Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

Mtanzamo wangu.
Chadema kupitia Mwenyekiti wake walishatangaza kuwa sasa ni lazima wafanye siasa za kuaminiàna.
Nadhani ni busara sasa Chadema kupeleka majina mengine ili hili swala sasa liishe. Cha msingi ni kuchagua watu sahihi wenye uwezo. Ukizingatia kwa sasa Bunge ni live na hali ya kiuchumi ni mbaya hivyo hii ni nafasi ingine Chadema imeipata ya kuonyesha uwezo wao wa kuwatetea wananchi, uwezo wa kuonyesha mawazo mbadala ya namna gani ya nchi kujikwamua, nafasi ya kuianika serikali kama kuna maovu wametendeka.

Hii nafasi Chadema waitumie vyema na wachunge mtego, wachague watu sahihi wenye uwezo madhubuti.
Tuna hoja kabla ya hilo.
Wafungwa/Mahabusu waliobambikiwa kesi za michongo wawe huru kwanza
 
Zitto kabwe alizungumza yoote kabisa kuhusu chadema kua nitakua mtu wa mwisho kutoka chadema akawa WA KWANZA
 
Hakuna uhuni zaidi ya kuwa msaliti wa chama ulichokivujia jasho na damu.

Kusaliti watu waliokuamini na kukuheshimu; hata ambao hawakuwa wanachama wa chama chako.
Aliteleza tu kibinadamu, alistahili msamaha
 
Ahahaa..mkuu umenigusa ..mwaka jana nikiwa mwenyekiti wa kwaya tukataka kuleta mapinduzi na katibu wangu ndani ya kikundi..mchungaji akatufukuza 😂😂😂😂😂😂
...mlitaka kujimilikisha kwaya mliyoikuta ?..😂😂😂
 
Hizo delaying technique zingeweza kufanya kazi zama zile mama hawezi ruhusu suala hilo lilete tension nchini na nchi ionekane ya ajabu huko ughaibuni simply kuwalinda hao kichwa ngumu walioshikilia msimamo wa kutoomba msamaha abadani na hakika wamevuna walichopanda.Ila wana nafasi ya kijiunga na vyama vingine ili waupate huo ubunge 2025
 
Mzee Mdee na Bibi Bulaya tunawaomba msikubali kirahisi, nendeni Mahakamani ili tujuwe ile barua ya kuwateua kuwa Wabunge iliandikwa kihalali na Chama chenu cha Chadema ama ilikuwa barua ya kihuni.

Kama ni ya kihuni wahusika washughiuljkiwe kwa mujibu wa Sheria za nchi na kama ni chama kiliandika wahusika wafahamike na wao pia hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 
Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kuwa watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Mbowe is on good terms with mama. Kazi iendelee .
 
Kuna wanao sema kwasababu CDM ilisema uchaguzi haukuzingatia haki haitambui mshindi kwahiyo wasifikirie kupeleka wabunge bungeni, yaani wasuse jumla.

Nawakumbusha, TANU kabla ya uhuru ilipata tatizo la kukubaliana namna ya kupiga kura iliyopendekezwa na serikali ya kikoloni.

Wengi walikataa kitu kiliitwa kura tatu.

Lakini kama kawaida Nyerere alishawishi TANU ikubali na waliitumia fursa kufikia malengo. Hebu tufukue historia hiyo vizuri. Wajuzi wailete hapa vizuri.
 
Memba, Makamba na Kinana waliitwa kuhojiwa na baadae maamuzi yalitolewa.

“Mpango huu ulikuwa ni adhabu kwanza halafu process (mchakato) nyingine zinaendelea na mimi nilijua mwezi mmoja kabla”.
 
Alitaka kuwakomoa vipi? Wameachiwa mwaka mzima wa kuwa wabunge au kusahihisha makosa yao. Wao hawakutaka kuachia ubunge. Mbowe kawakomoa kivipi? Unadhani wanachama wangelielewa Baraza lao kama lingeamua kuwasamehe na kuwaacha waendelee na ubunge wao? Kupanga ni kuchagua na wamevuna walichopanda.
Sasa wako huru kwenda Mahakamani, kujiunga na chama kingine, kustaafu au kujirekebisha. Wakiweka kiburi pembeni wanaweza kuomba msamaha na kuomba uanachama upya.
Ila kwa vile Tulia hawapendi basi nafasi zao zitatangazwa kuwa wazi fasta.

Amandla...
Kisa cha kulazimisha kuwavua uanachama haraka haraka ilikuwa ni nini?
 
Kwanza walishaga toa msimamo kwamba hawapeleki wabunge wa viti maalum kwa kuwa uchaguzi ulikuwa batili Sasa swala la kusema wataselect new mps hilo ni ngonjera tu
Mla ruzuku huyo ana msimamo gani kila siku kunywa juisi Ikulu na CCM ama kweli watizedi mmepigwa na kitu kizito. Sahizi aikaeli analamaba asali hutamsikia hata mara mona akifungua bakuli lake kukemea inflation na ufujaji wa kodi za wananchi
 
Aliteleza tu kibinadamu, alistahili msamaha
Angeacha kiburi basi?
Angesimama kama kiongozi na kujieleza mbele ya wajumbe, si alipewa nafasi au hakupewa?

Halafu haelezi lolote, anabaki kusema tu "Uhuni", sasa watu waelewe lipi?

Inasikitisha sana kwa binti kama huyu, aliyetokea kuonyesha msimamo thabiti kabisa katika anayosimamia, halafu mwishoni kabisa kuja kuporomoka namna alivyoporomoka bila hata ya maelezo!
Katika viongozi ndani ya CHADEMA, Halima nilimweka kati ya viongozi muhimu sana ndani ya chama hicho. Sasa hata haieleweki ni nini hasa kilichompata hata kabadilika kiasi kile, tena kwa muda mfupi kabisa!
 
Back
Top Bottom