Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kuwa watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Mbowe juzi, kabla ya mkutano wao wa Baraza kuu, alikua (aliitwa) Ikulu akiongea na Rais. Sidhani kama hawakuongelea hili. Tusubiri........
 
Mtanzamo wangu.
Chadema kupitia Mwenyekiti wake walishatangaza kuwa sasa ni lazima wafanye siasa za kuaminiàna.
Nadhani ni busara sasa Chadema kupeleka majina mengine ili hili swala sasa liishe. Cha msingi ni kuchagua watu sahihi wenye uwezo. Ukizingatia kwa sasa Bunge ni live na hali ya kiuchumi ni mbaya hivyo hii ni nafasi ingine Chadema imeipata ya kuonyesha uwezo wao wa kuwatetea wananchi, uwezo wa kuonyesha mawazo mbadala ya namna gani ya nchi kujikwamua, nafasi ya kuianika serikali kama kuna maovu wametendeka.

Hii nafasi Chadema waitumie vyema na wachunge mtego, wachague watu sahihi wenye uwezo madhubuti.
Umeandika vyema sana
 
Picha ipi tena? kama waligoma kwenda wakajifungia vyumbani kwao ulitaka niende kuwapigia huko? wewe uliwaona kwenye KK wakijitetea? naona bado umelewa usingizi endelea kulala.
Hawa ni wale ambao Zitto aliwaambia waende Chato wakachimbe pembeni wajizike. Huyu hapa hawatetei hawa Covid 19, bali anatetea Legacy ya Jiwe. Kwa sababu Jiwe ndiye aliyetengeneza huu uchafu, kwahiyo hapo anajaribu kuuona siyo uchafu ili kulinda legacy ya mwendazake.

Cc YEHODAYA na mwingine chinembe
 
Viti maalum wanawakilisha wananchi gani?

Kama mnataka wananchi wapate wawakilishi CCM na serikali yake warudie uchaguzi mkuu, hii kwangu ndio better option ili kufuta ule ujinga wa 2020, lakini sio kuwaliwaza CCM kwa ujinga wao waliofanya makusudi.
Mkuu mbona kama unaumia sana kina halima kufukuzwa? Wewe baki na ushauri wako ila wawakilishi bungeni lazima wapelekwe!
 
Shida ni kwamba kuna vitu kama nchi itapoteza. Je nchi ipoteze karibu 2 T kwa CHADEMA kuendelea na msimamo?
Kwa nini nchi (serikali) ilifanya faulo kwenye uchaguzi wa 2020 hadi kuanza kutoa watu magerezani usiku na kuwasafirisha usiku kwa usiku zaidi ya km 100, wakaapishwe garage ili wawe "wabunge"??
 
Waendelee kuwa wabunge hakuna mwenye shida na hilo bunge kibogoyo, cha muhimu maamuzi yameshachukiliwa. Suala la wao kuwa wabunge tayari walishapewa na Magufuli.
Safi sana. Hiyo ni ngumi ya pua.
 
Viti maalum wanawakilisha wananchi gani?

Kama mnataka wananchi wapate wawakilishi CCM na serikali yake warudie uchaguzi mkuu, hii kwangu ndio better option ili kufuta ule ujinga wa 2020, lakini sio kuwaliwaza CCM kwa ujinga wao waliofanya makusudi.
Mkuu, naona umewataiti mbaya. Kwa nini hawaamini kwamba uchaguzi wa 2020 chini ya mwendazake, uliharibu nchi?
 
Hapa patamu sana.

Ok, tukisema tumewasamehe CCM kwa zile rafu walizofanya makusudi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, rafu ambazo zimesababisha leo hii wakina Mdee wamefukuzwa chamani tukiwaita wasaliti, kwanini basi na wakina Mdee wasisamehewe?

Kwangu, uamuzi wowote utakaosema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, basi lazima uende moja kwa moja na kusamehe na kutibu yale majeraha yote yaliyosababishwa na kosa la msingi [rafu za uchaguzi 2020].

Je, utakuwa tayari kuwasamehe kina Mdee ili tuanze wote kwa pamoja? if No, kwanini uwagomee kina Mdee lakini uwasamehe CCM kwa zile rafu zao za makusudi?

Yes, ni CCM coz wakati ule wakitufanyia uhuni, Samia alikuwa mgombea mwenza, kama alikuwa hataki yale maovu angejiondoa kugombea, lakini nae akasikika akisema; "hata kama wasipotupigia kura bado tutangazwa washindi"

Hayo maswali unayoyaogopa kwangu ni suala dogo, nimeona next time wamesema Chadema watakutana na CCM na serikali yake kwa pamoja, hapa lazima CCM wakubali makosa yao na wafanye jambo kuyafuta, sijui kwanini unawatetea wasirudie uchaguzi? why unawahurumia?

Ujinga walioufanya wakati ule una gharama kubwa, na gharama hizo ndio wakati wao kuzilipa, na pesa za uchaguzi sio zao, ni za walipa kodi wa nchi hii.
Hoja hizi zinajadilika sana, kwa bahati mbaya muda wa kutuliza akili juu yake ni shida sana.

Akina Halima ni swala ndani ya chama moja kwa moja. "Uchafuzi" uliofanyika 2020 ni zaidi ya CHADEMA, ni swala la nchi nzima. Mhusika mkuu wa 'uchafuzi' kwa kudra za Mwenyezi hayupo tena. Hawa wasaidizi wake, wengine tayari wanamkana waziwazi.

Kuwaondoa akina Halima kwa ushiriki wao katika kukihujumu chama chao ni swala ambalo limo ndani ya uwezo wa chama chenyewe, bila ya kuhusisha watu wengine nje ya chama. Ni haki ya chama kufanya maamuzi wanayoona yanafaa, kama ilivyo haki ya chama hicho kuamua kutoitambua serikali iliyotokana na 'uchafuzi' au kuamua kushirikiana na serkali hiyo kutafuta suluhu ya maswala ambayo ni muhimu kwa taifa ili ule uchafuzi usijirudie tena.

Mbowe, kama kiongozi wa chama, anao wajibu wa kueleza na kushawishi viongozi wenzake na chama kwa ujumla kufanya maamuzi wanayoona yanafaa kwa kwenda mbele, na kutoshikilia yote yaliyopita.
Huu utakuwa ni uamzi utakaofanyika ndani ya chama hicho.
 
Nashangaa Halima ni mgemi wa WAJUMBE....kamuulize Stev Nyerere atakwambia kila kitu


Kwa sisi chapter is closed.

HAKUNA BINADAMU ALIYE HAI WA KUIUA CHADEMA.
 
Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kuwa watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Zitto ana vingi sana vya kujifunza kwa Mbowe
Screenshot_20220512-120606_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom