Wala hilo halijaanzia huko Mbeya ,Tunduma zipo tena 2 alafu hapo Mbeya kuna shule iko jirani na stand Kuu ilijengwa na Serikali miaka mingi na pia ziko pia mikoa mingine.
Kama unafuatilia utasikia wazuri huwa anazizungumzia hizo shule,pia zingine zilijengwa kama shule za mifano wakati wa Kikwete chini ya ufadhili wa Umoja wa Umoja wa Mataifa kama pilot project ya malengo ya Millenia.
Sema hivi ,kumeanza kuzuka huo mtindo kwa Halmashauri kujenga shule za mchepuo wa Kiingereza kwa kutumia pesa za walipakodi afu kwenye udahili zinageuzwa za biashara na chanzo cha mapato kwa Halmashauri husika.
Hii tabia haiwatendei haki walipakodi wote na inakuwa leta conflicts of interests na sekta binafsi.Kazi ya serikali ni kutoa huduma sio kufanya biashara.
Athari yake ni kwamba watoto wa maofisa na watu wenye uwezo ndio watasomesha watoto wao hapo huku Halmashauri husika ikitumia mapato waliyokusanya kutoka kwa wananchi kuhudumia vizuri hizo shule na kutelekeza shule zingine,zitafanywa bora liende.Hii sio sawa Kabisa na Serikali ipige marufuku.
Mwisho walimu wa hizo shule watakuwa wale wazuri na wako paid vizuri afu vilaza wanaletwa shule za kayumba ambako pia watoto wamerundikana madarasani hadi kukaa chini.