Hallelujah! Nchimbi Ameokoka, Bwana Asifiwe!!!?

Hallelujah! Nchimbi Ameokoka, Bwana Asifiwe!!!?

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vitu sitaki kuamini hata kama vinaonekana kuaminika kwa wengine. Yaani, leo hii Emmanuel Nchimbi amegeuka kuwa shujaa wa upinzani ati kwa vile ameonekana kutetea Katiba Mpya na haki za binadamu. Yaani, huyu Nchimbi amekuwa ni mtetezi wa demokrasia nchini. Kwamba Nchimbi amekuwa kinara wa kutetea haki za wanaharakati kukosoa nchi yao.

Nimejikuta najiuliza hisia ya shangwe na furaha na hata kupokea kwa matumaini kauli za Nchimbi kulinganisha na ile ya Rais Samia zinatokana na nini. Inawezekana kweli Watanzania ni wasahaulifu hivi? Au watu wanafikiri CCM imebadilika kiasi hiki au watu wanaombea kuwe kweli kuwe na mgongano ndani ya CCM?

Ila kama kweli Nchimbi ameokoka kweli ...

AACHIE NGAZI, AJIUZULU KWANZA!!!
Sisi yeyote anayemsimanga na kumnyima usingizi Samia ni vizuri tu
 
Ila mbona kama wanakata mizizi yake ili abakie bila meno? Vita siku hizi inaweza kupiganwa ndani kwako.
 
4. EN kasema Katiba itakayotumika 2029 serikali za mitaa na 2030 uchaguzi mkuu! hapa ndipo ghilba ilipo.
EN anataka watu wa focus huko ili kutoa ahueni ya hali ilivyo, kisha atakuja na story nyingine ili kupata katiba watu waridhiane. EN hakuzungumzia kilichotokea oct 29. Hakuona uchafuzi wa amani! wala hakuona haki ikisiginwa.

Majuzi niliandika hayo hapo juu. Leo Wasira anasema njia mojawapo ya kupata katiba mpya ni kufanya maridhiano.
Nchimbi alitumwa tu kumwaga mtama wa Katiba halafu kuna ''strings attached'' ni lazima maridhiano
 
Gentleman,
makamu wa Rais Dr.Emmanuel John Nchimbi ni mtumishi wa umma wa waTanzania. Anafanya kazi kubwa na nzuri sana ya kumsaidia Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika utendaji wa serikali, lakini zaidi sana katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025-2030.

Yote anayozungumza leo Dr Emmanuel John Nchimbi, na yale alivyowahi kuyazunzumza kabla huko nyuma, yote yapo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, ambayo ndio inatekelezwa hivi sasa na serikali sikivu ya CCM chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan.

So,
there is completely nothing new, ni mapenzi ya dhati tu waTanzania wote wameamua kuyaelekeza kwa Dr.Emmanuel John Nchimbi, ambayo pasina shaka yoyote ndie atakae kua agenda ya waTanzania wote kwenye nafasi ya urais, mara baada ya Dr Samia Suluhu Hassan kuhitimisha awamu yake ya pili mwaka 2030.

Kuaminika na kukubalika kwa Dr. Emmanuel John Nchimbi ndani na nje ya CCM, ni turufu muhimu sana ya kuwaunganisha waTanzania wote, kupendana na kujiskia kama watoto wa baba na mama moja Tanzania licha ya utafauti wa dini au makabila.

hakuna haja wala sababu yoyote ile ya muhimu au ya maana ya kujiuzulu.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Jaribu kusoma tena hilo kitu leo,CCM ina wenyewe
 
Back
Top Bottom