Halmashauri ya Wilaya ya Chato imetoa mitumbwi miwili kwa ajili ya Kisiwa cha Iyozu ambayo itatumika zaidi katika kuwasafirisha Wanafunzi bure wakati wa kwenda Shule na kurejea nyumbani.
Diwani wa Kata ya Muungano, Charles Kapembe amesema mbali na kupelekwa mitumbwi hiyo, suluhisho la kudumu ni Serikali na Wadau wengine wa maendeleo kujenga shule kisiwani hapo ili kupunguza adha ya watoto kuvuka na mitumbwi ambayo wakati mwingine imekuwa ikizama na kutishia uhai wao.
Amesema hali hiyo itasaidia kuondoa utoro kwa Wanafunzi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakikwepa kwenda shule kutokana na changamoto ya usafiri.
Asilimia kubwa ya Wanafunzi hao wanasoma Shule ya Msingi Rubambangwe na Sekondari ya Rubambangwe.