Heshima ya nchi lazima irudi tujenge nchi yetu sote pamoja bila makundi wala ubaguzi. Hatuwezi kubembelezana na mtu yeyote awe wa CCM au Upinzani, tufike mahali tukubaliane wote kwa pamoja kufuata sheria ambazo tumejiwekea. Kuheshimu mamlaka bila kuvunja sheria nk. angalia UK wapiga kura wamewaadhibu wote waliokuwa wanabeza Brexit na leo hii Theresa May analia uchungu mkubwa maana Boris ameshinda kwa kishindo. Sio kwamba British tax payers wanamkubali sana bali kupeleka message kwamba wapiga kura ndio waamuzi wa kila jambo Serikalini.
JPM kama hafanyi kazi alizopewa na wapiga kura wake ataadhibiwa kwenye box la kura na wala sio majungu ya kwenye mitandao na mavikundi ambayo yalifikiri Tanzania ni yao pekee. Tusisahau makundi makundi hasa wakati wa JMK.