Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Nikiwa mmoja wa Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha tunapongeza hatua ya kuanza kwa ukarabati wa Barabara ya Kibaha–Mpiji pamoja na Barabara ya Tankini–Muheza, kufuatia malalamiko niliyowasilisha kuhusu ubovu wa miundombinu hiyo.
Pia soma ~ Halmashauri ya Kibaha hizo Tsh. 420M za kuboresha Barabara, zimetumika katika Barabara zipi?
Wiki iliyopita nilichapisha andiko kupitia JamiiForums nikieleza changamoto za Barabara hizo ambapo nilisema Manispaa ilisema ilitenga Tsh milioni 30 kila kata lakini kata yetu hali imekuwa mbaya kwa muda mrefu.
Ambacho nimekishuhudia kwa sasa tunaona kazi za awali za ukarabati zinaendelea, ikiwemo kukwangua barabara na kusambaza vifusi kwa lengo la kuboresha hali ya miundombinu hiyo.
Sasa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na mamlaka nyingine zote zisiishie hapo kwa kuwa kuna taarifa badabara hiyo ni ya TARURA, kama ni hivyo basi washirikiane wote kwa faida ya Wananchi wote wakazi wa huku na wengine wanaokuja huku.
Pia soma ~ Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha: Tumetenga Tsh. 50 kuboresha barabara za Mtaa Kibaha Mwaka wa Fedha 2026/2027