Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 59
Habari za siku mingi wapendwa, nina wakati mgumu naomba mawazo yenu katika hili. Kwa kifupi shangazi yangu yaani dada wa baba yangu alitoka na boyfriend wangu wa kwanza. Hawakuwa wakifahamiana kabla, niliwatambulisha na sababu shangazi alikuwa kwa kiasi fulani karibu na mimi akazoeana na yule kijana. Ikatokea wakakutana SA wakaanza kuwasiliana na kutembeleana mwisho wa siku wakawa wapenzi! Waliporudi shangazi alijikausha, hakuniambia kwamba walikutana na kijana SA, kijana akaniambia walikutana briefly.
Miezi 2 baadae kijana alitukutanisha mimi na shangazi na akaniambia hawezi kuvumilia tena maana nafsi yake inamsuta kwa hiyo inabidi aniambie ukweli kuwa walikutana na shangazi walipokuwa SA na wakafanya waliyoyafanya, anajutiana tendo hilo na anaomba nimsamehe. Alijitahidi sana kuonyesha kujutia na kuomba msamaha kwa njia na lugha zote lakini kwangu ilikuwa ngumu kusamehe na kusahau - pengine nilikuwa bado mdogo kipindi hicho kuweza kuhimili na kukabiliana na masuala (sio matukio!) mazito kiasi hiki. Na huo ulikuwa mwanzo wa mwisho wa mahusiano yangu na kijana niliempenda na kuamini ananipenda pia.
Ni miaka 3 sasa toka tukio hili litokee, lakini kila mara nimejikuta narudia kuwaza na machungu yananijia upya... kimsingi nimewasemehe wote ingawa kwa huyu kijana bado siwezi hata kupokea salam yake... shangazi tumewahi kukutana mara moja kwenye kikao cha familia - aliniomba radhi na akaniomba yasifike kwa familia.
Sasa shangazi amepata internship huku niliko, ameniandikia anaomba niwe mwenyeji wake nimhifadhi kwa miezi 9 atakayokuwa huku, nashindwa nimjibu nini maana bado sijasahau yaliyotokea, nahofia anaweza kufanya jambo jingine hata kama sio kutoka na mchumba wangu maana anaonyesha kutojali masilahi ya wengine. Nabaki najiuliza nifumbe macho nimpokee? Nitaweza kuzuia hisia zangu kwake kwa kipindi chote hicho? Ushauri tafadhali.
Asanteni sana,