Halmashauri nyingine ziige hili la jiji la Mbeya kujenga English medium za Serikali

Halmashauri nyingine ziige hili la jiji la Mbeya kujenga English medium za Serikali

Wala hilo halijaanzia huko Mbeya ,Tunduma zipo tena 2 alafu hapo Mbeya kuna shule iko jirani na stand Kuu ilijengwa na Serikali miaka mingi na pia ziko pia mikoa mingine.

Kama unafuatilia utasikia wazuri huwa anazizungumzia hizo shule,pia zingine zilijengwa kama shule za mifano wakati wa Kikwete chini ya ufadhili wa Umoja wa Umoja wa Mataifa kama pilot project ya malengo ya Millenia.

Sema hivi ,kumeanza kuzuka huo mtindo kwa Halmashauri kujenga shule za mchepuo wa Kiingereza kwa kutumia pesa za walipakodi afu kwenye udahili zinageuzwa za biashara na chanzo cha mapato kwa Halmashauri husika.

Hii tabia haiwatendei haki walipakodi wote na inakuwa leta conflicts of interests na sekta binafsi.Kazi ya serikali ni kutoa huduma sio kufanya biashara.

Athari yake ni kwamba watoto wa maofisa na watu wenye uwezo ndio watasomesha watoto wao hapo huku Halmashauri husika ikitumia mapato waliyokusanya kutoka kwa wananchi kuhudumia vizuri hizo shule na kutelekeza shule zingine,zitafanywa bora liende.Hii sio sawa Kabisa na Serikali ipige marufuku.

Mwisho walimu wa hizo shule watakuwa wale wazuri na wako paid vizuri afu vilaza wanaletwa shule za kayumba ambako pia watoto wamerundikana madarasani hadi kukaa chini.
Tunduma shule gani mkuu?
 
Miaka ya 2000 mwanzoni jiji la Mbeya walijenga Shule ya Mkapa ambayo ni ya msingi lakini inafundisha kwa kiingereza, ada yake ni ndogo sana ukilinganisha na zile za private. Mpaka sasa wana shule 3 za aina hiyo na wana mpango wa kujenga zingine 3.

Kwa sababu kuanzia sekondari masomo ni kwa kiingereza nafikiri huu ni utaratibu mzuri katika kutoa elimu bora. Ingefaa halmashauri zingine kuiga jambo hili.
Brother hili swala lina advantage na disadvantage zake. Mimi nimesomea ualimu na naijua falsafa vyema kisiasa uchumi as related to education.
1.Kwa halmashauri hongeren Kwa kubuni miradi inayoongeza mapato Kwa halmashauri ya Jiji la mbeya.

2.watu waliobuni huu mradi hawasoma changamoto za huu mradi Kwa kina Kwa sababu zifuatazo

A. Serikali inaonyesha uwepo wa matabaka ya kiuchumi katika jamii. Watoto wa mtu wa kawaida(masikin) hawezi mudu gharama za hizo shule

B.Elimu inayotolewa na serikali ni huduma za kijamii kucharge tution fee ni kwenda kinyume na sera ya elimu( Elimu BURE)

Binafasi napongeza jitihada za halmashauri ya Jiji la mbeya ila tu ningependa kutoa pendekezo kuwa wanapokaa chini kubuni miradi basi miradi iendane na sera za central government (serikali kuu)
 
Ni kweli usemayo. Maana shule zinajengwa na kuhudumiwa kwa kodi lakini wenye pesa ndiyo wanafaidika, inaweza leta matabaka. Lakini pia nafikiri elimu ya msingi ipo chini ya serikali za mitaa, japo wanatakiwa kufuata sera za kitaifa lakini wana uhuru mkubwa wa kumodify mambo yao.

Ni jambo zuri sana lakini linachangamoto zake.
 
Back
Top Bottom