NTWENONU
Member
- May 6, 2019
- 8
- 4
INATIA KINYAA chama kinachojinasibu ni kikongwe na kilichokomaa kinachagua kiongozi wake kwa kigezo cha kuwa RAIS! Utamaduni na desturi isiyo na afya kidemokrasia inayompa Rais madaraka na maamuzi yasiyoweza kuhojiwa na yeyote. Tulitegemea kuwa CCM itakuwa imejifunza kupitia utawala uliopita lakini wapi! SI ajabu nchi yetu inaenda mrama kwa sababu chama kilichoshika hatamu za uongozi hakina maonoo chanya('kimekosa dira'HORACE KOLIMBA). Kweli kuna ulazima tena wa mwenyekiti wa CCM kuendelea kuwa ndiye Rais!? Kwani asipokuwa mwenyekiti atafanya nini!? Akifanya makosa mnamdhibiti kivipi na kinga zote alizowekewa na katiba yetu ? Bunge lenyewe ni la chama kimoja (CCM) na yeye ndo mwenyekiti wa vikao vyote vya juu vya chama kuna namna yoyote ya kumkosoa huyu(rais, Mteuzi wa majaji, amiri jeshi mkuu, mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, sehemu ya BUNGE(ana mamlaka ya kulivunja bunge wakati wowote na kuitisha uchaguzi mkuu na pia ni mteuzi pekee wa tume 'huru' ya uchaguzi ya taifa) hakika chama kongwe kimefeli kufanya mabadiliko chanya kwa ustawi wa demokrasia chamani na nchini kwa ujumla.