Halmashauri ya Chato yatoa mitumbwi miwili ili kusafirisha Wanafunzi bure katika Kisiwa cha Iyozu

Halmashauri ya Chato yatoa mitumbwi miwili ili kusafirisha Wanafunzi bure katika Kisiwa cha Iyozu

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Halmashauri ya Wilaya ya Chato imetoa mitumbwi miwili kwa ajili ya Kisiwa cha Iyozu ambayo itatumika zaidi katika kuwasafirisha Wanafunzi bure wakati wa kwenda Shule na kurejea nyumbani.

Diwani wa Kata ya Muungano, Charles Kapembe amesema mbali na kupelekwa mitumbwi hiyo, suluhisho la kudumu ni Serikali na Wadau wengine wa maendeleo kujenga shule kisiwani hapo ili kupunguza adha ya watoto kuvuka na mitumbwi ambayo wakati mwingine imekuwa ikizama na kutishia uhai wao.

IYOZU 1.jpg
Amesema hali hiyo itasaidia kuondoa utoro kwa Wanafunzi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakikwepa kwenda shule kutokana na changamoto ya usafiri.

Asilimia kubwa ya Wanafunzi hao wanasoma Shule ya Msingi Rubambangwe na Sekondari ya Rubambangwe.

Pia soma ~ Wanafunzi Kitongoji cha Iyozu (Chato) wanatumia mitumbwi kwenda Shule, wakishuka wanatembea Kilometa 4, hali hiyo imedumu kwa Miaka 10


IYOZU 2.jpg

IYOZU 3.jpg

IYOZU 4.jpg
​
 
Back
Top Bottom