Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

Halmashauri inayofuata kuwa jiji la 7 Tanzania ni


  • Total voters
    118
  • Poll closed .
Mpaka sasa nchi ina Idadi ya majiji sita, ambayo ni ;
  • Dar es Salaam
  • Mwanza
  • Tanga
  • Mbeya
  • Arusha
  • Dodoma
Ni miaka 3+ tangia kuongeza kwa Idadi ya majiji, ambapo Dodoma ilipandishwa hadhi na kuwa jiji. Mpaka kufika 2035 ni Manispaa/Mji upi utakuja kupandishwa hadhi na kuwa Jiji.
Manispaa/Miji hiyo ni,
  1. KINONDONI
  2. SONGEA
  3. KIBAHA
  4. MOROGORO
  5. BUKOBA
  6. KAHAMA
  7. IRINGA
  8. NJOMBE
  9. MOSHI
  10. SUMBAWANGA
Kwa mtazamo wako lipi ni Jiji linalofuata...!?

KUMBUKA
  • Hadhi ya Jiji hugewa Wilaya
  • Kuna mikoa ina majina sawa na mojawapo ya Wilaya zao
  • Mkoa mmoja unaweza kuwa na majiji mawili au zaidi.
  • Majibu ya wadau ,yatakusaidia kujua sehemu mpya ya kwenda kuwekeza.
  • Vigezo vikubwa vya kuwa Jiji ni Idadi ya watu + pato la Wilaya.
  • Majengo ya ghorofa siyo kipimo cha jiji,,

Hadhi za Wilaya kwa mpangilio wa ukubwa wa hadhi ni.
  • Halmashauri ya Wilaya
  • Halmashauri ya mji mdogo
  • Halmashauri ya mji
  • Halmshauri ya manispaa
  • Halmashauri ya Jiji
Njombe
 
Kahama haina miundombinu.. Lakini katika nchi nzima ndio mji pekee pamoja na ukuaji wa haraka, Manispaa imejitahidi Ku maintain access kwa taratibu za kimipango miji.

Squatter kahama ni chini ya asilimia 10-15 tuu.. Ukilinganisha na miji mingine mikubwa nchini
 
Mkoa Hauwi Jiji,ila Wilaya ndiyo huwa Jiji....
Wilaya ya Tanga ilikuja kuwa Jiji miaka ya 1970 by kipindi ilikuwa ina kubwa sana la fedha kutokana na mkonge na maelfu walikimbilia huko kutafuta ridhiki..
Mkoa mmoja unaweza kuwa na majiji mawili hata manne.
Halmashauri ndio hupewa hadhi hizo wilaya hubaki Kama zilivyo...ndio maana meya wa jiji NI mkuu wa madiwani..madiwani huunda halmashauri..
 
Back
Top Bottom