Haliniishi moyoni...

Haliniishi moyoni...

Habari za siku mingi wapendwa, nina wakati mgumu naomba mawazo yenu katika hili. Kwa kifupi shangazi yangu yaani dada wa baba yangu alitoka na boyfriend wangu wa kwanza. Hawakuwa wakifahamiana kabla, niliwatambulisha na sababu shangazi alikuwa kwa kiasi fulani karibu na mimi akazoeana na yule kijana. Ikatokea wakakutana SA wakaanza kuwasiliana na kutembeleana mwisho wa siku wakawa wapenzi! Waliporudi shangazi alijikausha, hakuniambia kwamba walikutana na kijana SA, kijana akaniambia walikutana briefly.

Miezi 2 baadae kijana alitukutanisha mimi na shangazi na akaniambia hawezi kuvumilia tena maana nafsi yake inamsuta kwa hiyo inabidi aniambie ukweli kuwa walikutana na shangazi walipokuwa SA na wakafanya waliyoyafanya, anajutiana tendo hilo na anaomba nimsamehe. Alijitahidi sana kuonyesha kujutia na kuomba msamaha kwa njia na lugha zote lakini kwangu ilikuwa ngumu kusamehe na kusahau - pengine nilikuwa bado mdogo kipindi hicho kuweza kuhimili na kukabiliana na masuala (sio matukio!) mazito kiasi hiki. Na huo ulikuwa mwanzo wa mwisho wa mahusiano yangu na kijana niliempenda na kuamini ananipenda pia.

Ni miaka 3 sasa toka tukio hili litokee, lakini kila mara nimejikuta narudia kuwaza na machungu yananijia upya... kimsingi nimewasemehe wote ingawa kwa huyu kijana bado siwezi hata kupokea salam yake... shangazi tumewahi kukutana mara moja kwenye kikao cha familia - aliniomba radhi na akaniomba yasifike kwa familia.

Sasa shangazi amepata internship huku niliko, ameniandikia anaomba niwe mwenyeji wake nimhifadhi kwa miezi 9 atakayokuwa huku, nashindwa nimjibu nini maana bado sijasahau yaliyotokea, nahofia anaweza kufanya jambo jingine hata kama sio kutoka na mchumba wangu maana anaonyesha kutojali masilahi ya wengine. Nabaki najiuliza nifumbe macho nimpokee? Nitaweza kuzuia hisia zangu kwake kwa kipindi chote hicho? Ushauri tafadhali.

Asanteni sana,

Annina


kama uliamua kusamehe samehe mara sabini kwani nambua kwamba usilipe baya kwa baya ni vyema kulipa baya kwa zuri
 
Pole sana Annie.
what ur aunt did is dishumanity against you!
but she gonna continue be your aunt!
allow her to be with u for those 9months,never show her any kind of negative reaction!
then tells her that you have forgiven her!.
by that way of displaying a loving heart to her,she will learn something and always gonna appreciate you.
remember -you can always fight with ur enemies by making them ur friends!
regards:-accept her to join wth u there,show her highly respect than ever,display a loving heart than ever,hide ur heart break that u got previously.
Then introduce before her ur lovingboy in a manner way,as you will to ur parents.
 
Pole Dada, BF wako huyo alikuwa hajatulia ndo maana alishindwa kuonyesha respect kwako. Ubinadamu ni kazi sana, unaweza kamilika katika area nyingi lakini chache ukawa si mkamilifu, Shangazi yako naye ni binadamu ana mapungufu yake. Unatakiwa kusahau kabisa habari zilizopita. Sisi wakristo tunaagizwa kusamehe saba nmara sabini, maana yake "as much as you can"
Naamini unamuamini mchumba wako, mkaribishe shangazi yako, akifika mueleze juu ya uamuzi wa wewe na mchumba wako kutaka kuishi pamoja. Mkumbushe mambo aliyoyafanya kuwa hukufuraishwa nayo, na pia umemkaribisha kwa sababu alijutia jambo alilolifanya na kwamba wewe ulimsamehe ndo maana hukuyafikisha kwenye familia. Pia mwambie kuwa una imani na yeye , na unatarajiwa kuwa anapenda kukuona una furaha maishani kama ambavyo wewe umeona kuwa ni muhimu kwa yeye kufanikiwa na kuwa na furaha, na ajue "you need her as much as she need u". Kama ni mtu wa kweli mwangalie machoni wakati mnaongea , macho yake yatasema kila kitu. Na likuishe Moyoni.
 
Nashukuru kwa maoni ninayoendelea kupata, kwa sasa nimetulia natafakari kwa kina, naomba Mungu aniongoze pamoja na michango yenu naamini nitafanya maamuzi ya busara. Kama nilivyosema awali, sina tatizo kumkaribisha kwangu, sina tatizo kumtambulisha kwa mchumba - tatizo ni namna ya kuishi kwa muda atakaokuwa hapa! Nisingependa kuishi maisha ya kuigiza - kwamba kila kitu kipo sawa kati yetu wakati si kweli, na sipendi pia kuishi nae katika hali ya kutomwamini kama ilivyo sasa.

Asanteni sana,

Annina
 
Msamehe kisha mtambulishe rasmi kwa b/f wako.sababu ya yote hayo ni nduguyo wa damu hata usipomkaribisha kwako bado anaweza akaja akapanga mahali na bahati mbaya wakakutana na bf wako bila kufahamiana na wakaweka mambo sana ukajikuta tena mmekutanishwa bila kujijua na hapo ndo kosa litakapokuwa lako kwelikweli.Tatizo hili mara nyingi husababishwa utokaji out mara kwa mara na kilauri kwa sana.hali hiyo usababisha ukaribu na kuondoa aibu na kutumia maneno yasiyofaa ambayo ktk hali ya kawaida hayapendezi masikioni
 
Back
Top Bottom