Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 59
- Thread starter
- #61
Asanteni sana kwa maoni yenu, ukweli nimefarijika baada ya kusoma mabandiko yenu. Najitahidi sana na kumuomba Mungu ili niweze kusamehe na kusahau maana hata mimi si mkamilifu - nimewahi na naendelea kuwakwaza wengine kwa namna moja au nyingine.
Tatizo si tu kumpokea na kuishi nae kwa muda atakaokuwa huku, tatizo ni kwamba mimi na yeye kwa sasa ni strangers - katika kipindi cha miaka 3 ndio tumewasiliana kwa mara ya kwanza , najiuliza tutaishije. Sina tatizo na mchumba wangu najua ana akili timamu na utashi, wasiwasi wangu ni namna tutakavyoishi - mimi nikiwa na mtazamo hasi juu yake na yeye akijitahidi kuthibitisha vinginevyo! kitu kingine ni kwamba anaonekana kujali masilahi yake zaidi - yuko tayari kufanya lolote ili yake yatimie (kuna alichokuwa anataka toka kwa yule kijana na alifanikiwa), kwa tabia hii kuna uwezekano mkubwa hata asiponiharibia mimi (naamini atajitahidi ktk hili) anaweza kuharibu kwa watu ninaofahamiana nao na kuwa kama ndugu zangu huku ugenini.
Kuhusu nafasi siwezi kumdanganya kwamba naishi kwa single room maana wengi toka huko wamewahi kufikia kwangu kwahiyo atakuwa na taarifa za kutosha. Kwa kifupi maswali mengi...
Asanteni sana kwa kunitia moyo, Mungu awabariki