuteka na kuwabambikia kesi binadamu wenzao ili kumfurahisha na kumridhisha Mwendazake, hapo ndipo utajua nguvu ya shetani.
 
Hakika kila mtu ana price tag
Halima nilikua namkubali sana aisee
 
Sasa tunasubiria majina ya hao 19 wa mbadala hapo chadema wasije wakaleta kutafutiana ulaji
Watapelekaje majina wakati walikataa uchaguzi haukuwa huru?
Au tumesahau?
Anyway,ebu tutibu majeraha ya uchaguzi na kazi ziendelee.
 
Mkuu, unaweza kunielewesha Zitto aliendeleaje kua mbunge wakati alikua kafukuzwa chadema?
 
Lakini wanaendelea kuwa wabunge hadi kesi iamuliwe ina maana Chadema hawatakuwa na uwezo wa kuteua wabunge wengine
Bora waendelee kukaa Bungeni kwa amri ya mahakama ila chama chao kimemaliza kazi yake kwa mujibu wa katiba.
 
Mtu husamehewa aliyeomba msamaha. Covi 19 wangeomba msamaha yaishe
 
Ukweli ni kwamba Mbowe na Mnyika wanajua wamewasaliti kina Mdee. Mawasiliano ya simu yapo na sauti. Subirini labda wasiende mahakamani.
Wangeyasema kwa wajumbe kuhusu huo uhuni na kuzitoa hizo sauti za akina Mnyika ushahidi kama sehemu ya rufaa. Wamekosa fursa nzuri ya kutetea hoja za rufaa zao
 
Wapange trip kwenda Chato kuhiji kisha Kongwa kuchunga mbuzi - maisha yanakwenda kwa kasi saana. Wanajua fika mama Samia hawezi kuwavumilia tena.
 
Mwache mzee Halima aendelee na ubishi wake this time atanyolewa vyuuzzz bila maji wala wembe.
 
Sio kweli, huwezi kufungua kesi ya kupinga matokeo ya Urais mahakamani.

Marais hawashitakiwi wakiwa madarakani au nje ya mdaraka.
 
HALIMA HALIMA...UMESHAWAPONZA WENZIO WAMEFUKUZWA CHAMA KWA TAMAA ZAKO HALIMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…