Halmashauri nyingine ziige hili la jiji la Mbeya kujenga English medium za Serikali

Tunduma shule gani mkuu?
 
Tunduma shule gani mkuu?
Tunduma TC pre and primary English Medium iko Mpemba njia ya Ileje.

Nyingine inajengwa pale Sogea unapopandisha Kilimanjaro upande ule uliokuwa na miti mingi ya misyeda/makazi ya maofisa usalama.
 
Brother hili swala lina advantage na disadvantage zake. Mimi nimesomea ualimu na naijua falsafa vyema kisiasa uchumi as related to education.
1.Kwa halmashauri hongeren Kwa kubuni miradi inayoongeza mapato Kwa halmashauri ya Jiji la mbeya.

2.watu waliobuni huu mradi hawasoma changamoto za huu mradi Kwa kina Kwa sababu zifuatazo

A. Serikali inaonyesha uwepo wa matabaka ya kiuchumi katika jamii. Watoto wa mtu wa kawaida(masikin) hawezi mudu gharama za hizo shule

B.Elimu inayotolewa na serikali ni huduma za kijamii kucharge tution fee ni kwenda kinyume na sera ya elimu( Elimu BURE)

Binafasi napongeza jitihada za halmashauri ya Jiji la mbeya ila tu ningependa kutoa pendekezo kuwa wanapokaa chini kubuni miradi basi miradi iendane na sera za central government (serikali kuu)
 
Ni kweli usemayo. Maana shule zinajengwa na kuhudumiwa kwa kodi lakini wenye pesa ndiyo wanafaidika, inaweza leta matabaka. Lakini pia nafikiri elimu ya msingi ipo chini ya serikali za mitaa, japo wanatakiwa kufuata sera za kitaifa lakini wana uhuru mkubwa wa kumodify mambo yao.

Ni jambo zuri sana lakini linachangamoto zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…