Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Camilius kitanzani. Front page ya news paper ya kesho hahahah...

Tafadhari mwenye kujua wanounda kamati ya usalama na maadili ya Taifa ya chama cha Mapinduzi ni nani na nani wajameni?
 
Katika taarifa yake kwa Umma ya tarehe 13, Desemba 2019. Chama Cha Mapinduzi kimeeleza maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hiko imepokea na kuwasamehe wanasiasa kadhaa ambao ni

1. Nape Moses Nauye
2. January Makamba
3. John Ngeleja
Ambao walisamehewa na Mwenyekiti Taifa ambaye walimkashifu kupitia njia ya mtandaoni.

Pia imetoa taarifa kuwaita mbele ya Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama wanachama watatu ambao wamesikika wakimkashifu na kumsema vibaya Mwenyekiti Taifa. Wanachama hao ni

1. Yusufu Makamba (Katibu Taifa) Mstaafu
2. Abdulrahaman Kinana ( Katibu Taifa) Mstaafu
3. Bernard Kamilius Membe

Katika hao wanaoitwa kuhojiwa, namba moja na mbili wameshamaliza utumishi wao katika Chama hasa kuzingatia umri wao na nafasi walizotumikia.

Pia walipaswa kutumia uzoefu wao wa Katiba na Kanuni za CCM hasa linapokuja suala la kutoridhishwa mambo yanavyokwenda/endeshwa ndani ya Chama na jukwaa la kutolea maoni au malalamiko yao.

Bwana Membe ambaye ameonyesha ndoto ya kutaka kugombea urais kupitia CCM, inaonyesha azimio la kuitwa mbele ya Kamati ni kigingi kwa ndoto yake hiyo.

Natabiri yafuatayo yanaweza kutokea

1. KUHAMA CHAMA

Membe kuhama CCM na kujiunga upinzani ili kukwepa rungu la Kamati ya Maadili

2. KUONYWA

Kuhojiwa na kupewa onyo ambapo inaweza kumpa haueni ya kuomba uteuzi kupitia CCM kwa kiti cha Urais

3. KUFUKUZWA CHAMA

Kuhojiwa na kukutwa na hatia kisha kunyang'anywa kadi ya chama huku akipigwa marufuku kugombea nafasi yoyote ndani ya Chama au kupitia Chama.

Naamini wajuzi wa mambo wanaweza kutuchambulia zaidi hasa kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za CCM.

Uzi tayari

IMG-20191213-WA0117.jpeg
IMG-20191213-WA0099.jpeg
IMG-20191213-WA0097.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila ndoto hutimia

Km kuna mtu aliamini lazima awe Rais ni Salim
Huyu alikuwa kipenzi cha Nyerer,Lakini ndoto hazikutimia
 
Nyie makanali wa Jeshi na watumishi wa CCM, hamuwezi kudhalilishwa namna hii na nyie mkaenda kupiga magoti.
KUBALINI MFE KWA HESHIMA, VIZAZI VITAWAKUMBUKA, MSIENDE KUPIGA MAGOTI
Jamaa anapenda sana 'kupigiwa magoti'.

Inamfanya ajisikie wengine wote 'kusalimu amri' mbele yake.

'Total submission' kwa kila mtu ndio raha yake.
 
Membe akiitikia huo wito uchwara na mimi narudisha kadi ya ACT
Hata kinana na makamba watakuwa wamejizalilisha. Ila watakwenda lazima kwa sababu wana makando kando mengi mabegani mwao. Ngao yao ni uanachama wao wa sisihem, wakikosea step chama kikawafukuza basi hata maisha yao haya ya uzeeni yanaweza kugeuka na kuwa magumu sana tofauti na wanavyowaza.
 
Mojawapo ya vitu ambavyo Magufuli anavilazimisha kufanyika sasa hivi ni kuwa asiwepo mtu ambaye "hagusiki" ama iwe kwa sababu ya cheo chake, hadhi yake au historia yake. Ila ukishatengeneza mazingira ya namna hii hata huko mbeleni watu wengine nao watakuja kuitwa vile vile bila kujali hadhi, cheo au historia waliyowahi kuwa nayo.
 
Mojawapo ya vitu ambavyo Magufuli anavilazimisha kufanyika sasa hivi ni kuwa asiwepo mtu ambaye "hagusiki" ama iwe kwa sababu ya cheo chake, hadhi yake au historia yake. Ila ukishatengeneza mazingira ya namna hii hata huko mbeleni watu wengine nao watakuja kuitwa vile vile bila kujali hadhi, cheo au historia waliyowahi kuwa nayo.
u
kabisa,
uko sahihi,na hii imesaidia sana kuondoa umimi,ujuaji na kujinafasi
as long as hakuna atakayemwita jpm huko mbeleni,mwache awnyooshe hawa watu
heshima iwepo
 
TUKUBALIANE KITU KIMOJA

Snitching ni kosa kama unawasnitch watu uko nao group moja, hata kama the snitching is for the benefit of the nation, tuende mbali zaidi , kama chama likiikosea TANZANIA NZIMA KUSIWE NA WAKEUP CALLZ ZOZOTE ZILE KWA WATU WA NDANI MANAKE NI BORA UWALINDE MTU ZA NDANI KULIKO TAIFA... why ? hata hili ni gumu kulielewa ndugu zetu ? nasikitika sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom