Katika taarifa yake kwa Umma ya tarehe 13, Desemba 2019. Chama Cha Mapinduzi kimeeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hiko imepokea na kuwasamehe wanasiasa kadhaa ambao ni
1. Nape Moses Nauye
2. January Makamba
3. John Ngeleja
Ambao walisamehewa na Mwenyekiti Taifa ambaye walimkashifu kupitia njia ya mtandaoni.
Pia imetoa taarifa kuwaita mbele ya Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama wanachama watatu ambao wamesikika wakimkashifu na kumsema vibaya Mwenyekiti Taifa. Wanachama hao ni
1. Yusufu Makamba (Katibu Taifa) Mstaafu
2. Abdulrahaman Kinana ( Katibu Taifa) Mstaafu
3. Bernard Kamilius Membe
Katika hao wanaoitwa kuhojiwa, namba moja na mbili wameshamaliza utumishi wao katika Chama hasa kuzingatia umri wao na nafasi walizotumikia.
Pia walipaswa kutumia uzoefu wao wa Katiba na Kanuni za CCM hasa linapokuja suala la kutoridhishwa mambo yanavyokwenda/endeshwa ndani ya Chama na jukwaa la kutolea maoni au malalamiko yao.
Bwana Membe ambaye ameonyesha ndoto ya kutaka kugombea urais kupitia CCM, inaonyesha azimio la kuitwa mbele ya Kamati ni kigingi kwa ndoto yake hiyo.
Natabiri yafuatayo yanaweza kutokea
1. KUHAMA CHAMA
Membe kuhama CCM na kujiunga upinzani ili kukwepa rungu la Kamati ya Maadili
2. KUONYWA
Kuhojiwa na kupewa onyo ambapo inaweza kumpa haueni ya kuomba uteuzi kupitia CCM kwa kiti cha Urais
3. KUFUKUZWA CHAMA
Kuhojiwa na kukutwa na hatia kisha kunyang'anywa kadi ya chama huku akipigwa marufuku kugombea nafasi yoyote ndani ya Chama au kupitia Chama.
Naamini wajuzi wa mambo wanaweza kutuchambulia zaidi hasa kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za CCM.
Uzi tayari
Sent using
Jamii Forums mobile app